Kuishi na mke kunataka uvumilivu wa chuma

daaah laiti wanawake wote wangekuwa na akili kama zako tungekuwa na raha
 
Mimi nadhani kuishi pamoja kama mume na mke ndo kunahitaji uvumilivu.

Wote mvumiliane na sio uvumilivu uwe wa upande mmoja tu.

Kumwona mwenzio ndiye mwenye mapungufu na wewe kujiona uko timilifu nayo ni mapungufu.

U said it all brother. Kuna watu wanajiona wao kama malaika. Wanajihesabia haki na kuwaona wenzao ndo wakosaji pekee.
 
Misingi muhimu ya ndoa..
1.Upendo
2.Uvumilivu
3.Kukubali mapungufu ya mwenzio 4.Kuheshimiana
5.Kukubali maelewano
6.Ukweli na uaminifu

Haya yakikoseka hata moja tu lazima uje jukwaani kuiponda ndoa. Kitu ambacho ni uonevu kwa taasisi ya ndoa. Nadhani mponde mkeo binafsi na wewe mwenyewe kwa kushindwa kuitetea katiba ya ndoa kama ulivyo apa kwa mfungisha ndoa na Mungu wako.
 
Sina la kuongeza maana nimeoa nauona moto wake,
Unaweza kuyayusha hata hicho Chuma cha uvumilivu.
Nataka kuoa ila kila mtu analalamika inaelekea huko ndoani kuna moto wa makaa ya mawe!...nimerudi nyuma hatua 200
 



Dah mkuu nikupe pole sana ,ila nikuombe ni nukuu maneno ya mtume(rehma na amani ziwe juu yake)Anasema;Mwannamke ameumbwa kwa ubavu uliopinda,ukitumia nguvu sana kuunyoosha basi utavunjika na ukiacha basi utapinda,
Nacho fahamu mimi siku zote hawa watu hawaposawa ,wanahitaji maelekezo kila kukicha namna unavyotakamuishi,na unaweza mwelekeza saiv akarudia tena kosa lilelile,pia zipo tabia nyingine haziwezi kubadilika maana kishakuwa kama kilema,
Ila naimani kila mwenye baya hakosi jema kubwa cha kuzingatia je yapi mengi?mema yake au mabaya? kama mema mengi endelea kustahamili mkuu maana hata sisi wenyewe pia tuna madhaifu na mapungufu mengi ambayo pia wanatustahmilia,
mwisho ni kumwombea mungu sana, huwenda akabadilika
 
Wanaume acheni kulia lia, je nasisi tukiwasema madhaifu yenu mtaona sawa, Kama msipotunyamba humu. Ndoa inataka uvumilivu ndio maana mlikula kiapo kwa shida na raha
 
Mwanamke anataka uhakika wa maisha ya kesho kupitia PESA/MALI uliyonayo ili aishi vizuri yeye na wazazi wake (kama bado wapo hai) endapo wewe ukifa, hayo ya upendo sijui uvumilivu yaliishaga enzi za wamisionari wa kwanza, hayapogo siku hizi
 
Nendeni mkapata ushauri kwa waislam ambao wanawake wanne na maisha mazuri tu ,nyie mwanamke mmoja mmoja tu mwalia
 
kuna vitu nawakubali waislamu, ikiwemo;
1. Sherehe ya kuoa (Harusi) - Huitaji mamilioni kufanya harusi ukiwa na laki moja (100,000/= TSH) unafanya harusi ya maandazi na chai, shughuli imeisha. Tofauti na Wagalatia harusi inafika mpaka 100m Tsh.
2. KUOA WAKE mpaka WANNE kwa mkupuo (na upo uwezekano wa kuwaacha kwa talaka wote kwa mpigo na ukaanza upya mchakato).

3. Utaratibu wa MAZISHI gharama ni sanda tu mbwembwe za makemera, jeneza sijui T-shirt, miwani, kuaga/kutoa salama za unafiki mara ya mwisho hakuna, ni kukamuliwa kisha kuwekwa kwenye mkeka na kwenda kuzikwa.
 
kabsaa, imeandikwa hata katika kitabu cha Mungu, Ishini na wake zenu kwa AKILI, mlidhani Mungu hakuliona hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…