Kujenga daraja kuunganisha Dar es Salaam na Unguja ni upotevu wa fedha za maskini. Tuachane na mpango huu!

Kujenga daraja kuunganisha Dar es Salaam na Unguja ni upotevu wa fedha za maskini. Tuachane na mpango huu!

Wewe ndo hujapevuka kiakili. Mleta mada kazungumzia hasara,ina maana kwake daraja halitakuwa na faida.
Daraja haliwezi kuwa na hasara tu bila faida!
Wewe ndiyo hujapevuka kabisaa bora ya mleta uzi.
 
Ni Mpango wa hovyo na WA uhuni tuu.Kama Kuna ulazima.bora kujenga Daraja kukatisha Lake Tanganyika Ili kuunganisha Tanzania na DRC it makes sense
Angalau hapo tutatengeza ajira nyingi na tutaingiza FOREX. Maana Mizigo yote ya kutoka Dar Port kwenda Congo itapita hapo, na Mizigo ya Kutoka Congo kwenda Dar Port nayo itapita hapo....Hizo ndio project za kuongelea.
 
Kama tu kwa miradi midogo tunayoendelea nayo hali imekuwa tete kiasi hiki, sembuse mradi mkubwa huo wa kujenga daraja Dsm hadi Unguja?!
Hebu tuweni serious jamani
 
Wakati Simba walipocheza fainali na Stella Abidjan ulikua hujazaliwa bado.
 
Daraja haliwezi kuwa na hasara tu bila faida!
Wewe ndiyo hujapevuka kabisaa bora ya mleta uzi.
Amezungumzia hasara upande wa gharama. Faida zitakuwepo pia....wapemba kusafirisha Nazi kwa baiskeli had dar
 
Japo hata sijui hili suala la daraja limetokea wapi ILA,
KWANGU HILO NAONA HALINA UMUHIMU KWA SASA KWANI KUNA CHANGAMOTO KUBWA ZAIDI KWA WANANCHI
hivi kweli katika Nchi ambayo bado baadhi ya wanafunzi wanakaa chini au hatuna fedha hata za kuajiri waalimu wa Hesabu kitu kinachopelekea kupoteza Vipaji muhimu kwa nchi, Mtu anawazia daraja ambalo eneo husika tayari lina mbadala wa Boat za kisasa & Ndege?
Ni heri hiyo hela ifufue viwanda ILI Vijana wetu wapate ajira; hela ikipatikana kupitia kodi hata kama ni miaka 35 ijayo daraja litafikiriwa
 
[QUOTE="Ndalilo, post: 46237098, member: 122228

Kisha muingie gharama kwaajili ya wao kuvuka tu?

Naona tumeamua kufuga MCHWA na KUPE.[/QUOTE]
 
Kisha muingie gharama kwaajili ya wao kuvuka tu?

Naona tumeamua kufuga MCHWA na KUPE.

Kumbe likijengwa na kukamilika sisi wa Bara hatutaruhusiwa kuvuka, watavuka wao tu.

Kama ndio hivyo hata mimi siungi mkono
 
Dar-Unguja ni takriban kilometer 85. Tuna madaraja muhimu sana ya kuunganisha mkoa kwa mkoa au wilaya kwa wilaya yenye urefu wa mita 20 au 50 tu na tumeshindwa kuyajenga leo hii tunafikiria kujenga daraja la km 85?!

Kwanini tusipanue bandari zetu na kuimarisha usafiri wa majini kwa kuweka boat kubwa na nyingi ili gharama zipungue?

Daraja la Kigogo Busisi pekee lenye urefu wa kilometer 3.2 tu kimetigharimu billioni 700 je km 85 tena juu ya bahari ni trilioni ngapi?! Ni zaidi ya trillion 10! Hii ni gharama ya kutosha kujenga SGR kutoka Dar hadi Arusha au Kigoma! Tuachane na kujenga madaraja kama mapambo, tuache kabisa hailipi!
Uzuri maneno yako sio msaafu kwenda huko
 
Ni Mpango wa hovyo na WA uhuni tuu.Kama Kuna ulazima.bora kujenga Daraja kukatisha Lake Tanganyika Ili kuunganisha Tanzania na DRC it makes sense
Nani akubali kujenga wakati ndo wanaingiaga ndani ya maji deep kuchimba uchawi wao wapate vyeo
 
Kumbe likijengwa na kukamilika sisi wa Bara hatutaruhusiwa kuvuka, watavuka wao tu.

Kama ndio hivyo hata mimi siungi mkono
We wa bara unaenda kufanya nini cha maana kule?
 
We wa bara unaenda kufanya nini cha maana kule?
Tunauzaga korosho, ice cream za ukwaju, tunauza ma apple, mobile kiosks, mama ntilie. Kuna wenzangu wanauza baa, wengine papuchi, kuna wafanyakazi wengi wa mahoteli. Kwenye sekta ya ujenzi, wengine wanasafirisha furniture kutoka Tanga na kadhalika na kadhalika siwezi kutaja vyote.
 
Ni Mpango wa hovyo na WA uhuni tuu.Kama Kuna ulazima.bora kujenga Daraja kukatisha Lake Tanganyika Ili kuunganisha Tanzania na DRC it makes sense
je unajua kwamba Lake Tanganyika ni la pili duniani kwa kuwa na kina kirefu kwenda chini?

siyo rahisi kujenga hapo kama unavyodhania
 
je unajua kwamba Lake Tanganyika ni la pili duniani kwa kuwa na kina kirefu kwenda chini?

siyo rahisi kujenga hapo kama unavyodhania
Kwani nani alikwambia nguzo za daraja Huwa zinakita chini ya bahari?

Kwa hiyo huko Zanzibar Dar nguzo zitafika chini ya Bahari si ndio? 🤪🤪

Uhandisi sio historia Mzee.
 
Back
Top Bottom