Kuifuta CCM sio kuondoa matatizo ya taifa hili. Hiyo ni propaganda yenye uongo Mkubwa

Nimesifia kilichofanyika,Kwa sababu umezungumzia watendaji,watendaji hao hao walikuwepo wakati halmashauri zinaongozwa na CCM na tuliona madudu yao,Kwa hiyo hapa siwezi kusifia watendaji.
Ndio maana nikasema upinzani wanacho cha 'kuprove" kwa jamii ndio maana wanapopata nafasi lazima waitumie vozuri ili kujenga imani.

Lakini misingi na mifumo mibovu ipo kila mahali na tumeijenga wenyewe kutokana na ubinafsi.

Hata chadema hawataki kukosolewa pale wanapokosea, wanahitaji kusifiwa tu. Yeyote mwenye mawazo mbadala anaonekana msaliti same as ccm.
 
Tindo tatizo lenu mnapenda kupindisha ukwel ila wananchi wana akili pia
unajua bob marley aliwahi kusema "you can fool some people some time, but you cannot full them everytime"

kama nyie ndo mnasema ukwel ama ccm wanasema ukwel basi, uhalisia utajitokeza, ccm ishafikaga sehem mbaya 2015 na wananchi walionyesha dhahiri hivo basi wacha wananchi waamue kama ccm iko sahihi ama nyie mko sahihi
 
Ni kweli kabisa.
Chadema wakiingia watajitutumua lakini CCM nao kwa kificho watakuwa wanawahujumu na kuwakwamisha ili ionekane wameshindwa.

Ndio yaleyale ya ubinafsi.
Tena ndio watakuwa na kazi hatari maana ccm tayari ina mizizi mipana ktk kila eneo. Hivyo tutajikuta tunarudi kule kuleeee.
 
Kwa nini Korea Kusini ni nchi tajiri yenye maendeleo makubwa wakati Korea Kaskazini ni nchi masikini yenye maendeleo duni wakati nchi zote zina utamaduni mmoja??
 
Ndio maana nikasema matatizo hayaishi ila hiyo ni proof.

Mimi sio fan wa Magufuli haswa kwneye upande wa uongozi ila utendaji huwezi kumpinga sana.

Ni katika kipindi chake hata maskini angeweza ingia ofisi yoyote mjini na akapewa huduma anayostahili.

Ni katika kipindi chake, alifanya maendeleo nchi nzima kuanzia barabara, masoko , huduma za afya lakini kikubwa, kuitengeneza dodoma kiutawala kwa kujenga mji na ikulu ili kufanya decentralization ya kutoka dar.

Ni katika kipindi chake utaona kila decision ukiitoa ya kuijenga chato. Ilionesha distribution ya maendeleo na kutaka nchi iendelee pasipo kujali interests za watu wachache

The Untouchables

Lakini nae alirudia tatizo lile la kuamini, nchi inahitaji viongozi strong kama yeye na CCM stronger. Akaua kabisa demokrasia

Unachosema kuhusu mfumo wa maisha ni sawa, lakini ipo valid zaidi kwa millenials na vizazi vya kabla yake. Kizazi cha 2000 hakikukuzwa sana katika hizo traditions ndio maana leo unaona kuna shift ya kiuongozi kww sbabau hii new generation wapo vocal lakini wanapitia shida za kiuchumi ambazo zinawaforce, kutaka serikali ifanye zaidi tofauti na zamani. Ambapo mtu alisoma na kupata kazi, angedemand nini kwa serikali

Kiufupi matatizo ni mengi, ilaaaaaaa bottom line ni CCM ikiondoka itasaidia kuleta balance of power kwa kuondoa ego ya kisiasa ambayo inawaaminisha watu wakishaingia CCM wamemaliza. Lazma viongozi wafikie sehemu ambapo watawaona wananchi wao kama maboss wenye uwezo wa kuwafuta kazi na si watawaliwa

Hii haitofanikiwa kama political supremacy ikiendelea kuwepo maana hata yenyewe haitoruhusu katiba ya wao kushtakiwa kwa sababu ni mzizi wa nguvu yao "absolute power". Kwa hiyo yote unayoongelea yataanza pale CCM itapowekwa pembeni kwa muda
 
Kwa nini Korea Kusini ni nchi tajiri yenye maendeleo makubwa wakati Korea Kaskazini ni nchi masikini yenye maendeleo duni wakati nchi zote zina utamaduni mmoja??

Umeuliza swali zuri na la msingi.

Korea kusini maendeleo yake makubwa yanatokana na uwekezaji wa mabeberu plus utamaduni wao.

Wakati Korea kaskazini maendeleo Yao yamekuwa yakisuasua kutokana na kuwekewa vikwazo na Mabeberu.
Ingawaje nao wanamaendeleo hats kama hayalingani na ndugu zao wa Korea ya Kusini.
 
Hakutoondoa matatizo yote ila kutaondoa 60% ya matatizo ambayo source ni chama cha ccm
 
Mifumo ya nchi yetu yooote imewekwa na CCM,kuanzia elimu,familia mpaka mifumo ya Kidini case study BAKWATA,Kwa hiyo chanzo Cha matatizo ni CCM,CCM ya Nyerere ilitengeneza ujamaa fake uliozaa hicho ulichokisema kuhusu familia,CCM ilitengeneza viongozi wa dini fake wanaofit kwenye malengo yao,kina Mwamposa,Gwajima n.k
Tatizo la Tanzania 90% ni CCM
 
Kuna mawazobmbadala ukiyasikia yanakuwa ni usaliti tu. Mfano ukimsikia Odero anasema maridhiano yanaweza kuendelea hata Lissu akiwa gerezani,hayo ni mawazo mbadala au usaliti? Suala la mifumo mibovu linabaki kuwa suala la CCM.
 
Lowassa hajawahi kuwa mwanacdm, bali alipewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya cdm kutokana na hela zake. Tafuta popote kama utaona akiwa na vazi la cdm maarufu kama Gwanda.
 
Unajua kutetea ujinga ni kazi sana,Kuna mtu yoyote amewahi ilaumu serikali Kwa tatizo lake binafsi? Nani huyo?
Kuna mtu amewahi kuilaumu serikali Kwa kukosa mke? Kukojoa kitandani? Kunyimwa unyumba na mke wake? Au tatizo binafsi unalozungumzia ni lipi?
Huwezi kusema ukosefubwa ajira ni tatizo binafsi,umaskini ni tatizo binafsi,kukosa maji ni tatizo binafsi hata upungufu wa chakula haliwezi kuwa tatizo binafsi.
Labda ufafanue hayo mambo binafsi ambayo serikali haitakiwi kulaumiwa
 

Upo sawa.
Na mimi nilichoeleza ni kuwa CCM inaweza kuondoka hata Kesho lakini kikiingia chama kingine uwezekano wa kuwa kama CCM ni Mkubwa Sana kutokana na tabia na mienendo inayoendelea katika jamii hasa huku mtaani.

Hiyo ndio hoja yangu.

CCM itaondolewa kimabavu hilo liko wazi kwa sababu wao hawapo tayari kuondoka kwa hiyari kwa kuweka uwanja sawa wa kidemokrasia ili watu wachague chama wanachokitaka.

Lakini hata CCM iondolewe Leo kimabavu uwezekano wa chama kitakachoshika hatamu ku-under perform ni mkubwa Sana.

Tabia walizonazo CCM ni hizohizo walizonazo Chadema kwa sehemu Kubwa. Tofauti yao ni ndogo Sana.
 
Nitajie moja kati ya kampuni 20 kubwa South Korea inayomilikiwa na mabeberu.
Nitajie mzungu, mhindi au mwarabu hata mmoja kati ya mabillionea 30 wa South Korea.
 
Katiba hata sasa ipo na kuna mambo yanakiukwa kinyume na katiba. Na ndio hapo tunarudi kule kuleee.

Hili pia tuliwahi jadii humu.

Sheria zipo nyingi Sana hazifuatwi.
Mfano Sheria za mazingira, mtaani watu wanatupa taka hovyo, tena watu wazima, wasomi wanasubiri serikali iwazuie.
Haya hiyo serikali IPO nayo. Afisa afya kata yupo yupo tuu. Kazi hafanyi, watu wanachoma moto mji unajaa moshi inakuwa kero. Sheria zinakataza. Lakini Nani anafuatilia?

Au ndio tunasema serikali ya CCM imeshindwa kusimamia Sheria?
 
Tume huru ya uchaguzi, ili tupate viongozi tunaowataka wakatuandikie katiba mpya itakayotenda HAKI,hakutakuwa na Urais,Mahakama,Wala Wabunge wa Mchongo
 
Shida yako unataka kuamini watu wote wanachangamoto ya malezi.

CCM ni sawa na koti tu, linasabisha kuficha wasio na malezi unayoyasema na kuleta shida. Ndio maana wengi wanaona kama ndio shida.

Lakin ingekuwa inaweka watu nora na kukimbiza wahuni wote, ingesaidia hata wahuni wadogo kubadilika. Lakini chenyewe ndio kinawakumbatia, kwa nini wahuni wasiendelee kuwepo.

Watu wanaimani kikipatikana chama mbadala labda kitajitahidi kuzuia wahuni kushika madaraka na kuwa watendaji katika ofisi za umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…