Kujenga na kumiliki nyumba ya kuishi ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini?

Hahahaha hahahaaa. Mkuu Kuna Mambo mawili
1.Ama hupendi wengine wawe kile ambacho wewe unacho?
Ama 2. Unaishi kwa ndugu,mama,n.k
Sasa kutokana na mazingira hayo utamshawishi Nani akuelewe?
Na je utawezaje kujimwambafai mkuu!!?????
Simlazimishi mtu anielewe, huu ni msimamo wangu. Kama wewe ulivyo na msimamo wako. Naishi kwa shemeji mkuu, acheni woga.
 
Za kuambiwa changanya na zako
 
Hivi mnajua kula kulala huwa hajui thamani ya kitu chochote kwa mfano :- Hawajui thamaani ya kula yao,vaa yao,lala yao, aamka yao n.k kwahiyo msimlaumu saaaaanaaaa mleta mada
 
Ingekuwa rahisi hivyo si kila mtu angekuwa tajiri mtaani?
 
Po
Simlazimishi mtu anielewe, huu ni msimamo wangu. Kama wewe ulivyo na msimamo wako. Naishi kwa shemeji mkuu, acheni woga.
Pole Mkuu.NAISHI KWANGU KWENYE TEMBE LENYE SLAB YA UDONGO
 
Kanunue hisa,ingia ubia na wanaojua biashara au jenga fremu za kupangisha.
Mafremu yaliyotapakaa huko mitaani na hayazalishi ndio akili?

Hisa nazo si zina vihela vya mboga tuu hakuna pesa ya maana
 
Baishara huwa ni salama kwa mtu mwenye mtaji mkubwa na aliye diversify vyanzo vyake tofauti na hapo mtu utarudi kule kule ulikokuwa .

Ndio maana wanaojiita Wana biashara eti nzuri vimtaji vyao wengi ni 5-10 mln sasa hapo si waganga njaa tuu hao kuna pesa hata ya kwenda vacation mwisho wa mwaka?
 
Haiwezekani kila mtu akanunua Eicher kwa sababu kila mtu anaangalia uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za fursa kadhaa ndio maana lazima tofauti iwepo.

Binafsi ukinambia biashara nazotaka ni hizo za real estates, Ukandarasi,financial na kuuza madawa ya binadamu/ mifugo na kilimo na mwisho kilimo/ufugaji wenyewe.
 
Na pia kwenye hyo milioni 5 mpaka 10 unajenga nyumba gan? Maana watumishi wengi hukopesheka kias hcho kutokana na mishahara duni wanayo pata.
 
Na pia kwenye hyo milioni 5 mpaka 10 unajenga nyumba gan? Maana watumishi wengi hukopesheka kias hcho kutokana na mishahara duni wanayo pata.
Unajenga taratibu ndani ya miaka kadhaa nyumba ya 30mln inaisha .

Watumishi Wana salary na Wana uhakika wa mwisho wa mwezi.
 
Exposure na lugha na mfumo wa maisha yenye mentality za kijamaa ndio yamechangia
 
Ni bora hadithi za kilimo cha matikiti kwa eka kuliko kuzika pesa chini.
Inategemeana na tafsiri yako ya kuzika pesa, maana thamani ya pesa ni kwenye vitu vinavyoonekana.

Binafsi nikiwa kwangu ndio nakuwa na utulivu wa kupanga na mipango ikapangika na ikatekelezeka kuliko kubanana kwenye nyumba za watu.
 
Mimi naona kuwa na nyumba ni muhimu sana kama huna kipato cha uhakika. Ila kama una uwekezaji wenye uhakika sidhani kama kuna haja ya kukimbilia kujenga
Asiye na kipato cha uhakika si ndio anatakiwa awekeze kwenye biashara ili apate zaidi sasa akitumia mtaji alionao kujenga anwezaje kuwekeza na kuwa na kipato cha uhakika?
Kwa maana nyingine umesema tajiri aendelee kuwa tajiri na masikini abaki na umasikini wake.

Mimi nadhani hapao ni vice versa
Asiye na kipato cha uhakika aelekeze nguvu na akili zake zote kuwekeza na kujijenga kiuchumi na aliye na uwekezaji wa uhakika hakuna shida akiamua kujenga nyumba ya kuishi.

Kwangu mimi shida si kuwekeza shida ni "Elimu ya uwekezaji"
kundi kubwa la watu hasa wa kipato cha chini na cha kati wanakosa elimu na ujuzi wa uwekezaji hii inapelekea kufeli mara kwa mara kwenye biashara na wengine wanawaangalia hao(waliofeli) kama mifano.

Kwenye kila biashara ambayo mmoja analalamika ilimwangusha na kumpa hasara kuna mwingine biashara hiyo hiyo imemtajirisha na anifanya mpaka leo kwenye hiyo nchi na sera hizo hizo anazolaumu mwingine.
Bado unadhani shida ni sera au sheria nk
Shida ni kutokuwa na taarifa sahihi na za kutosha za biashara/uwekezaji unaotaka kufanya.
Watu wengi wanatanguliza fedha kwenye biashara kabla ya kuwekeza "muda" na kutafuta ujuzi/uzoefu.
 
Unajenga taratibu ndani ya miaka kadhaa nyumba ya 30mln inaisha .

Watumishi Wana salary na Wana uhakika wa mwisho wa mwezi.
Miaka kadhaa mingap? Unajua mwalimu wa shule ya msingi mwenye take home ya 340k akichukua hyo mil 10 kwa makato ya 200k kila mwezi anabaki na 140k kwa miaka 7..
Huyo mtumishi akiwa na familia inayo mtegemea pia ana ndugu wanamtegemea..ataishije kwa kipindi chote hicho na hana posho wala marupurupu yoyote.
Na mbaya zaid nyumba haitaisha kwa pesa hyo..ataishi kwa kuacha kadi mitaani na kuwa omba omba..

Hyo ndo hali halisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…