Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Sahihi kabisa
Sasa hivi ukweli utakimbiwa hasa ukweli unaolenga kukukosoa. Ukweli wa kukukosoa watu hawataki.
Ndio maana MTU anakaa bunju unaenda kuswali Kimara
Yupi huyo unayemkusudia?Pamoja na yote ulivyosema kuwa ni kweli ila huyu Dr mapaka ni KIAZI wa mwisho
Kujaribu kuyaondoa matatizo ya nchi hii bila kuindoa CCM ni sawa na kujaribu kumfanyia rehabilitation mtumiaji wa madawa ya kulevya huku akiendelea kubwia unga full throttle!
hasihindi kihalali kwan mlikua na mgombea kwamba kuna kura zenu zimeibiwa?
Ukitaka kujua mambo hubadilila, tazama maandamano ya juzi ya siku chache mno, hakuna mwanaccm anathubutu tena kuvaa jezi ya ccm mtaani. Pikipiki na baiskeli za Samia hazionekani mtaani. Huyo Makonda hata kwenda kushukuru wananchi huko Arusha hajathubutu. Mabadiliko haya akina Makonda ndio wahanga wa mwanzo, kwani wao ndio wameendesha siasa za kikatili mno ndani ya nchi hii. Na ukimuona Makonda, mwambie wananchi wa Arusha wanasubiri Ahadi yake ya kumpeleka Schwazinneger usiku wa mwaka mpya.Baada ya samia , anafuata makonda alafu tindo anakuja kua president
Uchaguzi huu umefanyika amna alieibiwa, nyie mmejitengenezea akili uchaguzi wenuAnazungumzia desturi za ccm kufanya faulu
CCM ndiyo mnufaika wa mifumo mibovu iliyopo na ndiyo inayoilinda kwa gharama yoyote!Sasa unaifuta CCM na watu waliopo CCM bado wapo hiyo inamaanisha nini?.wengine walihamia vyama vingine ikiwemo Chadema
CCM ndiyo mnufaika wa mifumo mibovu iliyopo na ndiyo inayoilinda kwa gharama yoyote!
Ccm ndio inashape mambo mengi, tushukuru Mungu sasa hivi kuna mitandao ila kabla ya hapa ambapo vyombo vya habari vilikua 100% vinaratibiwa na serikali unategemea jamii iweje ilhali wanalishwa kile serikali yao inataka??
Yaani imeongoza kwa miaka zaidi ya 60 halafu ikwepe lawama??
Ccm sio mtu, ccm ni mfumo. Kwa maana hiyo huo mfumo uko na loop holes ambazo wanazitumia hao wahalaifu ambao sio kua wapo Tz tu bali duniani kote ila huko kwingine hawapati hizo loopholes.
Ccm imezitengeneza, wakiambiwa wazizibe kupitia katiba hawataki.
Hapo utalaumu vipi malezi mkuu??
Kunufaika na mifumo mibovu maana yake ni kwamba bila hiyo mifumo mibovu hayo manufaa huwezi kuyapata.Ni kweli. Lakini Watanzania wengi ukiwatathmini kwa kina utagundua pia ni wanufaika wa hiyo mifumo.
Mkuu fungua macho yako
Kunufaika na mifumo mibovu maana yake ni kwamba bila hiyo mifumo mibovu hayo manufaa huwezi kuyapata.
Ni manufaa gani wanayopata Watanzania wa kawaida kwa mahakama kunyimwa authority ya kusikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Rais, kwa mfano?
Tunaongelea injustices ambazo zimekuwa codified (i.e., zinalindwa na sheria). Zile ambazo hazijawa codified mara nyingi zina remedies zinazopatikana kirahisi.Kunyimwa Haki ya kusikilizwa ipo kuanzia level ya familia ndio maana sio ajabu ukaona mpaka kwenye level ya kitaifa, serikali(Mahakama).
Nakuhakikishia akitokea Rais mpenda HAKI akasema aitekeleze haki kama ilivyo. Nchi nzima kuanzia maskini mpaka tajiri wote watalia na kumchukia. Na atauawa mapema Sana.
Watanzania ni wabinafsi. Wanapenda kutetea haki zinazokandamizwa na wengine lakini zile wanazokandamiza wao wanajizima data.
Sio kwamba naitetea serikali au kuitetea CCM
Najaribu kueleza kuwa watu wakitaka kubadilika waamue kubadilike kikamilifu. Wawe waadilifu kikamilifu. Angalau kwa asilimia hata 70% maana asilimia 100% itakuwa ni adhabu na haiwezekaniki
Kenya sio ya kuifananisha na Tanzania kwa sasa Kuna maeneo wamepiga hatua japo bado wanna changamoto kadhaa bado zinawakabiliMkuu chadema sio kwamba hawataweza au wataweza. Ninachoeleza hapo ni kuwa Chadema na ccm wote wanatoka kwenye jamii ileile ya Watanzania.
So kushindwa kuongoza au kuleta Maendeleo sio kwa sababu upo chama fulani. Bali ni suala la utamaduni(malezi) na ukoloni mamboleo.
Unajua hapa Afrika ni nchi ngapi zimebadili vyama vya siasa na bado maendeleo yakawa Stori za kufikirika?
Mfano Hapo Kenya.
Hio unazungumzia incompetent culture ambayo mzizi wake mkubwa ni kukosa uwajibikaji kwa waliopewa mamlaka na hapo ndipo udhaifu wa ccm unapojidhihirisha. Ushajiuliza hao wanaopaswa kusimamia usafi kwenye miji wasipotimiza wajibu wao hua wanachukuliwa hatua gnHili pia tuliwahi jadii humu.
Sheria zipo nyingi Sana hazifuatwi.
Mfano Sheria za mazingira, mtaani watu wanatupa taka hovyo, tena watu wazima, wasomi wanasubiri serikali iwazuie.
Haya hiyo serikali IPO nayo. Afisa afya kata yupo yupo tuu. Kazi hafanyi, watu wanachoma moto mji unajaa moshi inakuwa kero. Sheria zinakataza. Lakini Nani anafuatilia?
Au ndio tunasema serikali ya CCM imeshindwa kusimamia Sheria?
Mkuu bilashaka hujafahamu CCM ni nini. Labda unaona CCM ni chama cha siasa kama vilivyo CHADEMA, ACT, CHAUMMA, NCCR, TLP, n.k. WRONG. Usije ukalinganisha CCM na chama cha siasa.KUIFUTA CCM SIO KUONDOA MATATIZO YA TAIFA HILI. HIYO NI PROPAGANDA YENYE UONGO MKUBWA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Kuna watu wanadanganya Watanzania matatizo ya Nchi hii ni uwepo wa chama cha mapinduzi( CCM ). Huo ni uongo mkubwa.
2. Wengine wanausema uongo huo kwa makusudi wakijua ni uongo(Siasa) wengine wanasema uongo huo bila ya kujua.
3. Sisi Watibeli hatupendi upotoshaji, uongo. Mtu yeyote au kikundi chochote bila kujali nafasi, cheo, mahusiano yetu na wao.
4. Kusema CCM ikiondolewa kwenye hii nchi matatizo ya taifa hili yataondoka ni uongo. Na kauli za kisiasa.
5. Matatizo ya nchi yetu Yana mizizi mikuu miwili;
a) Malezi kuanzia ngazi ya Familia.
b) Ukoloni Mamboleo.
6. Asilimia 60% ya Matatizo ya nchi hii yanatokana na Malezi Mabovu kutoka kwenye ngazi ya Familia. Hapo ndipo kuna mambo ya uadilifu, uchapakazi, nidhamu, uzalendo n.k.
7. Asilimia 40% ni Ukoloni Mamboleo.
Binafsi ninaamini taifa letu bado halipo huru. Hicho ndicho ninajua. Ingawaje ukiniambia nikupe ushahidi naweza kukosa lakini ninachoamini ndivyo ilivyo.
8. Akili Yangu inanituma kuwa kuna mikataba ya siri ambayo iliingiwa ambayo inaifanya nchi yetu isiwe huru.
9. Unaweza ukawa mzalendo kikamilifu. Ukapewa urais na ukaona ni rahisi. Unaingia ikulu unakutana na vitu vizito unabaki unabung'aa.
10. Ukisema ukaze watu wako wa chini wanakuwa sio waadilifu. Wanaungana na mabeberu wanakunyoosha.
11. Mabeberu wananguvu kwenye jamii lililojaa watu wasiowaadilifu. Wasio wachapakazi, wenye tamaa, wapenda Rushwa., wavivu, wasaliti n.k.
12. Tabia zote hizo mbaya MTU hujifunza alipolelewa, makuzi, na jamii inayomzunguka.
13. Hauhitaji kuwa CCM ili uwe mla rushwa, haihitaji uwe CCM ili uwe Fisadi, haihitaji uwe CCM ili uwe msaliti wa taifa lako.
14. Mambo hayo ni matokeo ya malezi mabovu tangu mtu akiwa mtoto Mdogo.
15. Sheria za ndoa, familia zikilegezwa na kutosimamiwa ipasavyo huwezi kuwa na taifa la maana lenye uadilifu na maadili.
16. Uwe CHADEMA au CCM au huna chama kama hauna uadilifu ni hauna tuu.
17. Ukandamizaji wa kisiasa hautokani na CCM bali ukandamizaji ni mfumo mzima wa jamii ya taifa letu.
18. Ukandamizaji na unyanyasaji ni utamaduni wa jamii zetu nyingi katika nchi yetu. Sio suala la uccm.
19. Nitakupa Mfano, kwa jamii zetu nyingi Mwanaume ambaye ni Baba na mume akikosea hapaswi kukosolewa na watoto wake au Mkewe.
20. Mwanamke au mke atakapojaribu kuhoji na kukosoa maamuzi na matendo ya mumewe atashukiwa na kukabiliwa vilivyo.
21. Mzazi hakosei. Mke awe msikivu tuu na hapaswi kutoa maamuzi au kukosoa. Hup ni utamaduni..
22. Ukienda Kanisani nako au Msikitini nako utakuta vituko na ukandamizaji mwingine.
23. Unaambiwa Kiongozi hakosei. Au unaambiwa huwezi challenge Quran au biblia. Hizo ndio akili za kikoloni hizo. Utumwa!
24. Quran kwa nini isi chalenjiwe? Ina mini hasa cha ajabu. Kama ingekuwa ukikikosoa unapigwa shoti, au ukisoma andiko inakuwa jambo Fulani tungesema ni kitabu tofauti.
25. Halikadhalika na Biblia kwamba isikosolewe. Kwa vipi? Inakipi cha ziada? Huo ni ukandamizaji wa watu wenye mawazo tofauti na vitabu hivyo.
26. Najaribu kueleza mifumo mbalimbali ya jamii yetu ambayo inatujengea matatizo ya mbali kuliko vyama vya siasa
27. Malezi yaliyojikita kwenye ulaghai na Mila potofu ni sehemu ya kubwa inayoleta matatizo ndani ya taifa letu.
28. Fikiria Mgeni anakuja kwenu mnampa chombo cha udongo ambacho ninyi wenyewe hamkitumii. Ninyi mnatumia vyombo vya plastiki au vibaya. Mazoea hayohayo yanafika ngazi ya kitaifa fursa muhimu na miradi nyeti hata kama kuna raia wenye uwezo wa kuendesha miradi hiyo hatapewa watapewa Wageni.
29. Ukisema ni UCCM, wewe kwako unapoweka vyombo vizuri na maalumu kwaajili ya wageni huku watoto wako mwenyewe wakila kwenye makopo na sahani za plastic au mifupa badala sahari nzuri za udongo au za vioo. Huo kwako sio uccm ni ukarimu.
30. Kutumia mabavu kwenye familia yako, kumtesa mkeo na watoto huoni tatizo lakini serikali ikifanya unaona ni tatizo na linasababishwa na CCM. Unaona?
31. Mkeo hajui akaunti na mapato ya familia yako. Hajui unaingiza kiasi gani. Hajui matumizi yako. Unaficha pesa na miradi yako. Na mnahamasishana kutokuwaamini wanawake. Muda huohuo unailaumu serikali kutokuweka mikataba wazi, kuficha pesa nje ya nchi, kufanya anasa n.k.
32. Huo ni UCCM serikali kufanya anasa na kujinunulia magari ya kifahari, viongozi kujipendelea lakini wewe unapoenda kunywa bia na Kula nyama choma huku mkeo na watoto wakiwa nyumbani na bajeti ya elfu 15 wakati wewe unatumia zaidi ya elfu 50 bar pekeako huo sio UCCM. Na sio vibaya.
33. Tabia ya ubinafsi ni suala la kimalezi, kiutamaduni ambapo likifika level ya kitaifa linakuwa NI tatizo sugu ambalo kulidhibiti ni kipengele.
34. Kwa kumalizia. CCM sio tatizo la nchi hii. Tatizo ni malezi na ukoloni mamboleo.
Kufikia hapo sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
CCM ipi, hii hii inayosema tukiwapoteza wapinzani, police msiwatafute au CCM gani unayotetea ?KUIFUTA CCM SIO KUONDOA MATATIZO YA TAIFA HILI. HIYO NI PROPAGANDA YENYE UONGO MKUBWA.

Hii no kansa kwenye taifa letu.10. Ukisema ukaze watu wako wa chini wanakuwa sio waadilifu. Wanaungana na mabeberu wanakunyoosha.