Kuifuta CCM sio kuondoa matatizo ya taifa hili. Hiyo ni propaganda yenye uongo Mkubwa

We jamaa Una akili Sana nafikiri wewe Una chembembe za Eastain.

Hii kitu umeelezea hapa ni 100%

Mimi jambo hill nililijua tangia mwaka 2015 nikabilidisha uelekeo wa siasa zangu.

Mkuu nilichoeleza wala hakihitaji akili nyingi Sana.
Wengi wanakijua na ni Jambo la kawaida.

Ubinafsi pia unahusisha Tabia ya kulaumu

Upo sahihi kabisa.
Hao viongozi WA CCM chimbuko lao ni familia zipi?
Au wanatoka mbinguni au nje ya nchi.
Familia za wanaccm ndio hizohizo familia za wanachadema na wasio na vyama.

Mambo ya nje mchango wao ni Mdogo na unategemea uthabiti wa tuliopo ndani
 
Unachosema ni kweli lakini ccm kama taasisi iliyoongoza hii nchi toka uhuru wana mchango mkubwa kwa kufail kutengeneza jamii inayochukia hayo matendo japo kwa asilia 80 tu.
 
TATIZO LA NCHI HII NI POLITICAL SUPREMACY na si hayo uliyoyasema..

Vyama vya siasa vimekuwa ni cult za watu wenye same interests wanaoendesha nchi kwa maslahi yao binafsi na si ya nchi.

Ubaya zaidi ni Nyerere ndiye alietengeneza hili, kwa kuhisi CCM yeye nguvu kubwa isiyomithilika, itamlinda yeye na nchi hii, pasipo kutengeneza mifumo kama katiba na mihimili ya serikali huru itakayoilinda nchi pasipo kujali ni nani atakuwa kwenye mamlaka.

Hii ndio sababu kuu

Na cha kusikitisha ni hicho, kama ambavyo magufuli alianza kusafisha aliyoyakuta ndani ya CCM na nchi ikatikisika kama Mizengo pinda alivyosema. Bhasi ni vivyo hivyo inahitajika group lingine lenye nguvu ya kuisafisha nchi pasipo kujali maslahi ya watu baadhi

And yes, siichukii CCM lakini nahisi wanatakiwa kuwekwa pembeni ili tupate balance of power.

Yes haitoondoa matatizo yote maana hata Marekani bado ina matatizo. Lakini itatupa new direction
 
Mimi ninachoamini ni kitu kimoja tu,nchi ili iendelee ni lazima iwe na mifumo imara ya kiungozi na kiutendaji,kwamba hata ikatokea akatokea kichaa mmoja kuwa kiongozi asiongoze nchi Kwa akili zake na matakwa yake, CCM hawataki Hilo litokee hata mara Moja Kwasababu wanataka kuendeleza koo na familia zao binafsi,hawaamini katika nchi.
Suala siyo CCM Wala upinzani,suala ni mifumo na ambaye alikuwa na nafasi kubwa ya kutengenezwa mifumo ya nchi ni CCM ndiyo maana tunasema matatizo ya Tanzania Kwa asilimia 90 yanatokana na kuwepo Kwa CCM.
 

Sahihi kabisa

Sasa hivi ukweli utakimbiwa hasa ukweli unaolenga kukukosoa. Ukweli wa kukukosoa watu hawataki.

Ndio maana MTU anakaa bunju unaenda kuswali Kimara
 
Si hiyo chadema uliyoisifia!!
Nimesifia kilichofanyika,Kwa sababu umezungumzia watendaji,watendaji hao hao walikuwepo wakati halmashauri zinaongozwa na CCM na tuliona madudu yao,Kwa hiyo hapa siwezi kusifia watendaji.
 
Unachosema ni kweli lakini ccm kama taasisi iliyoongoza hii nchi toka uhuru wana mchango mkubwa kwa kufail kutengeneza jamii inayochukia hayo matendo japo kwa asilia 80 tu.

Burundi CCM ipo? Au kuna CCM yakiburundi?
Zambia, msumbuji, Congo, vipi nchi za America ya kusini nako kuna CCM?

Hao CCM wanatoka kwenye familia za kitanzania.
Wapo waliokuwa chadema SASA hvi ni CCM. Na wapo walikuwa CCM SASA hivi ni chadema au hawana chama.

Tena kuna mwanaccm kama Lowasa alipewa mpaka Tiketi ya kuwania urais Chadema. Mtu ambaye alitajwa kwa ufisadi wa kutisha.
 
Na ndicho alichoongelea mtoa mada. Mifumo hiyo mibovu inaanzia ngazi ya familia. Ubinafsi ni mkubwa sana, kila mmoja anajiangalia yeye tu.

Baba anahitaji kuheshimiwa kwasababu tu yeye ni baba hata kama ni wa hovyo, mke anahitaji kupendwa,kusikilizwa na kuthaminiwa hata kama hatimizi wajibu wake. Mtoto pia anahitaji kusikilizwa na kutimiziwa mahitaji yake ilihali yeye hasikilizi wazazi wala kutimiza wajibu wake.

Kila mmoja anajiangalia yeye tu na maslahi yake binafsi. Hawa wote wakiwa viongozi lazima waendeleze tabia zao mbaya.
 
CCM hapa inawajibika kwa maana ya taasisi iliyopewa kujumu la kuiongoza nchi. Huko kwingine ulikotaja nao wana taasisi zao zilizopewa hayo majukumu.
Unadhani nani awe kiranja wa kuakikisha jamii inarudi kwenye mstari kuanzia ngazi ya familia. Kama baba au mama anakuwa chawa na anaona unalipa anaendesha familia yake vizuri, huyo mtoto atajifunza nini?
 
Mkuu, CCM hawajanza kuongoza Tanzania jana. Ni zaidi ya miaka 60 sasa.

Hiyo maana yake hawana sababu yoyote ya maana kujitetea au kusema aaah Chadema nao hawata weza wakipewa nchi. That’s a lame excuse
 

Magufuli hakuwahi kuondoa matatizo ndani ya taifa hili zaidi aliyaongeza kwa mfumo huohuo nilioueleza ingawaje weww umeona hakuna hoja.

Mfumo wa jamii unahitaji mabadiliko ya kimfumo ambayo yapo kwenye sheria na Katiba.

Katiba unayoiona matokeo yake makuu ni utamaduni ya jamii zetu na malezi yetu.
Ambapo Mkubwa hatakiwi kuwajibika kwa Makosa aliyoyafanya.
Kwamba Mzazi hakosei na kama hakoseu huwezi mshtaki.
Kwenye katiba desturi hiyo inaelezwa kama Rais hashtakiwi. Ila wengine mtashtakiwa.
Hiyo pekee ni ushahidi wa ukandamizaji wa wazi kabisa.

Magufuli angekuwa anataka kubadilisha nchi hii kimfumo hasa kwenye vipengele vya Sheria.

Siasa zinaathiriwa moja kwa moja na tamaduni za jamii husika.
 
Nakuhakikishia CCM imetufikisha hapa tulipo. Kama wangekuwa wanajitambua wangekuwa wamefanya makubwa. Kila idara haieleweke. Kwa rasilimali zilizopo nchi ingekuwa mbali sana hasa eneo la viwanda. CCM haina vision kabisa. Eneo lingine kwa mfano watanzania walioko Dar wanatunza mavi kwenye mashimo majumbani. Hakuna sewage system inayo eleweka.
 
Kuna mtu alisema hata sisi tunaolalamika ni kwakuwa hatujapata fursa, tukiipata tutakuwa the same🤔
Ndio maana tunataka katiba mpya na sio CCM tu kuondoka madarakani
 

Ni kweli kabisa.
Chadema wakiingia watajitutumua lakini CCM nao kwa kificho watakuwa wanawahujumu na kuwakwamisha ili ionekane wameshindwa.

Ndio yaleyale ya ubinafsi.
 
Usichanganye kuondoa matatizo ya nchi hii, na matatizo yaliyoletwa na ccm. Ukiifuta ccm matatizo makubwa yaliyoletwa na ccm ndani ya nchi hii yataondoka. Huenda unaelewa kuwa matatizo ya nchi hii yameletwa na ccm. Ni hivi, ndani ya nchi hii matatizo mengi yameletwa na uwepo wa ccm, na hayo yataondoka kwa kuiondoa ccm. Na hayo matatizo mengine ya taifa hili yataondolewa kwa njia nyingine. Jitahidi kwenye maandiko yako usiwe mpotoshaji.

Ertugrul Bey
 
Malezi mabovu tatizo, siku ile ya Oct29 baadhi ya hao wanaoitwa waandamanaji walikuwa wakisikika wakisema kabisa twende tukamtembelee Diamond, Twende tukamtembelee Jux yaani waliongozwa na roho mbaya wakataka wazimalize hasira na unyonge wao kwa kuharibu mali za wanamuziki ambao walitoka jasho miaka na miaka kufika pale walipofika.

Chuki na roho mbaya inayoletwa na uvivu wa kuumiza vichwa katika kufikiri zilikuwa sababu za uharibifu mwingi ndani ya siku zile mbili.

Mtu anasoma habari mbaya kuhusiana na mwanamuziki kwa muda wa mwaka mzima, ndani ya kichwa chake inatengenezwa chuki kwamba kufanikiwa kwa mwanamuziki huyo kuna mchango wa moja kwa moja katika umaskini alionao yeye mtu wa kawaida!.

Vijana wakachoma mabasi ya Ali Awadh wakidhani wanamkomoa Ridhiwani Kikwete!!, akili zao zimekuwa programed kwa mwaka mzima wa habari za kichochezi katika kufikiria kwamba adui yao ni mtoto wa Rais mstaafu.

Mange anatumia sana huu mtindo wa kutengeneza habari feki zinazohusu maisha ya watu maarufu ili awachonganishe na umma unaosoma habari zao, huyo dada hana uelewa kwamba fitina inapolipwa madhara huwakumba mpaka wale wasiohusika.
 
Mkuu, CCM hawajanza kuongoza Tanzania jana. Ni zaidi ya miaka 60 sasa.

Hiyo maana yake hawana sababu yoyote ya maana kujitetea au kusema aaah Chadema nao hawata weza wakipewa nchi. That’s a lame excuse

Mkuu chadema sio kwamba hawataweza au wataweza. Ninachoeleza hapo ni kuwa Chadema na ccm wote wanatoka kwenye jamii ileile ya Watanzania.
So kushindwa kuongoza au kuleta Maendeleo sio kwa sababu upo chama fulani. Bali ni suala la utamaduni(malezi) na ukoloni mamboleo.

Unajua hapa Afrika ni nchi ngapi zimebadili vyama vya siasa na bado maendeleo yakawa Stori za kufikirika?
Mfano Hapo Kenya.
 

Nipe matatizo matatu makuu ya nchi hii yaliyoletwa na CCM?

Mimi nitayakueleza mzizi wake upo wapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…