Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Kuishi kwingi kuona mengi: Soma kisa nilichokiona Kawe

Nilichokiona kwa Mwamposa watu wengi wapo na misongo ya mawazo tu, madeni, na wale ambao Koo zao zina mambo ya kishirikina.
Wengine matatizo ya kisaikolojia tu yanawasumbua.
Yupo very technical kwenye sadaka
 
Kuna jamaa yangu alinibembeleza Sana niende kanisani kwao kwenye maombi nikaenda, muda wa maombi watu wanaangukia tu asee nikashangaa...mchungaji akanifata na kuanza kuniombea lakini sikuanguka...ghafla nikapigwa kibao kwenye kisogo nikayumba nikafumbua macho na kugeuka nakutanisha macho na mchungaji, nilichukia Sana nikaondoka...tangu siku hiyo siwezi na sijawaji Tena kwenye makanisa ya aina hiyo.
Polee sana..😁
 
Pia mimi nilikuwa naombewa hivyox2 niache bangi miaka ya nyuma nikawa nakomaa kudondoka wakati wengine wanaoombewa wanadondoka. Mchungaji akanisogelea na kuninong'onezea Dogo Aisee chalii yangu jidondoshe basi mbona unazingua mbele ya kadamnas? Bado nikawa nimekomaa tu na kumuambia Mchungaji aniwekee laki mfukoni kwanza kisiri. Bas nikamuona kaenda kunong'onezana na wale wanawashikilia wanaodondoka wasijibamize halafu nakuendelea kumpigia Mungu kelele na sauti za ajabux2 baadaye wale wanaosaidia wanaojidondosha wawili wakanisogelea kwa nyuma. Mchungaji akanifuata na kuanza kubwabwaja kwa sauti za ajabu nikashtukizia nachomwa vipini kama sindano makalioni nilipiga ukunga wa hatarii nikasikia mchungaji akipaza sauti toka kwa jina yesu nikawa bado nakomaa kudondoka nikachomwa tena kipini cha hatarii na mtama kima cha nyoka na wale wanaowashikilia wanaodondoka wasijibamize ikabidi tu niende chini
Vipini vya matako [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna muingiliano UPI kati ya kuombewa na kuangukaa, yani ukiombewa lazima uende chini ???,
 
Nishawai kwenda kanisani tukapangwa foleni ya kupakwa mafuta[emoji3][emoji3][emoji3]...ikawa mchungAji anakupaka mafuta kuchwani alafu akaongea maneno yake...Mimi nikawanashangaa Watu wanaanguka TU...mmoja baada ya mwingine.

Kuna Watu nyuma yetu na wamama wamebeba khanga...

Kila mtu akawa anaanguka ..ilivyofika zamu Yangu nami nikaapiga kelele...alafu nikaajiangusha chini[emoji3][emoji3][emoji3]....

Wengine wanajinyonganyonga Kama nyoka nguo zinawavuka wamama wanakuja kuwafunika...

Kwakweli Sijawai kujua Sababu ya Watu kuanguka...Mimi nilifuata mkumbo.
Ha haaaaaa WeWe Ni mapepe kwani?mbona Mimi siwezi hata kupiga hizo kelele?wananiombea Hadi wanasanda sidondokiii
 
Pia mimi nilikuwa naombewa hivyox2 niache bangi miaka ya nyuma nikawa nakomaa kudondoka wakati wengine wanaoombewa wanadondoka. Mchungaji akanisogelea na kuninong'onezea Dogo Aisee chalii yangu jidondoshe basi mbona unazingua mbele ya kadamnas? Bado nikawa nimekomaa tu na kumuambia Mchungaji aniwekee laki mfukoni kwanza kisiri. Bas nikamuona kaenda kunong'onezana na wale wanawashikilia wanaodondoka wasijibamize halafu nakuendelea kumpigia Mungu kelele na sauti za ajabux2 baadaye wale wanaosaidia wanaojidondosha wawili wakanisogelea kwa nyuma. Mchungaji akanifuata na kuanza kubwabwaja kwa sauti za ajabu nikashtukizia nachomwa vipini kama sindano makalioni nilipiga ukunga wa hatarii nikasikia mchungaji akipaza sauti toka kwa jina yesu nikawa bado nakomaa kudondoka nikachomwa tena kipini cha hatarii na mtama kima cha nyoka na wale wanaowashikilia wanaodondoka wasijibamize ikabidi tu niende chini
Ha haaaaa umenichekesha
 
Kuna jamaa yangu alinibembeleza Sana niende kanisani kwao kwenye maombi nikaenda, muda wa maombi watu wanaangukia tu asee nikashangaa...mchungaji akanifata na kuanza kuniombea lakini sikuanguka...ghafla nikapigwa kibao kwenye kisogo nikayumba nikafumbua macho na kugeuka nakutanisha macho na mchungaji, nilichukia Sana nikaondoka...tangu siku hiyo siwezi na sijawaji Tena kwenye makanisa ya aina hiyo.
Ha haaaaa uminikumbusha vibao vya kustukiza vya kisogoni E.A.G.T city center kwa pastor Katunzi....vinavurugaaa ila sikudondoka
 
Ha haaaaaa WeWe Ni mapepe kwani?mbona Mimi siwezi hata kupiga hizo kelele?wananiombea Hadi wanasanda sidondokiii
Dada Joannah...nilfuata mkumbo tuuu..maaana wote wanadondoka nikajua nifashion..

Nikafuata mkumbo
 
Nilichokiona kwa Mwamposa watu wengi wapo na misongo ya mawazo tu, madeni, na wale ambao Koo zao zina mambo ya kishirikina.
Wengine matatizo ya kisaikolojia tu yanawasumbua.
Kwa hiyo hayo hayatakiwi kuombewa, au??? Hivi unajua chanzo hasa cha hayo matatizo???
 
Mwaka 2011 nilimtembelea ndugu yangu maeneo ya Block T, Mbeya.

Yeye na familia yake wanasali AGAPE, ni walokole kweli kweli na mkuu wa kaya ni mzee wa kanisa.

Viongozi wengi wakubwa AGAPE hupenda kutembelea kaya ile kwa maombi, mafundisho, maongezi na chakula.

Hadi Mr. Fenandez na mkewe, Annie nao huwatembelea kila wafikapo Mbeya.

Wakati nimefika nilikuta wiki ya maombi ya kazi, na msaidizi wa Askofu Fenandez alikuwa Mbeya akiongoza maombi hayo ya wiki.

Kulikuwa kile kinaitwa kufunguliwa, ambao hawajampokea Bwana walimpokea, wengi makumi kwa makumi, isipokuwa mimi. Jambo lile halikuwafurahisha wenyeji wangu, walitaka niokoke pia.

Maombi yakawa maombi, kila siku usiku wanatembelea kaya ile na kufanya maombi, kama kawaida waombewaji hudondoka.

Wao wakifanya maombi, mimi huwa chumbani nikiperuzi FB na Twitter. Ndugu walinishawishi sana, nikaona acha nifanye watakayo kwakuwa nipo kwao, nikiondoka kurudi home, naendelea na kanisa langu.

Kabla ya maombi, ilianza Sala ya toba, nikifuatisha maneno ya yule msaidizi ya Fenandez. Baada ya hapo alinishika kichwani kuniombea. Kwa kweli sikusikia nguvu yoyote ya ajabu, ulikuwa mkono tu, jambo lililofanya niendelee kusimama wima tena mwenye utulivu huku nimefumba macho.

Nahisi alipoona sitetereki, nikaona anaanza kunifinya maeneo ya misuli ya macho, yakaanza maumivu ya kichwa, nikavumilia... Alipoona nimetulia, akaweka mkono wa pili na kuzidi kuomba huku akiniminya zaidi, maumivu yalizidi, nikapata akili kuwa anataka nidondoke, basi taratiiiiiiibu nikaanza kushuka chini.

Bro alipoona nanyong'onyea, akaja nyuma yangu na kunidaka, kisha nikalazwa chini na kila mtu akaanza kukemea pepo chafu la kiburi litoke ndani yangu.

Baada ya kuamka, mchungaji akasema pepo aliyekuwa ndani yangu hakuwa wa kawaida, kama angekuwa mchungaji dhaifu, asingetoka hakika.

Nilicheka kimoyomoyo, siku ikaisha
Hujui mambo mengi sana. Watu wanasali eti wewe unafesibuka, jamani. Isijekuwa kweli kalikuwa kapepo ka kiburi kanakutesa.
 
Nakumbuka miaka kama kumi na kidogo hivi mjini Arusha, alikuja nabii mmoja mwanamke ambaye alikuja kufungua kanisa jipya na kumuweka wakfu mchungaji mpya wa kanisa hilo.

Nilichoshangaa ni pale mchungaji mpya alipodondoka alipokuwa anawekwa
a wakfu kwa kuombewa na nabii huyo mwanamke.
Nilishangaa sana, sasa kama yule ambaye anakuwa mchungaji anaanguka ikimaanisha ana mapepo sisi wengine itakuwaje??

Imani yetu tuiweke kwa Mungu Baba, Mwana na Roho mtakatifu, na sio kwa watu.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Ungeuliza wenyewe maana ya kuanguka nini; labda ndio utaratibu wakati wa kuombewa. Sasa wewe uliamua kutoka na tafsiri yako. "Don't apply saliva as your writing tool while the pen is there there!"
 
Nishawai kwenda kanisani tukapangwa foleni ya kupakwa mafuta[emoji3][emoji3][emoji3]...ikawa mchungAji anakupaka mafuta kuchwani alafu akaongea maneno yake...Mimi nikawanashangaa Watu wanaanguka TU...mmoja baada ya mwingine.

Kuna Watu nyuma yetu na wamama wamebeba khanga...

Kila mtu akawa anaanguka ..ilivyofika zamu Yangu nami nikaapiga kelele...alafu nikaajiangusha chini[emoji3][emoji3][emoji3]....

Wengine wanajinyonganyonga Kama nyoka nguo zinawavuka wamama wanakuja kuwafunika...

Kwakweli Sijawai kujua Sababu ya Watu kuanguka...Mimi nilifuata mkumbo.
Ungeuliza, jamani. They who ask, remain fool for five minutes; they who don't ask, remain fool forever. ~ Chinese Proverb
 
Picha linaanza napokea simu kwa ndugu zangu upande wa mama watoto wangu wanasema, samahani tunakuja kwenye maombezi kwa Mwamposa wewe kama mwenyeji tunaomba utupokee ili utupeleke kwa Mwamposa tukaombewe.

Nikasema ok poa nitawapeleka nyie njooni. Ijumaa wakaingia ndani ya jiji la Dsm nikawapokea, Jumamosi chapu nikawapeleka Kawe kuombewa, mimi nikaamsha kwenye mishe zangu za hapa jijini.

Kesho yake Jumapili waakambiwa warudi tena kweli Jumapili tena nikawarudisha kwenye ibada kama kawaida nikasema ibada ikiisha mtanistua nije kuwachukua.

Mida ya saa nane ibada ikaiisha wakanishitua nikawachukuwe nilipofika kwa Mwamposa mmoja wao akasema kuwa kuna mfanyakazi mwenzake walishawahi kufanya naye kazi miaka ya nyuma kwenye kampuni kampigia simu waonane maeneo ya PICOLO HOTEL kuna maombezi pia.

Basi bwana tukaenda pale Picolo hotel kufika pale wakatupandisha juu kuna ukumbi kule wanasali.

Nilichokikuta kule kinashangaza sana kwa kuwa ilibidi niwasubiri basi nikasema hebu ngoja nikae nisikilizie hapahapo ukumbini.

Kanisa lina waumini 13 tu, wanawake 10 na wanaume 3. Maombi yakaanza nguvu ya upako sijui nini inawashukia wakawa wanadondoka waumini wote hadi ndugu zangu nao wanadondoka.

Nikajisemea moyoni mbona haya majanga. Ikawa kama mchezo sasa wanaombewa watano waliobaki wanasimama nyuma yao kuwashikilia ili wasijibamize sakafuni. Wakizinduka wengine tena wanaombewa halafu waliodondoka wanaamka tena kuwashikilia wenzao.

Nikachoka kuangalia movie ya kitoto nikawambia oya nyie si mnadondoka humu hebu niwaache mkipona mtanishitua nije niwachukue twende nyumbani. Nimeshangaa hivi kipi kinamfanya mtu anadondoka hovyo wakati wa maombezi au ni michezo ya kuigiza?​
Nduguzo walikuwa ni sehemu ya waigizaji?
 
Back
Top Bottom