Kuhusu Nyerere kutangazwa mtakatifu: Kanisa Katoliki mnataka watu wamwige Nyerere kwa lipi hasa? Umaskini, udikteta, ujamaa, ucheshi au nini hasa?

Kuhusu Nyerere kutangazwa mtakatifu: Kanisa Katoliki mnataka watu wamwige Nyerere kwa lipi hasa? Umaskini, udikteta, ujamaa, ucheshi au nini hasa?

Na declare interest kuwa mimi ni mkatoliki wa kuzaliwa. Ila hili nafikiri kuna agenda fulani hivi, kwa viwango vyovyote hastahili na binafsi nimekwazika sana ila sina jinsi.
Mimi ni Mkatoliki, katika hili pia naona walakini. Sistahili kumhukumu Mwalimu kwasababu sifahamu mwenendo wake wa ndani na hata alivyomalizia maisha yake.

Lakini naona walakini kwasababu ya muonekano wake kwenye jamii, nikisoma historia za watakatifu wengi naona kabisa kulikua ni vingi vya kujifunza kwao kuanzia katika maisha ya kila siku waliyoishi na jamii zao. Sioni hilo kwa Mwalimu Nyerere, huwa nikisikiliza sifa zake kwenye hotuba ama makongamano mengi ni kama zimekaa kujipendekeza ama kuonesha alivyokua kiongozi mzuri na sio Mkristo mtakatifu.

Najua alishika vema imani yake Katoliki, kuweza kushiriki ibada ya misa takatifu kila siku pale St. Peters inadhihirisha hilo, lakini haitoshi kuwa mtakatifu.

Nakumbuka wakati mchakato unaanza, kabla hata hajapewa hadhi ya Mtu wa Mungu, watu walionesha kutokubaliana na jambo hilo, wengine wakaenda mbali hadi kusema tulipewa ishara juu ya jambo hilo kupitia vifo vya wenyeviti wawili waliopewa jukumu la kuongoza jopo hilo (Aliekua Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma, na aliekua Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Mwanza).
 
katika mojawapo ya story zake, alieleza namna alivyokutana na wazee wa bagamoyo, na mambo ya kishirikina, na anasema hata yeye mambo hayo alikuwa mtundu. nikajiuliza, kumbe wakatoliki mtu aliyekuwa mshirikina anaweza kuwa mtakatifu? au hata wao ni washirikina?
Mecheka khaaaaa!! 😂😂😂😂
 
"Heri uamini kama Mungu yupo usimkute kuliko kutokuamini ukamkuta" - Julius K. Nyerere
 
Muandikie Father Kitima katibu mkuu wa TEC.
Kama huna mawasiliano yake Google TEC utapata.
Karibu sana kanisa moja takatifu katoliki la mitume.
Kwani hao unaowaona leo wameandikwa kwenye biblia kuwa ni watakatifu unadhani hawakuwa binadamu na hawakuwa na mapungufu??
Kwanza may be tudefine utakatifu. Lakini kwa mwenendo wako, huko ni mabli kufikiri. May be ngoja nikupe rejea ujue kuwa Nyerere alikuwa tyrant! Tafuta kitabu hiki:
Julius K Nyerere
Servant of God or Untarnished Tyrant
by Ludovick S Mwijage
 
Nyerere anahusishwa na matambiko ya kitaifa: tambiko la Bagamoyo, tambiko la Zanziba na tambiko la Lindi, je Kanisa Katoliki mnataka tuige nini hasa kutoka kwa Mwalimu? Hata kama mambo haya ni hearsay tu, je hamuoni kwamba tayari ni chanzo cha makwazo?

Nyerere aliruhusu mtu kunyongwa wakati wa uongozi wake. Tangu ruhusa hii italewe, sio Mwinyi, Mkapa, Kikwete hata Magufuli na Samia wamewahi kusaini mtu anyongwe. Pengine hawa waweza kuwa watakatifu zaidi ya Nyerere kwa hili.
Mkuu Proved, asante kuni tag
fazili Nyerere alikuwa mchanungu kweli. Utakatifu wa Katoliki hausiani na kusaini death warrant, kama uliwahi kusikia kitu kinachoitwa WICCA, ma Papa wa Catholic wamefanya ukatili wa ajabu kwa binadamu, na bado ni watakatifu!. Yale matukio ya matambiko hayo ni ya Kaisari.

Kati ya mchakato migumu duniani, ni mchakato wa Canonisation ya Catholic, Hatua ya kwanza ni kutangazwa Mwenye Heri, baada ya hapa sasa Wakristo wanatakiwa kusali na kuomba muujiza kwa jina la Julius Kambarage Nyerere, muujiza huo utokee, uthibitishwe ndipo awe Mtakatifu!. Sometimes it takes hundreds years and hundreds of years!. Mother Therese ndio amechukua shortest time recently. Foleni ni ndefu.

Ila pia kwenye Catholicism kuna vitu ni devilishly kama kufukiza ubani, kupakana majivu, mafuta ya upako, maji ya baraka etc, Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.
P
 
Hakuna aliyemkalifu, ila ni Mungu mwenyewe.

Utakatifu ni nini?
Ili uwe Mt. unapaswa kuwaje?
 
Tusubiri miaka 200 ipite lakini sasa ni mapema mno ndio maana nimeweza kuandika hivi kwani namjua Nyerere.
Nitakuelewa ikiwa hapa umemaanisha unamjua kwa sababu umekuwa ukimuona ktk picture na kumsikiliza ktk audio kumbukizi mbalimbali zilizohifadhiwa..........

Lakini siyo kwamba unamjua kwa kumuona matendo yake,maisha yake alivyoyaishi etc,haya mambo tunayakuza sana.
 
Hakuna aliyemkalifu, ila ni Mungu mwenyewe.

Utakatifu ni nini?
Ili uwe Mt. unapaswa kuwaje?
Mambo ya Nyakati 15:7 "Tukimaliza kazi, tutavishwa taji".
Hii inaonesha kwamba tukiishi maisha yanayotufanya tuwe watakatifu basi tutavishwa taji.

Rom 12:1
1 Petro 1:16
1 Thesalonike 4:3

Hizi zote zinaelezea kwamba tunatakiwa kuwa watakatifu kwasababu ya Baba yetu alie Mtakatifu.
 
Na declare interest kuwa mimi ni mkatoliki wa kuzaliwa. Ila hili nafikiri kuna agenda fulani hivi, kwa viwango vyovyote hastahili na binafsi nimekwazika sana ila sina jinsi.
Ukikwazika bila kuwa na sababu hiyo ni roho mbaya au huelewi taratibu za kanisa lako.

Hiyo ni mahakama ya kupokea ushahidi wa maisha mema na mabaya ya Nyerere. Ushahidi utakao patikana utafunga mjadala huo moja kwa moja au utausukuma mchakato kwenda hatua zinazofuata.
Kwa hiyo kama una ushahidi positive or negative upeleke kwenye mahakama hiyo, utapokelewa.
 
Ukikwazika bila kuwa na sababu hiyo ni roho mbaya au huelewi taratibu za kanisa lako.

Hiyo ni mahakama ya kupokea ushahidi wa maisha mema na mabaya ya Nyerere. Ushahidi utakao patikana utafunga mjadala huo moja kwa moja au utausukuma mchakato kwenda hatua zinazofuata.
Kwa hiyo kama una ushahidi positive or negative upeleke kwenye mahakama hiyo, utapokelewa.
Sababu zote zimetolewa na mtoa uzi nami namuunga mkono. Hakutakiwa hata kuanzishiwa hiyo process. Moja kubwa la wazi alisaini kunyongwa kwa Mwamwindi, achilia mambo mengine ya ovyo ovyo ya wanasiasa nawe wayajua.
 
Na declare interest kuwa mimi ni mkatoliki wa kuzaliwa. Ila hili nafikiri kuna agenda fulani hivi, kwa viwango vyovyote hastahili na binafsi nimekwazika sana ila sina jinsi.
Unajua historia ya hawa Paulo, mt. Dismas, Daudi, Musa, Augustine, Mathayo?
 
Kwamba licha ya Nyerere kuwa na mapungufu mengi, kumtangaza mtakatifu ni jambo ambalo litakuwa kikwazo zaidi kwa watu kuliko kuwa chachu ya maisha ya utakatifu. Kwanini msisubiri miaka 200 ipite ili watu wote wanaomjua "Nyerere wa kweli" wawe wamefariki ili kusiwe na scandalization yoyote kwa jamii na kumfanya Nyerere aonekane "The Legend"? Ni kosa kumtangaza mtu mtakatifu hata kabla mwili wake haojaoza kikamilifu kwani ni kikwazo kwa wale waliokuwa wakimfahamu fika wakati wa uhai wake. Huu ndio "utaratibu" wa magwiji wa Kanisa kufuatia uzoefu wao wa karne nyingi.

Nyerere anahusishwa na matambiko ya kitaifa: tambiko la Bagamoyo, tambiko la Zanziba na tambiko la Lindi, je Kanisa Katoliki mnataka tuige nini hasa kutoka kwa Mwalimu? Hata kama mambo haya ni hearsay tu, je hamuoni kwamba tayari ni chanzo cha makwazo?

CCM na uchafu wao wote wakati wa Nyerere na baada ya Nyerere ndio kitu kikubwa alichoacha Nyerere kwa Watanzania, na wote hata nyie mapadre na maaskofu mnajua kikundi hiki kinachoitesa nchi hii na kulifanya Taifa letu kuendelea kubaki katika lindi la umaskini na ufisadi mkubwa! Je Kanisa Katoliki mnafikiri kwamba kwa kumtangaza Nyerere kuwa mtakatifu sio kuwakwaza watanzania zaidi ya kuwapa mwanga?

Je katiba mbovu tuliyonayo sio matunda ya Nyerere? Juzi juzi maaskofu "mmetaabika" kukataa mkataba mbovu wa bandari, mambo hayo sio yanatokana na utamaduni mbovu wa usiri na katika mbovu iliyoasisiwa na Nyerere? Bado tu mnaona anafaa kuigwa au mmeamua kuwatafutia makwabwela "mtakatifu" wao?

Nyerere alijitahidi kuishi ukatoliki vizuri lakini hakufikia kiwango cha "utakatifu" wa kuigwa na jamii ya kitanzania. Kama ni kufa maskini licha ya kuwa rais, basi wapo wengi waliokufa maskini ambao nao walikuwa na madaraka makubwa serikalini.

Nyerere alifanya mambo mengi ambayo ndio yameifanya Tanzania kuwa nchi ya amani na umoja. Jambo hili halitoshi kumfanya mtu kuwa mtakatifu. Nyerere pia alifanya mengi ya kuwarudisha watanzania nyuma kimaendeleo, iwe ni kwa maksudi au kwa bahati mbaya. Leo hii kama nchi tumeendelea kuwa maskini kutokana na siasa na staili ya uongozi wa Nyerere. Kama Kanisa Katoliki linafikiri umaskini ni utakatifu, basi linalo sababu ya kumtangaza Nyerere kuwa Mtakatifu.

Nyerere aliruhusu mtu kunyongwa wakati wa uongozi wake. Tangu ruhusa hii italewe, sio Mwinyi, Mkapa, Kikwete hata Magufuli na Samia wamewahi kusaini mtu anyongwe. Pengine hawa waweza kuwa watakatifu zaidi ya Nyerere kwa hili.

Nyerere alibana baadhi ya makabila na kuyarudisha nyuma kimaendeleo na kuwafanya kuwa maskini. Leo hii taifa lipo huru zaidi kuliko wakati wa Nyerere ambapo yeye alikuwa kila kitu na kuvaa sura ya dikteta, a limiting figure.

Wapo wakristo wengi tu wenye heroic life (maisha matakafifu) tena kwa kuweka juhudi kubwa na jasho la damu. Nyerere hakuwa na juhudi za kipekee kuwa mtakatifu na alibebwa zaidi na nafasi yake kama rais.

Kanisa Katoliki mnafikiri Nyerere mwana wa kichifu na mtu aliyeishi ikulu muda mwingi wa maisha yake alikuwa kweli heroic katikati ya life securities alizo enjoy wakati wote wa maisha yake? Wale wengi ambao Nyerere aliwafanya kuwa maskini wakubwa leo hii wananyimwa hata kumunio takatifu na kuzikwa bila padre kwasababu ya umaskini wao, je bado mnataka tumwone Nyerere kuwa mtakatifu na atuombee kwa Mungu au sisi tumwombee kwa Mungu?

Marais wengi hutunukiwa tuzo mbalimbali kwasababu tu wapo katika nafasi ya urais. Nyerere halikadhalika anatunukiwa "utakatifu" kwasababu hizo hizo.

Kanisa Katoliki lijiulize hasa kwanini linataka kumtangaza Nyerere kuwa mtakatifu na kuacha hata kufanya utafiti kidogo juu ya wakristo wengi sana nchini wanaoishi "heroic life" kimyakimya. Je, ni kutafuta sifa ya kuwa na mtakatifu? Je ni kulifanya Kanisa Katoliki nchini kujulikana zaidi? Je ni political ambitions za baadhi ya wanajamii, mapadre na maaskofu kupata sifa juu ya mchakato huu?

Maaskofu mjiulize kwanini kati ya watawa na makleri lukuki wa Kanisa Katoliki hakuna juhudi kubwa kama hizi za kumtangaza Nyerere kuwa mtakatifu? Je ni siasa tupu?

Tunaojua madhara ya siasa za Nyerere katika maendeleo ya Tanzania tunaamini kuwa hakupaswa kufikia hatua hizo za kuelekea kwenye kutangazwa mtakatifu. Umaaruru wa mtu usiwekwe kwenye mchakato wa utakatifu, Kanisa linapaswa kutenganisha haya mambo.

Kanisa Katoliki liangalie zaidi nini matokeo ya kumtangaza Nyerere kuwa Mtakatifu kwa wale waliobakia hai na wanaomjua Nyerere na sera zake zilizoiachia Tanzania alama ya kudumu ya umaskini. Je Kanisa Katoliki mnataka hasa tumwige Nyerere kwa lipi? Umaskini, ucheshi, udikteta au nini hasa?

Je maaskofu mnaamini kweli kwa Nyerere kuwa mtakatifu kuna faida gani za kiroho au hata za kimwili kwa watu? Mnafikiri tunaongeza idadi ya "waombezi" wetu kwa Mungu? Au ni suala la kisiasa zaidi lisilo na faida kiroho wala kimwili? Je mnatazama na upande wa pili au kofia zenu zinawazuia kuona upande mwingine?
Msabato kunywa maji utulize hasira
 
Hata kumuabudu ni tambiko kama tunavyo abudu mizimu ya kizungu kila siku, st maria , st hellen, st peters st joseph hiyo yote ni mizimu na tunaiomba na kuiabudu ila wao wanao kuambia uabudu mzimu yao, wanakuambia USIIABUTU wala KUTAMBIKIA mizimu ya kwenu, sasa hapo nani atafanikiwa na kuendelea
 
wengine wakaenda mbali hadi kusema tulipewa ishara juu ya jambo hilo kupitia vifo vya wenyeviti wawili waliopewa jukumu la kuongoza jopo hilo (Aliekua Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma, na aliekua Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Mwanza).
Kwa hiyo mchakato umehamia jimbo kuu la Dar es Salaam ina maana kwamba Askofu Mkuu Jude Thadeus na wasaidizi wake Musomba na Mchamungu nao WATAKUFA?
 
Back
Top Bottom