Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Kwa nyinyi wanaharakati hisia zako zinaweza kuwa na mashiko. SSH yupo juu sana kumzidi huyo mwanasheria msomi wa CDM.Lisu 1 = Samia 100
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa nyinyi wanaharakati hisia zako zinaweza kuwa na mashiko. SSH yupo juu sana kumzidi huyo mwanasheria msomi wa CDM.Lisu 1 = Samia 100
Jambo moja tu, nadhani umelisahau na limefanya mada yako nzima itiwe dosari.
Huyo Advocate Tundu Antipas Lissu ndiyo mzodoaji mkubwa wa Mzee Nyerere.
Wengine wote hufanya hivyo hapa JF, ila Lissu alifanya hivyo mbele ya ulimwengu mzima na mpaka sasa kumbukumbu ziko kwenye mtandao wa bunge la Tanzania. Labda, tukumbushane tu alichokisema ndugu Tundu Lissu: "Waliozoea vya kunyonga, hawawezi vya kuchinja" akimaanisha kwamba Mzee Nyerere alizoea kuvunja sheria, hivyo hata CCM hawawezi leo hii kuanza kuheshimu katiba.
Kiufupi, Mzee Nyerere anapendwa sana, hata mimi binafsi nampenda. Ila huu ujinga wa kutaka kulazimisha asisemwe hata pale alipotusababishia tuvae viraka na kukosa hata sabuni za kuogea ni jambo la hovyo. Wengi walioishi miaka ya 80's watakwambia ukweli wa hali ilivyokuwa.
Binafsi huwa nashukuru UJAMAA uliisha, na Mzee Dr Salim Ahmed Salim alitusaidia mno. Ukiisoma historia ya Tanzania kwenye vitabu pamoja na UJAMAA unaweza kuhisi kila kitu Mzee Nyerere anaonewa, ila wale walioiishi walau kuanzia 1975-1985 watakwambia ukweli.
Kwamba tuogope kuwasema kisa ni International Statemen, au Nobel Laureates nadhani linanipa mno ukakasi. Kina Winston Churchill, Abraham Lincoln, Julius Ceaser, Joseph stiglitz, Henry Kissinger, hadu Mother Theresa wote tunawasema na kuwazodoa mpaka leo hii. Mzee Nyerere, Mandela na Tutu ni kina nani hadi wasizodolewe ???
Bwahahahaha, mzee unajua mno taarabu. Hata hivyo wala haiondoi ukweli wowote ule.
Uzodolewe, unangwe, ubagazwe, ukosolewe, uchambwe, usutwe huo wote ni ubinadamu ambao kiongozi yoyote yule mkubwa duniani anatakutana nao. Kwamba unataka kusema hao niliowataja wanakumbukwa kwa mabaya yao nadhani tunarudi palepale, unapenda mno taarabu na mipasho mtoto wa kiume.
Dada yangu, wewe hata unikashifu mimi kwamba natokea ndani ya choo cha shimo binafsi wala haliniumizi kichwa. Hivyo wewe choma nguvu tu kuniita majina yote, ila nafasi na umri niliyofika nimesikia matusi, kebehi, kejeri za kila aina, hivyo hainidhuru kitu.
Matter of fact, hata wewe ni masikini tu, sema tunatofautiana viwango, kwamba unaweza ukawa hujazaliwa porini kama wazazi wako. Mtanzania kumcheka mwenzake umasikini, ni akili za CHICHI DODO, kupenda maggots halafu kuchukia Feaces. Umeelewa wewe masikini na mpori-pori mwenzangu ???
Haya turudi kwenye mada. Mzee Nyerere, Mandela na Lissu are giants who a person like me is not even coming close to shinning their shoes. Mchango wao kwenye jamii ni mkubwa mno, lakini kuzodolewa lazima watazodolewa tu. Kisa wamepata Nobel ? Kisa ni wenyeheri ? AU kisa nini haswa hadi wasizodolewe ???
Kama ni michango ya hawa watu, basi THIS IS A SUBJECTIVE TOPIC WITH LIMITLESS SCOPE. Wengine wanamuona Mandela as a pathetic quisling. Wengine wakiaangalia Tanzania na jinsi ilivyo wanaona Nyerere alikuwa anapoteza muda tu. ITS A SUBJECTIVE PERSPECTIVE AND YOU DONT GET TO DECIDE THE STANDARDS.
Labda niambiwe tu, vigezo gani vinamfanya Mzee Nyerere aheshimiwe kama MUNGU mtu, kwamba ambao tunamzodoa tujidhalilishe ?
Mtikila alikuwa mjuzi wa sheria.Ni kwa vile tuna siasa za hovyo tu… TL na Mchungaji mtikila walitakiwa waandikwe kwenye historia kwa maandishi ya dhahabu.
Kwa upande wa upinzani, Vijana wamefanya mazuri, lakini hawa ndugu wamewazidi wengi.
Hata angekuwa keshatangulia mbele za haki hana hadhi ya kukaa kundi moja na hao waasisi wa afrika.Mwulize hata Msigwa kama ana lolote dhidi ya Lissu.
Hapo Lissu anawakilisha walio hai.
Lissu ni jembe. Husuda za nini?
Long live TAL!
Huwezi kumlinganisha Mandela na Nyerere na vitu vya kijinga vya miaka hii ya mwendokasi (TAL) .Yamekuwa yakisikika maneno:
"JF ni Raha sana."
Kwa hakika ni kwa maana yake kamili.
Hayo ni pamoja na kuwaona baadhi ya wajumbe wakijitutumua kujaribu kuwazodoa watu ambao dunia Kwa ujumla wake imewavulia kofia.
Wandugu kwa level za kwetu kujimwambafai dhidi ya kina Lissu au Nyerere ni wenda wazimu.
Kwa level za dunia kujimwambafai dhidi ya watunukiwa nobeli (nobel laureates) yaani aina ya kina Mandela, Obama, Tutu na wa namna hiyo kwa nini isiwe zaidi burudani kwa wenye kujua maana?
Wanasema waswahili:
"Aibu mbona naona miye?"
Huyu ndiye Mandela, kwa ufupi mno katika hulka yake kama binadamu:
"After I became president, I asked my escort to go to a restaurant for lunch. We sat down and each of us asked what we wanted.
On the front table, there was a man waiting to be served. When he was served, I said to one of my soldiers: go and ask that gentleman to join us. The soldier went and conveyed my invitation to him. The man got up, took his plate and sat down right next to me.
While he ate his hands trembled constantly and he did not lift his head from his food. When we finished, he said goodbye without looking at me, I shook his hand and he left.
The soldier told me:
Madiba that man must have been very ill, seeing as his hands didn't stop shaking while he ate.-
Absolutely no! the reason for his trembling is another.
Then I told him:
That man was the warden of the prison where I stayed. After he tortured me, I screamed and cried asking for some water and he came humiliated me, laughed at me and instead of giving me water, he urinated in my head.
He is not sick, he was afraid that I, now president of South Africa, would send him to prison and do to him what he did to me. But I'm not like that, this conduct is not part of my character, nor of my ethics.
′′Minds that seek revenge destroy states, while those that seek reconciliation build nations. Walking out the door to my freedom, I knew that if I didn't leave all the anger, hatred and resentment behind me, I would still be a prisoner."
- Nelson Mandela.
Huwezi kumlinganisha Mandela na Nyerere na vitu vya kijinga vya miaka hii ya mwendokasi (TAL) .
Tundu Lissu mnyera tu na hafai kabisa kuweka kundi moja na Kina Nyerere hao ni wanafalsafa wa viwango vya kidunia.Umekurupuka kutokea wapi kamanda?
Wapi kalinganishwa Mandela, Nyerere au Lissu au hata baina yao? Kwamba ni kukurupuka tu kama ni uliyetiwa ufunguo?
Ama kweli kama mada ilivyoanza:
"JF ni Raha sana."
Hata angekuwa keshatangulia mbele za haki hana hadhi ya kukaa kundi moja na hao waasisi wa afrika.
Jazba nyingi, ukosefu wa busara za kawaida tu za kwenye maongezi, kauli zenye kudharau mamlaka zinazomtoka bila ya sababu ya msingi.
Hawezi kuwekwa kundi moja na Mzee Mandela.
Tundu Lissu mnyera tu na hafai kabisa kuweka kundi moja na Kina Nyerere hao ni wanafalsafa wa viwango vya kidunia.
Kila siku watu wanasoma maandiko yao na wengine hawaishi kuyanukuu.
Wanadumu katika kiwango chao tofauti na wanasiasa wengine. Hao ni waasisi waliyoyafanya yanawaweka katika ngazi ya juu sana.Kwani ungependa tungewaweka nani pale labda roho yako kamanda isuuzike?
Au si ungetuwekea hata credentials zako hapa tuziangalie labda unaweza kuwa jembe zaidi ya Lissu?
Labda kwamba hatukujui tu vitu vyako ndugu?
Lissu ni mnyera tu hawezi kuweka katika nafasi moja na kina Mandela, Nyerere.Wapi kawekwa Lissu kundi Moja na Mandela?
Kwani Lissu ni nobel laureate?
Hukuona hata Kwa Mandela Nyerere hayumo?
Inafahamika Pana makamanda waliofura kuliko ma CCM kwenye ukweli huu?
Kulikoni ndugu?
LISU ,kamtuma msigwa aende aseme mapungufu ya mbowe ili mbowe ajirekebishe
Ccm,wawe makini siku mbowe hayupo chairman na LISU akashika hatamu Msigwa pita atarudi
Wanadumu katika kiwango chao tofauti na wanasiasa wengine. Hao ni waasisi waliyoyafanya yanawaweka katika ngazi ya juu sana.
Nyerere alitembea nchi nzima kupambana katika kuleta uhuru wakati huo barabara nyingi ni za vumbi tupu.
Mandela alifungwa miaka 28 jela kwa sababu ya kuitetea Afrika ya Kusini hakuna tena mwanasiasa mwenye kuja kuwa na historia yenye uzalendo wa viwango hivyo.
Lissu kwanza ajifunze kuutumia vyema mdomo wake mbele ya watu kabla hajaweza kupandishwa hadhi yake.
Lissu hana haiba yenye kulingana na ya Nyerere/Mandela. CCM kumkalia kimya katika masuala mengi ya kisiasa ni muendelezo wa demokrasia, haina maana kwamba anao uwezo mkubwa kama tunavyodanganyana humu mitandaoni.Hapa unaungana nami kusisitiza kumzodoa huyu ni kujidhalilisha.
Hapa unaona je ungenitumia ushauri wako huu ili tuone vitu vyako ndugu?
Au wewe kipaji chako ni kwenye ushauri tu?
Kama ndivyo hayo si ndiyo yale ya chenga twawala basi tu magoli wanatufunga?
Muogope sana tundu LISU kwenye mikakati na msigwa alisafiri kwenda kumuaga LISU singida kwenye mikutano ileeee , ikabidi msigwa asubiri LISU aende kwa Mama wawili ubelgiji akijifanya kitibiwaKama ndivyo litakuwa kombora matata sana. Makombora ya aina hii ndiyo yanaweza kuwasambaratisha aina za CCM. Kwani pana hata haja ya kumung'unya maneno? Siyo hii upuusi mingine.
Lissu hana haiba yenye kulingana na ya Nyerere/Mandela. CCM kumkalia kimya katika masuala mengi ya kisiasa ni muendelezo wa demokrasia, haina maana kwamba anao uwezo mkubwa kama tunavyodanganyana humu mitandaoni.
Sawa ndugu.Hata darasani si lazima kila mtu kuelewa ndiyo maana kuna distinction, pass, supp na hata disco.
Wewe ni mgeni JF ndugu?
Anasema Museveni, maendeleo ya Uganda hayawezi kuwasubiria wakaramojong wajue umuhimu wa kuvaa suruali.
Kwamba tukusubirie wewe hadi uelewe mantiki?
Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu
Si walisema asiyejua maana haambiwi maana?
Mtu mmoja asiyeelewa wa nini? Kwa hakika kujikita kumwelewesha hiyo inaweza kuwa matumizi mabaya kabisa ya muda.
Habari ndiyo hiyo ndugu.