Pamoja na kuwa inshu ya shaidi kuingia na note book Kizimbani ijumaa wiki iliyopita Jaji alihaidi kuwa mahakama itaifanyia maamuzi Jumatatu hii. Yani ataanzia na objection ya kina kibatala.
Jumatatu mahakama haikukumbuka ata si kuianzia tu maana ndipo walipoishia. Pia nikiamini pingamizi Hilo lingeshugulikiwa kabla ya kufanya maamuzi ya kesi ndogo kwani ushaidi wa kwenye note book ulitumika. Lakini ata baada ya kutoijali na kufanyika maamuzi ya kesi ndogo bila kuzingatia pingamizi lililokuwepo. Lakini ata baada ya kufanya uamuzi wa kesi ndogo alilipotezea na kuendelea na Mambo mengine tu. Baada ya maamuzi ikabidi akina kibatala wakumbushie Tena.
Ndio nikajua kumbe sio inshu siliasi. Au sio kitu kikubwa au kwasababu kimetoka kwa utetezi.
Kwa alivyokipotezea Jaji Basi Tena ata leo Akina kibatala wasitegemee jipya, linaenda kutupiliwa mbali.
Hii kesi NI fedhea kubwa kwa kibatala na Jopo lake. Aiwezekani kila pingamizi linatupiliwa mbali. Maana yake hawezi kujenga hoja au hajui wanachokifanya. Akina Kidando wanaonekana wanauwezo mkubwa zaidi yao.
Mi nazani na pingamizi Hilo likifeli Basi kibatala ajitoe tu kwenye hii kesi haiwezekani kung'ang'ania likitu lisilo na tija na linaloleta hisia za kuhoji uwezo wako Kama Mwanasheria.