Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

What if it's a mortgage won't it be termed as a liability for the foreseeable term?
It will be an asset in a specific period of time let say 5 years after then it will automatically change to be an asset soon after all the debts cleared.
 
All in all nyumba ni muhimu uanweza jenga na kupangisha iyo kodi unapanga sehem karib na kazin kwako
 
Haya tajiri endelea kuponda pesa kesho zingine zitakuja.
Mwenzako nakufundisha kitu ambacho nimewahi kushuhudia na nimeyapitia yote wewe unaleta mawazo ya kudanganyana vijiweni na hesabu za kwenye makaratasi kama kilimo cha matikiti.
Mimi hata sio tajiri, ni jobless tu ninaejitafuta kitaa. Ila kujenga nyumba kwa miaka 5+ kwa kipato cha kutegemea wanaume wenzako huo ni us*nge ambao mimi siwezi kuufanya.

Nyumba ya 50m ni biashara yenye kukuingizia 3m minimum p/m. Unaifukia chini then unaendelea kupigia magoti wanaume wenzio ili family yako ile.

Huu si ukichaa.
 
Kwa hiyo na kulala kwenye nyumba za wanaume wenzako halafu mwenye nyumba anakupangia masharti na kukufokea mbele ya watoto wako ndio ujanja?
 
Kwa hiyo na kulala kwenye nyumba za wanaume wenzako halafu mwenye nyumba anakupangia masharti na kukufokea mbele ya watoto wako ndio ujanja?
Hivi wenzetu mnapanga nyumba zip hizo ambako mnafokewa?? Au kule uswazi??
 
Kwa hiyo na kulala kwenye nyumba za wanaume wenzako halafu mwenye nyumba anakupangia masharti na kukufokea mbele ya watoto wako ndio ujanja?
Nyumba ya kupanga ni biashara, tunakubaliana terms, tukishindwana naenda kupanga nyumba nyingne. Yani mjini zilivojaa nyumba nije nifokewe na mstaafu ambae anategemea kodi yangu kuishi!!?

Umasikini wa nchi yetu unaanzia kwenye vijana bellow 35 kushindwa kujifunza kupoteza kabla haujafika serikalini. We love to play safe, kwamba nijenge ili kazi ikipotea au nikifa, family yangu iwe na hifadhi. mshahara wenyewe kipato chenyewe 2m. Unatumia 5yrs kujenga. Huo ni wendawazimu.

Huo muda ungetumia kujifunza biashara, hata kama ungepoteza, miaka 3 ya mwanzo bado ungefanikiwa tu mwaka wa 4.

Family za kitanzania tuna shida mahali sio bure. Mi familia ilitumia not less than 10m kunisomesha, nilipomaliza nilipeleka business idea kwa aliyekuwa ananilipia ada (bro) la kama 2.5m akasema hana.

Hapo ndiyo nilijua bado tuna mlima mrefu wa kuupanda.
 
Mimi nilianza kujenga nyumba na sasa hivi najifunza biashara hapo kuna ubaya gani?kama unadai kwenye biashara kuna mafanikio kwani na mimi si nitayapata hayo mafanikio au mimi nitanyimwa hayo mafanikio kwa vile tu nilianza kujenga nyumba mwanzoni?
Haya baadae umemaliza kusoma unampiga kibomu mtu ambaye hajui biashara wakati wewe una knowledge ya biashara unadhani huyo mtu atakuamini vipi kama hiyo pesa yake itakuwa salama na haitopotea?Ilitakiwa umuonyeshe mfano wa projects ulizozianza mwenye ili kuprove kwamba una knowledge ya biashara ndipo mtu atakuamini
 
Ukishakua una miliki familia ya watu wa nne tu, utajua ubaya na uzuri wa nyumba ya kupanga, na ubaya na uzuri wa kumiliki nyumba yako.

kuna kero kumkusanyia mtu fedha milion, kila baada ya miezi sita, ukikaa nyumba kupanga miezi inakimbia sana.
Mbaya Zaidi, anakuja mtu anakuja kukupa miongozo juu ya utunzaji wa nyumba yake.
 
Mimi nilianza kujenga nyumba na sasa hivi najifunza biashara hapo kuna ubaya gani?kama unadai kwenye biashara kuna mafanikio kwani na mimi si nitayapata hayo mafanikio au mimi nitanyimwa hayo mafanikio kwa vile tu nilianza kujenga nyumba mwanzoni?
Haya baadae umemaliza kusoma unampiga kibomu mtu ambaye hajui biashara wakati wewe una knowledge ya biashara unadhani huyo mtu atakuamini vipi kama hiyo pesa yake itakuwa salama na haitopotea?Ilitakiwa umuonyeshe mfano wa projects ulizozianza mwenye ili kuprove kwamba una knowledge ya biashara ndipo mtu atakuamini
Tatizo sio kujenga. Tatizo ni kipato cha 1.5m dar afu uanzishe ujenzi wa 50m. Project itakayochukua 5+yrs. Hii nyumba kama ulianza kuijenga ukiwa 32 utaimaliza ukiwa 38. Huu sio umri wa kujifunza kitu kipya wala kutake risks, maana majukumu ya family tayari yalishakomaa. Au wewe ulishamuona mtu anajifunza biashara akiwa na miaka 40+?

Ningemuonyesha project nilizozifanya kwa mtaji upi? Mkuu unaona sawa kutupa 10m afu ukimaliza ukapange foleni kama manamba kulilia kibarua cha mshahara wa 500k?
 
Mimi hata sio tajiri, ni jobless tu ninaejitafuta kitaa. Ila kujenga nyumba kwa miaka 5+ kwa kipato cha kutegemea wanaume wenzako huo ni us*nge ambao mimi siwezi kuufanya.

Nyumba ya 50m ni biashara yenye kukuingizia 3m minimum p/m. Unaifukia chini then unaendelea kupigia magoti wanaume wenzio ili family yako ile.

Huu si ukichaa.
50 m then utafute 3m per month, huo ni uwenda wazimu.
Maybe 15-20m hapo, speaking from experience
 
Boss una mawazo positive sana and for addin up wahindi na arabs especially wahindi wanafanya sana hizo mambo
Wanafanya hivyo sababu familia zao zina upendo ndani yake na wanaishi pamoja hata kushirikiana inakuwa rahisi,lakini jaribu wewe kuchukua hata mdogo wako tu asimamie mradi wowote utalia kaka
 
Ukikopa mil 100, ukaiweka UTT , baada ya miaka 5 unakua na zaidi ya mil 300. lakini ukijenga nyumba ya mil 100 baada ya miaka 3 nyumba hiyo itakua na dhamani ha mil 50
Ingekuwa rahisi hivi wenye malori wangeacha biashara.
Utt faida yake kwa mwaka ni 12% ambayo ndani ya mwaka unapata faida 12m
.
MWaka jnaofuata ni 112×12% =s
Mwaka wa 3 ni s×12% .

Ikizidi sana ni 50m, so unapata daida lakjn c mara 3
 
Sasa wewe ukiona umekaa tu unangojea mtaji kisha ndio uanzishe mradi jua wewe bado hujakwiva kwenye mambo ya Business skills kama unavyojinasibu mwenyewe,mtaji huwa ni kitu cha mwisho kabisa kwenye projects tena inatakiwa projects zako mwenyewe ndio zikupe mtaji ukitumia hela za mtu mwingine ytazitapanya tu hautazijali maana hauna uchungu nazo
 
Habari,

"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko", njia hii na mawazo haya yamekuwa kwa vijana wengi wanaoanza maisha, hususani waliobarikiwa kupata ajira au biashara zao binafsi ambazo zinawapa kipato flani cha kuendesha maisha yao. Kwa uzoefu wangu hii imekuwa kati ya sababu moja kubwa zinazosababisha watu kuwa maskini na kushindwa kufikia uhuru wa kifedha.

Lakini tujiulize swali la msingi, kwanini watu wengi wameamua kuchagua njia hii ya maisha. Nimefanikiwa kuwahoji watu wengi kidogo kuhusu hili na majibu niliyoyapata mengi yalikuwa kama ifuatavyo:

  • Gharama ya kupanga nyumba ziko juu sana, ni bora kujenga ya kwako.
  • Nyumba ni asset.
  • Usafiri ni shida sana eneo niliko jenga ni bora kuvuta gari yangu.
  • Mama/baba mwenye nyumba ana gubu sana.
  • Nikiwa na kwangu nakuwa na uhuru mkubwa sana.
  • Siku nikifukuzwa kazi au biashara ikiyumba nibaki na pakulala na familia yangu.

Sababu hapo juu nyingi ni za maana kabisa ila tatizo ni kwamba njia zilizotumika kutatua hizo changamoto zinaongeza changamoto zaidi, kivipi?. Ngoja tujadili mambo machache kuhusiana na maisha ya watu wengi hususani mijini (e.g. Dar):

  • Wengi wananunua viwanja maeneo ya mbali kutoka mahali wanapofanyia shughuli zao zinazowapa kipato.
  • Baadhi ya hayo maeneo yana changamoto za miundombinu ya maji, umeme, barabara na hata kiusalama.
  • Wengi wanajenga kwa kuunga unga sana, unaweza jenga nyumba hata miaka sita au zaidi. Kuna msemo wanasema "nyumba haiishi".
  • Nyumba nyingi wanazojenga watu kukaa zinakuwa ni kubwa na za kifahari bila kukumbuka lengo la mwanzo lilikuwa ni makazi tu na sio jengo la maonesho (Hapo utajibiwa kuwa tunajenga mara moja ya kuzeekea)

Kuzingatia hizo hoja hapo juu, yafuatayo yanakuwa ni matokeo ya gharama za maisha baada ya huyu mtu kuhamia kwake:

  • Gharama za usafiri au mafuta zinakuwa juu ukilinganisha na awali.
  • Mazingira yanakuwa sio rafiki kwa familia kuishi, maana nyumba nyingi zinakuwa bado hazijaisha (Wengine wanasema unakuwa unaishi site).
  • Kama una gari, gharama za matengenezo zinakuwa juu kwa sababu ya pengine barabara kuwa mbaya, lakini kwa kuwa unasafiri umbali mrefu kila siku, basi hata service ya gari utafanya mara nyingi zaidi.
  • Pia kama una gari utalazimika kuendesha gari umbali mrefu kila siku, hii si nzuri kwako kiafya.
  • Gharama za umeme na maji pia zinaweza kuongezeka kwa kuwa nyumba ni kubwa sasa na pengine maji hayajafika.
  • Maeneo mengine hata watu hawajahamia wengi hivyo hata usalama unakuwa hatarini.
  • Mara nyingi unaweza ukajikuta mbali na huduma bora za kijamii ikiwemo hospitali, shule, n.k.

***NOTE: Gharama zinaweza kuongezeka ukilinganisha na mwanzo.

Kwanini kuna hofu ya kuwekeza hizo pesa?

Tujiulize swali hili la msingi. Ni kweli baadhi ya watu wanatamani sana kuffanya biashara, lakini wengi wanasema, BIASHARA HAZITABIRIKI. Ni kweli kabisa, lakini ukweli ni kwamba hilo sio tatizo la watu kutokuwekeza.
SHIDA KUBWA NI WATU KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA. Hili ni jambo la muhimu sana kwa vijana kupata elimu. kwanza kabisa sio kweli kwamba ukitaka kuwekeza ni lazima ukafanye biashara fulani kama kuuza nguo, vinywaji au duka la mangi. Unaweza ukafanya uwekezaji kwa njia nyingi sana ambazo hazitahitaji your active time kuweza kusimamia ila mwisho wa siku ukaja kuwa na uchumi mkubwa kabisa. Uwekezaji huu ni kama mifano ifuatayo:

  • Kununua viwanja na mashamba (Kumba muda unavyokwenda ardhi inapanda thamani lakini nyumba inashuka thamani)
  • Kununua hisa za makampuni
  • Tressury Bonds and Bills
  • Mifuko ya uwekezaji ya pamoja (e.g. UTTAMIS)
  • Fixed deposits accounts
  • Kuwekeza kwenye elimu (Hii sio lazima zile za darasani, inaweza kuwa hata kujiendeleza katika fani flani)
  • N.k.

La muhimu ni kupata elimu sahihi ya mambo ya fedha ili ujue jinsi ya kufanya maamuzi ni vipi utumie pesa yako.

Ngoja nitoe mfano halisi mmoja ulio hai kabisa kwa lengo la kupata uhalisia wa ninacho kisema:

Mwaka 2013 niliajiriwa mahali na tulikuwa kama waajiriwa sita wapya katika hiyo kampuni, mwenzetu mmoja alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo ya fedha, na mara nyingi alikuwa anatushauri kuhusu haya mambo lakini tulikuwa tunamuona kama kachanganyikiwa: Mimi na wenzangu wengine wa tano tulikwenda mahali tukanunua viwanja na kuanza kujenga kwa kasi sana na badae tukachuku na mikopo kuongeza kasi hiyo. Kwa haraka haraka kwa wastani tuliweza kutenga kama milioni moja kwa mwezi kila mmoja wetu kwa ajiri ya miradi ya ujenzi. Mungu si athumani baada ya miaka mitatu paka minne wote watano tukawa tumehamia kwenye site zetu huku tukiendelea na finishing.

Jamaa alikuwa kila mwezi anaweka milioni moja kwenye mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamoja na alikuwa anapata average interest kama ya 11.85% kwa mwaka. Badae akawa ananunua na bond za serikali pamoja na mambo ya kununua mashamba mbali kidogo na mji yakichangamka anakata na kuyauza. Kiufupi jamaa ana zaidi ya milioni 200 kwenye mfuko anaoweka pesa pamoja na kuwa na asset ya viwanja na mashamba na benki ana pesa chafu.

Turudi kwetu tuliojenga na sasa tuna mikoko yetu, umbali wa kwenda na kurudi nyumbani ni 50 Km kila siku. Na pia siwezi pata picha ile hofu ya kwamba nikiachishwa kazi bado ipo maana siwezi nikala nyumba.

Kwa ajili ya muda niishie hapa kwa leo, nipate mawazo ya watu wengine pia. Kiufupi mimi naona kuna mitaji mingi ya biashara na uwekezaji inapotea kwa huu mwamvuli wa kujenga na kununua hii mikoko.

Ahsanteni!!!
Ni elimu nzuri, lakini kama lengo la kuwekeza ni kwa ajili ya kuja kuwa navyo hivyo vitu, kama unaweza kuanza navyo anza navyo.

Hiyo faida ya asilimia 11 kwa mwaka, ndiyo unayotumia kulipa kodi ya pango, (jiulize kwann ww unapewa hiyo faida) gharama utakazotumia kufanya ujenzi itakuwa ni kubwa kuliko kama ungefanya b4.

Cha kujifunza hapa, "DO WHAT IS POSSIBLE AND COMES FIRST" kila kimoja kina faida endapo utakuwa serious,

Lakini pia zingatia nyakati e.g. kwa graduates au bachelor with fresh age anaweza kuanza na uwekezaji, lakini kwa mtu ambaye ameshaanzisha familia, ni vyema aanze ujenzi kwa ajili ya welfare ya familia yake, vinginevyo kuna hasara ambazo hazionekani kwa macho zitakazo athiri mkeo na watoto wako mkiishi kwenye makazi ya kupanga otherwise ukapange ushuani nyumba nzima yenye fence ambayo gharama yake ni mara 100 ukaishi site kwako.
 
Back
Top Bottom