Kuhusu mwanamke mjamzito aliemwambia mume wake akatumie kisu na mikasi kumzalisha, Chalamila ametoa utetezi hauna kichwa wala mdomo, wa hovyo kabisa!

Kuhusu mwanamke mjamzito aliemwambia mume wake akatumie kisu na mikasi kumzalisha, Chalamila ametoa utetezi hauna kichwa wala mdomo, wa hovyo kabisa!

Huyu ni mkuu wa mkoa wa ajabu sana, kiufupi hana akili
 
Nimesikiliza utetezi wa Chalamila kuhusu kauli yake kwamba yule mama mjamzito aliemwambia kama hatoi Tshs 50,000 achukue bajaji aende kwa mume wake atumie kisu na mikasi kumzalisha ni wa ovyo, usio na lojiki na ambao hata mtu asieenda shule angeweza kufanya vizuri zaidi. Ni afadhali hata angekaa kimya.

Chalamila amebwabwaja tu wala hakuna alichosema cha maana kutuambia kwa nini, yeye kama kiongozi mwakilishi wa raisi, alitoa kauli kama ile ya kubeza, kudhalilisha na hata kumtukana mama ambae alikuwa akimlilia kuhusu kulazimishwa kutoa Tshs 50,000 ili apewe huduma ya kujifungua. Mtu yeyote mwenye akili hawezi kudhania kwamba huu ni utetezi unaotolewa na msomi wa Masters degree. Chalamila hata anagusia kwamba huyu mama mjamzito alishindwa kulipa Shsh 50,000 kwa sababu alimaliza fedha kwenye ngoma za vigodoro! In fact, hayo ni matusi kwa watu wasio na uwezo kwamba wanashupalia ngoma ndio maana hawawezi kumudu gharama za matibabu!

Ushauri wangu kwa Chalamila ni kwamba aache kiburi. Aombe msamaha kwa huyo mama mjamzito, kwa mume wake, kwa Rais Samia na kwa Watanzania wote kwa ujumla. In fact, kwa kauli ya Chalamila, kiongozi yeyote mwenye akili za kiasi angeandika barua ya kujiuzulu kwa Raisi Samia badala ya kusubiri kuondolewa. Kuendelea kujitetea ni kuwaambia wananchi alichosema ndio msimamo wa serikali ya Samia - kama huna hela ya kuchangia kujifungua mwambie mumeo achukue kisu na mikasi akuzalishe!

Na niseme wazi, Raisi Samia usipomchukulia Chalamila hatua yeyote basi utaonekana na watu wengi zaidi kuwa wewe ndio tatizo. Uchaguzi ni wako, umsuke Chalamila au umnyoe!

Hebu msikilize Chalamila wewe mwenyewe u-judge kama huu ni utetezi unaopaswa kutolewa na kiongozi kama Chalamila


Ona pia: CHADEMA amsheni watu kwa kauli za kina Chalamila kwa mjamzito kwamba kama hatoi Shs 50,000 arudi nyumbani mume wake amkate kwa kisu na mkasi ajifungue
Kwa akili yake huu ndo anaita Ufafanuzi? Kwa mwanamke akitumia hela vibaya ndo akapasuliwe na mumewe?
 
Huyo ni kichwa maji, elimu yake haijamtoa ushamba, kichwa chake hakina uwezo wa kuchakata kipi azungumze kipi ameze.
Kwa viongozi wa namna hii hatuwezi fika mahali.
 
Hivi kuzaa si wanasema ni bure
Sio bure na haijawahi kuwa bure ila kuna kipindi ilikuwa afadhali kuliko sasa.
Masikitiko ni kauli ngumu isiyo na uweledi kutoka kwa mtu ambaye ni mkuu wa ulinzi na usalay wa mkoa mkubwa na wa mfano wa dar es laam.
 
Basi ndio maana anazidi kuropoka, maana alishatikisa kiberiti akaona hakina njiti ndani, mteuzi hana kauli kwake, labda anajua siri zake je?
Mteuzi hana nguvu akimuona RC Chalamila
 
Huyo ni kichwa maji, elimu yake haijamtoa ushamba, kichwa chake hakina uwezo wa kuchakata kipi azungumze kipi ameze.
Kwa viongozi wa namna hii hatuwezi fika mahali.
Lakini ndo ukweli Sasa mtu huna uwezo wa kutoa elfu 50 ya huduma ya kujifungua huyo mtoto utaenda kumlea vipi atakula Nini?
 
Alivyokuwa RC mwanza mama alimpiga benchi akaenda ikulu analia makamasi yanamtoka kama mtoto kuomba msamaha
Nakumbuka! Mama alikuwa anafanya zira akawaambia watu wako huru kuandika mabango ya ujumbe, hata wakitaka kutukana sawa tu!
 
Mkiambiwa ukweli hamtaki, sasa mnataka muendelee kudanganywa kama tunavyodanganywa na CCM kwa zaidi ya miaka 60 tungali masikini
 
Katika RC wa hovyo ni huyu mm sijajua kwanini Rais alimrudisha katika wadhifa huo baada ya kumuengua.
Ni mropokaji asiyeweza kufuatilia mambo ya msingi kwa faida ya wananchi.DSM sasa hivi ni shaghala baghala kila kitu kama vile hamna utawala.
Leo nimepita njia ya mabibo sokoni nikajikuta natusi serikali kwa sauti nikiwa ndani ya gari.
Yani vituo vya daladala pale sokoni ni wamachinga wa ndizi wamepanga ndizi na kituo cha upande wa pili ni boda boda wamepaki hivyo daladala zinasimama katikati ya barabara.
Kutoka NIT mpaka ufike zile taa za kuunga moro Road nimetumia dakika 25 wakati ni kipande cha mita 120.
Sasa unajiuliza hii serikali ipo kweli?
Mama anapaswa ajue huyu anasaidia kupunguza kura za ccm .
 
Lakini ndo ukweli Sasa mtu huna uwezo wa kutoa elfu 50 ya huduma ya kujifungua huyo mtoto utaenda kumlea vipi atakula Nini?
Una umri gani mzee!? Kuna watu elfu 5 ya kula wanaibahatisha, ila kuipata 50 ndio kimbembe, jamani tembeeni muone hali zilivyo nchini.

50 unaitaja eazy tu, kuna watu 50k ni kipengele kikubwa kwake.
 
Back
Top Bottom