Kuhusu mwanamke mjamzito aliemwambia mume wake akatumie kisu na mikasi kumzalisha, Chalamila ametoa utetezi hauna kichwa wala mdomo, wa hovyo kabisa!

Kuhusu mwanamke mjamzito aliemwambia mume wake akatumie kisu na mikasi kumzalisha, Chalamila ametoa utetezi hauna kichwa wala mdomo, wa hovyo kabisa!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Nimesikiliza utetezi wa Chalamila kuhusu kauli yake kwamba yule mama mjamzito aliemwambia kama hatoi Tshs 50,000 achukue bajaji aende kwa mume wake atumie kisu na mikasi kumzalisha ni wa ovyo, usio na lojiki na ambao hata mtu asieenda shule angeweza kufanya vizuri zaidi. Ni afadhali hata angekaa kimya.

Chalamila amebwabwaja tu wala hakuna alichosema cha maana kutuambia kwa nini, yeye kama kiongozi mwakilishi wa raisi, alitoa kauli kama ile ya kubeza, kudhalilisha na hata kumtukana mama ambae alikuwa akimlilia kuhusu kulazimishwa kutoa Tshs 50,000 ili apewe huduma ya kujifungua. Mtu yeyote mwenye akili hawezi kudhania kwamba huu ni utetezi unaotolewa na msomi wa Masters degree. Chalamila hata anagusia kwamba huyu mama mjamzito alishindwa kulipa Shsh 50,000 kwa sababu alimaliza fedha kwenye ngoma za vigodoro! In fact, hayo ni matusi kwa watu wasio na uwezo kwamba wanashupalia ngoma ndio maana hawawezi kumudu gharama za matibabu!

Ushauri wangu kwa Chalamila ni kwamba aache kiburi. Aombe msamaha kwa huyo mama mjamzito, kwa mume wake, kwa Rais Samia na kwa Watanzania wote kwa ujumla. In fact, kwa kauli ya Chalamila, kiongozi yeyote mwenye akili za kiasi angeandika barua ya kujiuzulu kwa Raisi Samia badala ya kusubiri kuondolewa. Kuendelea kujitetea ni kuwaambia wananchi alichosema ndio msimamo wa serikali ya Samia - kama huna hela ya kuchangia kujifungua mwambie mumeo achukue kisu na mikasi akuzalishe!

Na niseme wazi, Raisi Samia usipomchukulia Chalamila hatua yeyote basi utaonekana na watu wengi zaidi kuwa wewe ndio tatizo. Uchaguzi ni wako, umsuke Chalamila au umnyoe!

Hebu msikilize Chalamila wewe mwenyewe u-judge kama huu ni utetezi unaopaswa kutolewa na kiongozi kama Chalamila

Ona pia: CHADEMA amsheni watu kwa kauli za kina Chalamila kwa mjamzito kwamba kama hatoi Shs 50,000 arudi nyumbani mume wake amkate kwa kisu na mkasi ajifungue
 
Nimesikiliza utetezi wa Chalamila kuhusu kauli yake kwamba yule mama mjamzito aliemwambia kama hatoi Tshs 50,000 achukue bajaji aende kwa mume wake atumie kisu na mikasi kumzalisha ni wa ovyo, usio na lojiki na ambao hata mtu asieenda shule angeweza kufanya vizuri.

Chalamila amebwabwaja tu wala hakuna alichosema cha maana kutuambia kwa nini, yeye kama kiongozi mwakilishi wa raisi, alitoa kauli kama ile ya kubeza, kudhalilisha na hata kumtukana mama ambae alikuwa akimlilia kuhusu kulazimishwa kutoa Tshs 50,000 ili apewe huduma ya kujifungua. Mtu yeyote mwenye akili hawezi kudhania kwamba huu ni utetezi unaotolewa na msomi wa Masters degree. Chalamila hata anagusia kwamba huyu mama mjamzito alimwambia nimeshindwa kulipa kwa sababu nimemaliza fedha kwenye ngoma za vigodoro! In fact, hayo ni matusi kwa watu wasio na uwezo kwamba wanashupalia ngoma ndio maana hawawezi kumudu gharama za matibabu!

Ushauri wangu kwa Chalamila ni kwamba aache kiburi. Aombe msamaha kwa huyo mama mjamzito, kwa mume wake, kwa Rais Samia na kwa Watanzania wote kwa ujumla. In fact, kwa kauli ya Chalamila, kiongozi yeyote mwenye akili za kiasi angeandika barua ya kujiuzulu kwa Raisi Samia badala ya kusubiri kuondolewa. Kuendelea kujitetea ni kuwaambia wananchi alichosema ndio msimamo wa serikali ya Samia - kama huna hela ya kuchangia kujifungua mwambie mumeo achukue kisu na mikasi akuzalishe!

Na niseme wazi, Raisi Samia usipomchukulia Chalamila hatua yeyote basi utaonekana na watu wengi zaidi kuwa wewe ndio tatizo. Uchaguzi ni wako.

Hebu msikilize Chalamila wewe mwenyewe u-judge kama huu ni utetezi unaopaswa kutolewa na kiongozi kama Chalamila

Ona pia: CHADEMA amsheni watu kwa kauli za kina Chalamila kwa mjamzito kwamba kama hatoi Shs 50,000 arudi nyumbani mume wake amkate kwa kisu na mkasi ajifungue
Mkuu wa Mkoa ameshindwa ku act kama kiongozi badala yake ame act kama muhuni na mvuta SHISHA! Shame!
 
Mie nimemuelewa. Ebu imagine mkeo ana uchungu wa kujifungua, kaambiwa hawana gloves lipua 50,000/=. Hivi inskuingia akilini kwamba badala ya kutoa hela hizo utachukuacsimu kupiga kwa Mkuu wa Mkoa kweli, huku pia ulijiunga na Mtandao wa Maria Sarungi? La pili, umeenda hospitali baba yako mahututi, ukapokelewa, madaktari eakapambana juu chini lakini Mungu hakupenda ukakuta Dad amekufa. Kweli utakataa kulipwa deni la matibabu ya baba yako usingizie mdaiwa amekufa? Kwa kifupi, Watanzania hatuko hivi.
 
Mkuu acha hilo,!!! Usipende kutetea uongo. Kuna gloves za 50,000? Hata kama zipo, nami nikawa sina fedha, umejuaje nimezimalizia kwenye vigodoro? Mkuu wa Mkoa aombe radhi, full stop.
 
Back
Top Bottom