Kuifuta CCM sio kuondoa matatizo ya taifa hili. Hiyo ni propaganda yenye uongo Mkubwa

Jes
Heshima unaweza ijenga kwa mwezi mmoja..ila ukaiharibu ndani ya dk 2...
 
Katiba hata sasa ipo na kuna mambo yanakiukwa kinyume na katiba. Na ndio hapo tunarudi kule kuleee.
Ubovu mkubwa wa katiba ya sasa ndio unasababisha hata yale mazuri kukiukwa,
 
Tatizo ni watu wenye tabia mbaya, wajinga, wabinafsi kama wanyama (kiwango hutofautiana kati yao) wanaopata madaraka.
Madaraka kwa sasa hupatikana zaidi kupitia CCM.
Hata hivyo, chama kingine kikitawala, kama hakuna mchujo, mambo yatakuwa hayo hayo.
Ukoloni mamboleo huendelezwa na watu hao hao waovu.
Siyo wote waliopo madarakani ni waovu, wengine hukumbwa tu kutokana na wingi wa hao wabaya.
 
Matatizo ya nchi hii yataondolewa na katiba bora basi period

Malezi na makuzi na tamaduni yanarekebishika mara tu tutapokuwa na katiba bora yenye kuweka misingi ya uwajibikaji na uwajibishaji

Mwanadamu kwa asili anaongozwa kwa nadharia ya karoti na fimbo,hiyo ndio ramani sahihi ya kumshape huyu mwanadamu

Ndio maana kwenye vitabu vya dini tunaambiwa kwa watenda mema wataenda peponi na waovu motoni,ndio maana hapo kuna ambao wanapambania pepo kwakuhofia mwisho wa siku wataingizwa motoni

Na sheria za nchi hivyo hivyo, iwapo kiongozi akila rushwa na kudhibitishwa na akachukuliwa hatua stahiki hakuna kiongozi mwingine kesho atakaye rudia kosa hilo tena

Ikiwa mfanyakazi wa serikali au sekta binafsi akakamatwa ameomba rushwa katika kuwahudumia wananchi na ikadibitisha kafanya hivyo na kuchukuliwa hatua stahiki hakuna mpuuzi mwingine kesho atarudia hilo kosa hiyo ndio nadharia ya karoti na stick

Ikiwa kuna mfanyakazi ametimiza wajibu wake na akatambuliwa mchango wake na akathaminiwa kesho kuna wengine wengi watafanya vuzuri,hiyo ndio kanuni ya karoti na stick

Kwahiyo malezi,utamaduni,sijui mazoea yote hayo yananyooshwa na sheria ambazo zimenyooka na hazimpendelei mtu

Period.
 
Yale mauaji mliyofanya October 29 yanawapa maluweluwe sana,kama Ccm isingekuwa tatizo isingetumia nguvu kubwa kubaki madarakani ikiwemi kuiba kura, kufanya utekaji na mauaji.
Ingeunda tume huru ya uchaguzi, ingeruhusu wagombea binafsi, ingeruhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani ingekubalu kuwepo katiba mpya.
Wangeruhusu Tanganyika kuwa na serikali yao
 
Sikatai hoja yako Tanzania tuna utamaduni dhaifu wa uwajibikaji, unaoanzia kwenye familia, kwenye jamii na hatimaye kufika serikalini. Hilo ni tatizo la kweli na la muda mrefu.

Hoja yangu hapa ni kwamba baada ya kutambua kuwa tatizo hili lipo hatuwezi kubaki kulikubali kana kwamba halina suluhisho. Tunachopaswa kufanya ni kuchukua hatua za makusudi kubadili mwelekeo wa uongozi hasa kwa kuondoa uongozi wa CCM ambao kwa miaka mingi umeendeleza na kuimarisha mifumo hii mibovu
 
Unajikomba Kwa ccm usitekwe maana unajulikana na unatoa location Kila siku.
 
Kwa nini Vietnam na Thailand zimeendelea huku Cambodia, Myanmar na Laos zimebaki masikini wakati tamaduni zao wote zinafanana??
 

Sahihi kabisa.

Kinachohitajika kwa sasa ni wananchi kwa pamoja bila kujali itikadi ya vyama kuungana pamoja kupigania Katiba mpya ambayo itadhibiti MTU au kikundi au chama chochote ambacho kitakuwa na wanachama wenye tabia za kifisadi na kiovu.

Tukitumia maneno kuifuta CCM vuguvugu na kampeni hiyo inapoteza nguvu ya watu wema waliopo CCM ambao bado wanakipenda cham chao.

CCM bado inawanachama na wafuasi wengi wanaokiamini chama Chao sema wanaamini kuna kikundi kidogo kimepotoka na kuharibu Sura ya chama.

Sijui kama unaelewa hoja Yangu
 
Ndio maana tunataka uchaguzi wa haki ili ukweli ufahamike. Lakini ccm hawako tayari kwa hilo. Ukiona team haitaki mfumo wa VAR utumike uwanjani, jua team hiyo huwa haishindi kihalali.
 
Kujaribu kuyaondoa matatizo ya nchi hii bila kuindoa CCM ni sawa na kujaribu kumfanyia rehabilitation mtumiaji wa madawa ya kulevya huku akiendelea kubwia unga full throttle!
 
Ndio maana tunataka uchaguzi wa haki ili ukweli ufahamike. Lakini ccm hawako tayari kwa hilo. Ukiona team haitaki mfumo wa VAR utumike uwanjani, jua team hiyo huwa haishindi kihalali.
hasihindi kihalali kwan mlikua na mgombea kwamba kuna kura zenu zimeibiwa?
 
hasihindi kihalali kwan mlikua na mgombea kwamba kuna kura zenu zimeibiwa?
2019, 2020, na juzi 2024 tuligombea na uchafu ulikuwa wazi. Na hata sasa ndio kilichofanyika kupika matokeo, na zaidi ikawa na mauaji ya halaiki. Ila fundisho limetokea, tuombe uzima maana uchaguzi ujao kutakuwa na heshima, utaleta mrejesho hapa. Tunza hii post.
 
unajua ni mwaka wa 60 sasa ccm iko madarakani na watu kama wewe wlaikuepo toka mwanzo, kuna watu mpaka waliteka ndege!

Mauaji ya wahalifu weka sentensi vizuri
 
unajua ni mwaka wa 60 sasa ccm iko madarakani na watu kama wewe wlaikuepo toka mwanzo, kuna watu mpaka waliteka ndege!

Mauaji ya wahalifu weka sentensi vizuri
Wakati ukuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…