Kuhusu Nyerere kutangazwa mtakatifu: Kanisa Katoliki mnataka watu wamwige Nyerere kwa lipi hasa? Umaskini, udikteta, ujamaa, ucheshi au nini hasa?

Na declare interest kuwa mimi ni mkatoliki wa kuzaliwa. Ila hili nafikiri kuna agenda fulani hivi, kwa viwango vyovyote hastahili na binafsi nimekwazika sana ila sina jinsi.
Mimi ni Mkatoliki, katika hili pia naona walakini. Sistahili kumhukumu Mwalimu kwasababu sifahamu mwenendo wake wa ndani na hata alivyomalizia maisha yake.

Lakini naona walakini kwasababu ya muonekano wake kwenye jamii, nikisoma historia za watakatifu wengi naona kabisa kulikua ni vingi vya kujifunza kwao kuanzia katika maisha ya kila siku waliyoishi na jamii zao. Sioni hilo kwa Mwalimu Nyerere, huwa nikisikiliza sifa zake kwenye hotuba ama makongamano mengi ni kama zimekaa kujipendekeza ama kuonesha alivyokua kiongozi mzuri na sio Mkristo mtakatifu.

Najua alishika vema imani yake Katoliki, kuweza kushiriki ibada ya misa takatifu kila siku pale St. Peters inadhihirisha hilo, lakini haitoshi kuwa mtakatifu.

Nakumbuka wakati mchakato unaanza, kabla hata hajapewa hadhi ya Mtu wa Mungu, watu walionesha kutokubaliana na jambo hilo, wengine wakaenda mbali hadi kusema tulipewa ishara juu ya jambo hilo kupitia vifo vya wenyeviti wawili waliopewa jukumu la kuongoza jopo hilo (Aliekua Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma, na aliekua Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Mwanza).
 
Mecheka khaaaaa!! 😂😂😂😂
 
"Heri uamini kama Mungu yupo usimkute kuliko kutokuamini ukamkuta" - Julius K. Nyerere
 
Kwanza may be tudefine utakatifu. Lakini kwa mwenendo wako, huko ni mabli kufikiri. May be ngoja nikupe rejea ujue kuwa Nyerere alikuwa tyrant! Tafuta kitabu hiki:
Julius K Nyerere
Servant of God or Untarnished Tyrant
by Ludovick S Mwijage
 
Mkuu Proved, asante kuni tag
fazili Nyerere alikuwa mchanungu kweli. Utakatifu wa Katoliki hausiani na kusaini death warrant, kama uliwahi kusikia kitu kinachoitwa WICCA, ma Papa wa Catholic wamefanya ukatili wa ajabu kwa binadamu, na bado ni watakatifu!. Yale matukio ya matambiko hayo ni ya Kaisari.

Kati ya mchakato migumu duniani, ni mchakato wa Canonisation ya Catholic, Hatua ya kwanza ni kutangazwa Mwenye Heri, baada ya hapa sasa Wakristo wanatakiwa kusali na kuomba muujiza kwa jina la Julius Kambarage Nyerere, muujiza huo utokee, uthibitishwe ndipo awe Mtakatifu!. Sometimes it takes hundreds years and hundreds of years!. Mother Therese ndio amechukua shortest time recently. Foleni ni ndefu.

Ila pia kwenye Catholicism kuna vitu ni devilishly kama kufukiza ubani, kupakana majivu, mafuta ya upako, maji ya baraka etc, Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.
P
 
Hakuna aliyemkalifu, ila ni Mungu mwenyewe.

Utakatifu ni nini?
Ili uwe Mt. unapaswa kuwaje?
 
Tusubiri miaka 200 ipite lakini sasa ni mapema mno ndio maana nimeweza kuandika hivi kwani namjua Nyerere.
Nitakuelewa ikiwa hapa umemaanisha unamjua kwa sababu umekuwa ukimuona ktk picture na kumsikiliza ktk audio kumbukizi mbalimbali zilizohifadhiwa..........

Lakini siyo kwamba unamjua kwa kumuona matendo yake,maisha yake alivyoyaishi etc,haya mambo tunayakuza sana.
 
Hii dunia ina maajabu sana. Niishie hapo.
 
Hakuna aliyemkalifu, ila ni Mungu mwenyewe.

Utakatifu ni nini?
Ili uwe Mt. unapaswa kuwaje?
Mambo ya Nyakati 15:7 "Tukimaliza kazi, tutavishwa taji".
Hii inaonesha kwamba tukiishi maisha yanayotufanya tuwe watakatifu basi tutavishwa taji.

Rom 12:1
1 Petro 1:16
1 Thesalonike 4:3

Hizi zote zinaelezea kwamba tunatakiwa kuwa watakatifu kwasababu ya Baba yetu alie Mtakatifu.
 
Na declare interest kuwa mimi ni mkatoliki wa kuzaliwa. Ila hili nafikiri kuna agenda fulani hivi, kwa viwango vyovyote hastahili na binafsi nimekwazika sana ila sina jinsi.
Ukikwazika bila kuwa na sababu hiyo ni roho mbaya au huelewi taratibu za kanisa lako.

Hiyo ni mahakama ya kupokea ushahidi wa maisha mema na mabaya ya Nyerere. Ushahidi utakao patikana utafunga mjadala huo moja kwa moja au utausukuma mchakato kwenda hatua zinazofuata.
Kwa hiyo kama una ushahidi positive or negative upeleke kwenye mahakama hiyo, utapokelewa.
 
Sababu zote zimetolewa na mtoa uzi nami namuunga mkono. Hakutakiwa hata kuanzishiwa hiyo process. Moja kubwa la wazi alisaini kunyongwa kwa Mwamwindi, achilia mambo mengine ya ovyo ovyo ya wanasiasa nawe wayajua.
 
Na declare interest kuwa mimi ni mkatoliki wa kuzaliwa. Ila hili nafikiri kuna agenda fulani hivi, kwa viwango vyovyote hastahili na binafsi nimekwazika sana ila sina jinsi.
Unajua historia ya hawa Paulo, mt. Dismas, Daudi, Musa, Augustine, Mathayo?
 
Msabato kunywa maji utulize hasira
 
Hata kumuabudu ni tambiko kama tunavyo abudu mizimu ya kizungu kila siku, st maria , st hellen, st peters st joseph hiyo yote ni mizimu na tunaiomba na kuiabudu ila wao wanao kuambia uabudu mzimu yao, wanakuambia USIIABUTU wala KUTAMBIKIA mizimu ya kwenu, sasa hapo nani atafanikiwa na kuendelea
 
wengine wakaenda mbali hadi kusema tulipewa ishara juu ya jambo hilo kupitia vifo vya wenyeviti wawili waliopewa jukumu la kuongoza jopo hilo (Aliekua Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma, na aliekua Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Mwanza).
Kwa hiyo mchakato umehamia jimbo kuu la Dar es Salaam ina maana kwamba Askofu Mkuu Jude Thadeus na wasaidizi wake Musomba na Mchamungu nao WATAKUFA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…