Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,913
Sawa basi komaa hivyo hivyoKwangu woga ni mapungufu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa basi komaa hivyo hivyoKwangu woga ni mapungufu.
Simlazimishi mtu anielewe, huu ni msimamo wangu. Kama wewe ulivyo na msimamo wako. Naishi kwa shemeji mkuu, acheni woga.Hahahaha hahahaaa. Mkuu Kuna Mambo mawili
1.Ama hupendi wengine wawe kile ambacho wewe unacho?
Ama 2. Unaishi kwa ndugu,mama,n.k
Sasa kutokana na mazingira hayo utamshawishi Nani akuelewe?
Na je utawezaje kujimwambafai mkuu!!?????
Za kuambiwa changanya na zakoKuwa na maamuzi sahihi ni kipaji:
Watu A, B, C, D,E, F walikopa bank, kila mmoja sh. 20m kwa marejesho ya jumla ya sh. 36m kwa muda miaka 6, Kila mmoja aliamua kuwekeza fedha yake kama ifuatavyo:-
Mtu A
Mtu B
- Aliamua kuwekeza fedha yote kwenye ujenzi wa nyumba, na nyumba haikumalizika iliishia kwenye kupaua.
Mtu C
- Aliamua kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba ndogo,na ilimalizika na hatimaye aliweza kuhamia
Mtu D
- Aliwekeza milioni 10 kwenye ujenzi na kumi kwenye biashara ya kuuza vilevi
Mtu E
- Aliwekeza fedha yote kwenye ujenzi wa ofisi ya ushonaji,ofisi imekamilika ila vitendea kazi bado kukamilisha
Mtu F
- Aliwekeza fedha yote kwenye usafiri wa kutembelea
- Aliwekeza fedha yote kwenye bashara ya vifaa vya ujenzi
Swali,je baada ya miaka sita (6) hawa watu (A,B,C,D,E,F) ni yupi atakuwa na maisha ya kuridhisha?
Ingekuwa rahisi hivyo si kila mtu angekuwa tajiri mtaani?Duniani tunapita tu, sasa kwa nini nijenge njiani?🙂🙂🙂🙂, Mimi masuala ya kujenga nyumba, mfano ya milioni 70, halafu niipangishe kwa laki 3 au laki 4 nipate hizo kodi.. kwanza inategemea na niliko ijenga (hata nikiishi mwenyewe baado).. hesabu zake ni baada ya miaka 15 au 17 ndo narudisha milioni 70 yangu niliyo jengea, hapo sijaweka hela niliyo nunulia kiwanja, repair, kodi ya ardhi na kodi ya majengo ya serikali na asilimia zingine.
Sasa hela hiyo si bora nika fanyie biashara ndani ya muda huo wa kusubiri kodi izalishe faida na mafaida.. au hela nilio weka irudi mara buku.. Milioni 70 ntakayo wekeza kwenye biashara ni lazima italeta faida kubwa mara idadi itakayo jizungusha.. potelea mbali mawazo ya kupata hasara..(biashara haidanganyi ukiwa serious na una imani) kwan ukijenga likaja tetemeko au bomoa bomoa na hulipwi fidia kama wale wa kimara ile inakuaga ni faida ?
Pole Mkuu.NAISHI KWANGU KWENYE TEMBE LENYE SLAB YA UDONGOSimlazimishi mtu anielewe, huu ni msimamo wangu. Kama wewe ulivyo na msimamo wako. Naishi kwa shemeji mkuu, acheni woga.
Yote maisha kikubwa uhai.Po
Pole Mkuu.NAISHI KWANGU KWENYE TEMBE LENYE SLAB YA UDONGO
Karibu kwenye matembe mkuu RRONDO hata ufanye ka tour ka utalii tu bwana karibu sanaYote maisha kikubwa uhai.
Kwani biashara zingine ni za kugangia nini?Biashara utakayoanzisha baada ya kujenge nyumba mara nyingi ni ya kuganga njaa tu si kwa ajili ya mafanikio makubwa.
Mafremu yaliyotapakaa huko mitaani na hayazalishi ndio akili?Kanunue hisa,ingia ubia na wanaojua biashara au jenga fremu za kupangisha.
Baishara huwa ni salama kwa mtu mwenye mtaji mkubwa na aliye diversify vyanzo vyake tofauti na hapo mtu utarudi kule kule ulikokuwa .Kuna swala pia la kutambua nyakati majira na fursa. Kwa mfano, wakati mimi naanza kupata pata pesa angalau, viwanja vilikuwa vinapatikana kuanzia mbezi makonde , mbezi jogoo kuelekea tegeta , kwa bei chini ya tzs 3,000,000.
Wakati huo mimi niliamini katka kufanya biashara na kupata pesa ambayo kwayo jambo la 'ununuzi wa kiwanja na ujenzi wa nyumba lingerahisika. Kwa bahati mbaya, kabla malengo hayajatimia biashara zikayumba na mpaka leo zina survive, na 'sijaweza 'kupata kiwanja maeneo hayo, maana sasa bei haishikiki.
Kwa hiyo maamuzi mengine ni vizuri yakafanyika katika mu da muafaka ili kuepusha majuto ya baa dae , maana mambo na /maisha kwa ujumla yanaweza kubadilika usivyotarajia..
Haiwezekani kila mtu akanunua Eicher kwa sababu kila mtu anaangalia uwezo wake wa kukabiliana na changamoto za fursa kadhaa ndio maana lazima tofauti iwepo.hata kujenga nyumba ya kupangisha bado sio uchaguzi mzuri kibiashara.
mfano nyumba uliyojenga kwa 80mln tabata,unawezapangisha kwa 250-300 kwa mwezi.
300×12=3.6ml÷ 80mln=biashara kichaa.
wakati eicher la 80ml linaingiza 4.5ml kwa mwezi.
4.5mln×12=54 mln
ndani ya miaka 2 tayari hela imesharudi na hapa ni kama si mkataba,kama ni mkataba unaachia gari ukiwa na hela nyingi zaidi.
nyumba si uwekezaji mzuri kabisaa,labda kwa malengo ya muda mrefu.
Na pia kwenye hyo milioni 5 mpaka 10 unajenga nyumba gan? Maana watumishi wengi hukopesheka kias hcho kutokana na mishahara duni wanayo pata.Baishara huwa ni salama kwa mtu mwenye mtaji mkubwa na aliye diversify vyanzo vyake tofauti na hapo mtu utarudi kule kule ulikokuwa .
Ndio maana wanaojiita Wana biashara eti nzuri vimtaji vyao wengi ni 5-10 mln sasa hapo si waganga njaa tuu hao kuna pesa hata ya kwenda vacation mwisho wa mwaka?
Unaweza Jenga kama huna pesa?Tengenezeni Future ya watoto wenu wakuu,acheni kukimbilia kuzika pesa..acheni ubinafsi..matokeo yake watoto wanakuja kuanza upya as if hakuwa na wazazi..
Unajenga taratibu ndani ya miaka kadhaa nyumba ya 30mln inaisha .Na pia kwenye hyo milioni 5 mpaka 10 unajenga nyumba gan? Maana watumishi wengi hukopesheka kias hcho kutokana na mishahara duni wanayo pata.
Exposure na lugha na mfumo wa maisha yenye mentality za kijamaa ndio yamechangiaWatanzania wengi hawana mawazo ya kufanya biashara za maana, wengi wanaofanya biashara hasa ndogo ndogo na umachinga ni baada ya mambo mengine yote kushindikana.
Watanzania wengi ikiwemo pamojavna wewe wanaamini mafanikio yanapatikana kwa kusoma kisha kuajiriwa serikalini, ujenge nyumba.
Inategemeana na tafsiri yako ya kuzika pesa, maana thamani ya pesa ni kwenye vitu vinavyoonekana.Ni bora hadithi za kilimo cha matikiti kwa eka kuliko kuzika pesa chini.
Asiye na kipato cha uhakika si ndio anatakiwa awekeze kwenye biashara ili apate zaidi sasa akitumia mtaji alionao kujenga anwezaje kuwekeza na kuwa na kipato cha uhakika?Mimi naona kuwa na nyumba ni muhimu sana kama huna kipato cha uhakika. Ila kama una uwekezaji wenye uhakika sidhani kama kuna haja ya kukimbilia kujenga
Miaka kadhaa mingap? Unajua mwalimu wa shule ya msingi mwenye take home ya 340k akichukua hyo mil 10 kwa makato ya 200k kila mwezi anabaki na 140k kwa miaka 7..Unajenga taratibu ndani ya miaka kadhaa nyumba ya 30mln inaisha .
Watumishi Wana salary na Wana uhakika wa mwisho wa mwezi.