Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!

Ni vyema kabla ya kuendelea mno kujivua nguo hadharani kujiridhisha na yote yaliyokwisha kuwekwa wazi kuhusiana na jambo. Beberu akiita kufanya literature review.

Hivi uliweza ndugu kabla ya kuandika lolote kuyatambua haya:

Kuwa yalikuwa yameandikwa mapema mno tena kabla yako, haya si ndiyo anayoimba Prof. Jay kuwa:

"Utaniambia nini?!

Kama ng'ambo nilitimba kitambo mapema kabla yako?
utaniambia nini?!

Kama mjengoni nilikuwa na baba zako
na wengine mama zako?!

Utaniambia nini?!" 🎼🎼🎶

Kwamba kumbe hadi sasa ungali kuwa hujui tofauti ya kukosoa na kuzodoa na unaendelea kubwabwaja tu kama umetiwa ufunguo?!

"Kweli JF ni Raha sana."

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Kwamba kimsingi mzodoa waungwana kwenye kama hizi list tena bila kuwa na CV ya kueleweka, huyo si ni mbwabwazaji yule yule pendwa wa ndugu kutokea pande za kwa mfuga mbwa ndani ndani huko, macho makavu huku uso umepauka kwa vile ana mdomo tu?"

Kwamba hao dunia au jamii imewakubali ni kwa sababu ya ubora wao. Si kwa sababu ya ujinga wao ndugu.

Kwamba wewe dunia au jamii haijakukubali au haikutambui ni kwa sababu hauna qualities hizo. Kumbuka kutokuwa nazo si dhambi!

Makasiriko ya nini kwa kuzidiwa maarifa au karama? Kuwachukia hawa ndugu hakukuongezei wala kuwapunguzia wao lolote zaidi ya kuwa ni kujidhalilisha mwenyewe hadharani.

Kwamba labda wewe ni bora zaidi kwenye lipi basi? Si uliweke japo hapa nawe tukuunganishe au uwe mbadala humo?

Ama kwa hakika kama thamani yako haimo humo na una neno dhidi ya waliomo kwa vile una mdomo tu, Looh!

Huo ndugu hata kuku anao!
 
Twaarabu tena? Hii si twaarabu ndugu. Ukitaka hizo fika "Mwananyamala Koma Koma" kwao mama Kopa.

Huku ni mwendo wa uwazi na ukweli pekee.

Kwamba, bila ya kutofautisha misamiati na kuwa specific, kumbe tofauti yetu na zile ngwamba za kwa mfuga mbwa ndani ndani huko, iko wapi?

Nikuitishe kwa mara nyingine ikikupendeza kwenye literature nyingine hii, iliyokuwepo mapema mno kabla ya maandiko yako:

Hii nayo ilikuwa imekwisha ainisha mno umuhimu wa uangalifu katika matumizi ya maneno kwa maana yake kamili.

Ninakazia:

"Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!"​

LISU ,kamtuma msigwa aende aseme mapungufu ya mbowe ili mbowe ajirekebishe

Ccm,wawe makini siku mbowe hayupo chairman na LISU akashika hatamu Msigwa pita atarudi
 
Ninasikitishwa na kuitana kwako majina ambapo hakuna popote nilipokuita jina lolote.

Dalili ya kufilisika kwa mawazo. Ambapo kama ndivyo kuna uzi wa afya ya mwili huku:

Prof.Janabi: Ukifunga Siku ya Jumatatu na Alhamisi Unakuwa na Afya Bora,Asema Sukari na Pombe Havijawahi Kumuacha Mtu Salama.

Udada? Miye si mdada ndugu. Hata kama wewe ni mdada na labda ukiwa katika zako za kuuweka utambulisho wako rasmi hapa, pengine ya ukitegemea lolote la mafao, inihusu nini humo ndugu?

Kama ndivyo, si upambane na hali yako?

Kulikoni makasiriko yenu haya kuliko hata ya ma CCM?

Au ni jina la Lissu kuwamo kwenye orodha? Kwamba labda sababu tu Lissu nyota yake inang'aa mngependa kulazimisha iwe yenu?

Si mkang'arishe zenu hata kama ni kwa waganga huko, kwani taabu iko wapi?

Kwamba kwenye orodha hii kuna majembe?

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Kwamba kwa husuda zenu ndiyo maana tuko kwenye sintofahamu tuliyomo isiyokuwa na matumaini?

Kusuasua kwa harakati za ukombozi nchini ni matokeo ya uongozi dhaifu

Kwamba ghafla tofauti ya kukosoa na kuzodoa au ubinadamu na utakatifu hamjui?

Ya kuwa na Bado hata aibu kidogo hamuoni? Macho makavu, nyuso zimeyapauka? Looh!

Kwamba naendelea kusoma kipi katika ulichoandika?

Angalizo:

"Nisiache kukwambia kwenye andiko lako pathetic hili, nimeishia kusoma aya ya kwanza tu, utterly in disbelief!"
 
Mwulize hata Msigwa kama ana lolote dhidi ya Lissu.

Hapo Lissu anawakilisha walio hai.

Lissu ni jembe. Husuda za nini?

Long live TAL!
Hata angekuwa keshatangulia mbele za haki hana hadhi ya kukaa kundi moja na hao waasisi wa afrika.

Jazba nyingi, ukosefu wa busara za kawaida tu za kwenye maongezi, kauli zenye kudharau mamlaka zinazomtoka bila ya sababu ya msingi.

Hawezi kuwekwa kundi moja na Mzee Mandela.
 
Huwezi kumlinganisha Mandela na Nyerere na vitu vya kijinga vya miaka hii ya mwendokasi (TAL) .
 
Huwezi kumlinganisha Mandela na Nyerere na vitu vya kijinga vya miaka hii ya mwendokasi (TAL) .

Umekurupuka kutokea wapi kamanda?

Wapi kalinganishwa Mandela, Nyerere au Lissu au hata baina yao? Kwamba ni kukurupuka tu kama ni uliyetiwa ufunguo?

Ama kweli kama mada ilivyoanza:

"JF ni Raha sana."
 
Umekurupuka kutokea wapi kamanda?

Wapi kalinganishwa Mandela, Nyerere au Lissu au hata baina yao? Kwamba ni kukurupuka tu kama ni uliyetiwa ufunguo?

Ama kweli kama mada ilivyoanza:

"JF ni Raha sana."
Tundu Lissu mnyera tu na hafai kabisa kuweka kundi moja na Kina Nyerere hao ni wanafalsafa wa viwango vya kidunia.

Kila siku watu wanasoma maandiko yao na wengine hawaishi kuyanukuu.
 
Wapi kawekwa Lissu kundi Moja na Mandela?

Kwani Lissu ni nobel laureate?

Hukuona hata Kwa Mandela Nyerere hayumo?

Inafahamika Pana makamanda waliofura kuliko ma CCM kwenye ukweli huu?

Kulikoni ndugu?
 
Tundu Lissu mnyera tu na hafai kabisa kuweka kundi moja na Kina Nyerere hao ni wanafalsafa wa viwango vya kidunia.

Kila siku watu wanasoma maandiko yao na wengine hawaishi kuyanukuu.

Kwani ungependa tungewaweka nani pale labda roho yako kamanda isuuzike?

Au si ungetuwekea hata credentials zako hapa tuziangalie labda unaweza kuwa jembe zaidi ya Lissu?

Labda kwamba hatukujui tu vitu vyako ndugu?
 
Wanadumu katika kiwango chao tofauti na wanasiasa wengine. Hao ni waasisi waliyoyafanya yanawaweka katika ngazi ya juu sana.

Nyerere alitembea nchi nzima kupambana katika kuleta uhuru wakati huo barabara nyingi ni za vumbi tupu.

Mandela alifungwa miaka 28 jela kwa sababu ya kuitetea Afrika ya Kusini hakuna tena mwanasiasa mwenye kuja kuwa na historia yenye uzalendo wa viwango hivyo.

Lissu kwanza ajifunze kuutumia vyema mdomo wake mbele ya watu kabla hajaweza kupandishwa hadhi yake.
 
Wapi kawekwa Lissu kundi Moja na Mandela?

Kwani Lissu ni nobel laureate?

Hukuona hata Kwa Mandela Nyerere hayumo?

Inafahamika Pana makamanda waliofura kuliko ma CCM kwenye ukweli huu?

Kulikoni ndugu?
Lissu ni mnyera tu hawezi kuweka katika nafasi moja na kina Mandela, Nyerere.
 
LISU ,kamtuma msigwa aende aseme mapungufu ya mbowe ili mbowe ajirekebishe

Ccm,wawe makini siku mbowe hayupo chairman na LISU akashika hatamu Msigwa pita atarudi

Kama ndivyo litakuwa kombora matata sana. Makombora ya aina hii ndiyo yanaweza kuwasambaratisha aina za CCM. Kwani pana hata haja ya kumung'unya maneno? Siyo hii upuusi mingine.
 
Hapa unaungana nami kusisitiza kumzodoa huyu ni kujidhalilisha.

Lissu kwanza ajifunze kuutumia vyema mdomo wake mbele ya watu kabla hajaweza kupandishwa hadhi yake.

Hapa unaona je ungenitumia ushauri wako huu ili tuone vitu vyako ndugu?

Au wewe kipaji chako ni kwenye ushauri tu?

Kama ndivyo hayo si ndiyo yale ya chenga twawala basi tu magoli wanatufunga?
 
Lissu hana haiba yenye kulingana na ya Nyerere/Mandela. CCM kumkalia kimya katika masuala mengi ya kisiasa ni muendelezo wa demokrasia, haina maana kwamba anao uwezo mkubwa kama tunavyodanganyana humu mitandaoni.
 
Kama ndivyo litakuwa kombora matata sana. Makombora ya aina hii ndiyo yanaweza kuwasambaratisha aina za CCM. Kwani pana hata haja ya kumung'unya maneno? Siyo hii upuusi mingine.
Muogope sana tundu LISU kwenye mikakati na msigwa alisafiri kwenda kumuaga LISU singida kwenye mikutano ileeee , ikabidi msigwa asubiri LISU aende kwa Mama wawili ubelgiji akijifanya kitibiwa

CHADEMA ,ili ikae sawa lazima mbowe awe pembeni , kibodi zikamatwe na akina heche
 
Lissu hana haiba yenye kulingana na ya Nyerere/Mandela. CCM kumkalia kimya katika masuala mengi ya kisiasa ni muendelezo wa demokrasia, haina maana kwamba anao uwezo mkubwa kama tunavyodanganyana humu mitandaoni.

Wewe unayo?

Dk. Remmy na beetle yake archaic aliandika kwa nyuma:

"Baba yako analo?"

Kwa hakika ujumbe huo uliwakata maini sana vizaba zabina waliokuwa wazodoaji kabla ya kuuona.
 
Sawa ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…