Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Ajira ni ipi
Kuna aina kadhaa za ajira zikiwemo:

Ajira ya kudumu - (permanent employment) ni ajira ambayo mwajiriwa hana woga wa kuachishwa au kuacha kazi ila tu anapopigwa kalamu kwa sababu ya makosa yake, afikishapo miaka ya kustaafu au kuacha kazi kwa hiari yake. Waajiriwa wa kudumu hufuata ratiba fulani na wanaweza kuwa wafanyakazi wa mchana kutwa (full time employment) au wa masaa machache (part-time employee).

Ajira ya mkataba - (contract employment) hii ni ajira ambayo mwajiriwa huajiriwa kufanya kazi fulani au kwa muda fulani na muda wake au kazi yake ishapo mkataba wake na mwajiri unaisha. Mwajiriwa wa mkataba huwa na uhakika, hawezi kuachishwa kazi kabla mkataba wake uishe, ila tu afanye makosa yasiyo weza kuvumiliwa. Pia yeye hawezi acha ile kazi kwa hiari bila kugharamia hasara yote inayoweza kutokana na kuvuja ule mkataba.

Ajira ya muda - (temporary employment) ni ajira ambayo mwajiriwa hufuata ratiba ya wafanyakazi wa kudumu lakini anaweza akaachishwa kazi wakati wowote. Mwajiriwa hana usalama wa kazi. Kibarua ni mfano wa ajira ya muda; ni ajira isiyo ya mara kwa mara na mtu huajiriwa tu kazi ipatikanapo na kazi ikiisha anaenda zake bila kujua kazi ingine itapatikana lini.

Ajira ya binafsi - (self employment) ni ajira ambayo mtu hujiajiri yeye mwenyewe
 
Bodaboda ni kazi kama kazi nyingine mbona huongelei walima na madaktari wazee, siajabu hako kasalari kako unakoingiza hakafikii kipato Cha huyo mzee
Na hakafikii… mtu tarehe 22 anaanza ulizia kama msg ishaonekana.
Ila hapa sasa kanataka jifanya matawi kudharau source of income za wengine.
9B409A4E-089A-46D8-9EED-A57C5E68CB6E.jpeg
 
Na hakafikii… mtu tarehe 22 anaanza ulizia kama msg ishaonekana.
Ila hapa sasa kanataka jifanya matawi kudharau source of income za wengine.View attachment 2230282
Huwezi kumlinganisha bodaboda na mtumishi wa umma kwa namna yoyote ile labda mtumishi wa umma mlevi.
Mimi ninadhaminika, naweza kupata milioni zaidi ya kumi bila barua ya udhamini kutoka kwa mwenyekiti.
Mimi nikiugua hata miezi kadhaa nitaendelea kulamba mshahara na posho , natibiwa kwa bima n.k
Nyumba yangu sijawahi kumuona bodaboda mwenye nyumba kama yangu.
Acheni ujinga, bodaboda ni last option
 
Habari!

Binafsi ninapomwona bodaboda mtu mzima mwenye miaka 50-60 napata mshituko kidogo na kuanza kuiogopa kesho yangu.

Najiuliza maswali yafuatayo;

1. Kayumba ukumbwani mpaka kaamua kuingia kwenye kazi za vijana wanaoishi vijiweni kutwakutwa kwa utani na matusi?
2. Atafanya hiyo kazi mpaka lini, na siku akiacha ataenda kufanya kazi gani?
3. Je, Mimi nikiyumba uzeeni nitafanya kazi gani?

NJE YA MADA

Vijana tijifunze kuwekeza kwenye shughuli ambazo zitaleta matunda baadaye na si kuangalia leo tu.
Kama shughuli gani?
 
Halafu akiumwa anafany nin, atafanya kazi , hizo hela atapata ,bodaboda anaweza kuamka asubuhi pikipiki imeibiwa , kazi haina security yoyote future ya kijana ambaye ni bodaboda ni kuja kuwa nani,mfano Mimi nalima na mkulima my future ni kwamba siku moja MUNGU akipenda nije kuwa mkulima mkubwa, unaweza shauri mwanao awe bodaboda
Na anaweza hata mzidi OP na take home yake.
 
Huwezi kumlinganisha bodaboda na mtumishi wa umma kwa namna yoyote ile.
Mimi ninadhaminika, naweza kupata milioni zaidi ya kumi bila barua ya udhamini kutoka kwa mwenyekiti.
Mimi nikiugua hata miezi kadhaa nitaendelea kulamba mshahara na posho , natibiwa kwa bima n.k
Nyumba yangu sijawahi kumuona bodaboda mwenye nyumba kama yangu.
Acheni ujinga, bodaboda ni last option
una shida kichwani. wewe kwa akili yako unajua ajira ni kuajiri tu? sasa serikali itaajiri watu wote, private sector itaajiri watu wote? kwani boda hakopesheki? kwani boda hawezi kuwa na bima?
mwajiri wako ana hasara kuwa na mtu kama wewe.

Kama suala ni kujiajiri mbona hujazungumzia barber shop, salun za kike, mgahawa,mama ntilie au ajenti wa bus. Wote hawa wamejiajiri
 
Kuna aina kadhaa za ajira zikiwemo:

Ajira ya kudumu - (permanent employment) ni ajira ambayo mwajiriwa hana woga wa kuachishwa au kuacha kazi ila tu anapopigwa kalamu kwa sababu ya makosa yake, afikishapo miaka ya kustaafu au kuacha kazi kwa hiari yake. Waajiriwa wa kudumu hufuata ratiba fulani na wanaweza kuwa wafanyakazi wa mchana kutwa (full time employment) au wa masaa machache (part-time employee).[1]
Ajira ya mkataba - (contract employment) hii ni ajira ambayo mwajiriwa huajiriwa kufanya kazi fulani au kwa muda fulani na muda wake au kazi yake ishapo mkataba wake na mwajiri unaisha. Mwajiriwa wa mkataba huwa na uhakika, hawezi kuachishwa kazi kabla mkataba wake uishe, ila tu afanye makosa yasiyo weza kuvumiliwa. Pia yeye hawezi acha ile kazi kwa hiari bila kugharamia hasara yote inayoweza kutokana na kuvuja ule mkataba.
Ajira ya muda - (temporary employment) ni ajira ambayo mwajiriwa hufuata ratiba ya wafanyakazi wa kudumu lakini anaweza akaachishwa kazi wakati wowote. Mwajiriwa hana usalama wa kazi. Kibarua ni mfano wa ajira ya muda; ni ajira isiyo ya mara kwa mara na mtu huajiriwa tu kazi ipatikanapo na kazi ikiisha anaenda zake bila kujua kazi ingine itapatikana lini.
Ajira ya binafsi - (self employment) ni ajira ambayo mtu hujiajiri yeye mwenyewe
Kwa tafsiri hii bodaboda ni ajira binafsi.
 
Back
Top Bottom