Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Naona watu wengi humu ni wafanyakazi na ndio wananaounga mkono hoja ya ujenzi wa nyumba ya makazi dhidi ya biashara.
Kwangu mimi mfanyabiashara ni tofauti, huu wimbo wa kujenga nyumba ya makazi hata ukiniimbia kwa miaka 10 sitakuelewa.

Nitajenga pale tu malengo yangu ki biashara yatakapotimia.
Kama ninaishi vyema na familia yangu sioni haja ya kukimbilia kujenga nyumba just for Pride.
 
Hizo nyumba alizojenga trump ni za biashara na sio za kuishi yeye na hayo magari ya shabiby ni ya biashara! Watanzania wengi wanadhani kujenga nyumba ya kuishi ndo mafanikio bila kujua kujenga nyumba ya kuishi ni liability kubwa mno maishani!
 
Asee hongera sanaa, Mimi kwa Sasa teali na nimewekeza mfuko wa bond UTT, Sasa naitafutaa hati fungani, treasure Bond ya.miaka 20 au 25, then niache kibarua.. my target UTT ni kupata gawio la 2 mil plus..na treasure bonds mil 90 kwa mwaka. Gawio la UTT litanifanya niishi kama mtumishi wa serikari maana Kila mwisho wa mwezi tutakuwa tunakutana bank na watumishi wa serikari wao wakiwa wanasubiri mshahara Mimi nasubiri gawio.
 
Natamani kujua zaidi hii kitu. Mfano nikiwa na mill. tano nawezaje pata faida kwenye hiyo mifuko.
 
Hongera sana kaka
 
Natamani kujua zaidi hii kitu. Mfano nikiwa na mill. tano nawezaje pata faida kwenye hiyo mifuko.
Kama una Milioni tano approximately faida ni kama elfu 50 na chenji kwa mwezi.. UTT bond fund faida kwa mwaka ni 14.9%, Treasury Bond ya BOT inategemea unanunua wakati gani but huwa inakuwa 12% mpaka 13% kwa mwaka na mara chache sana inafika mpaka 15% inategemea wakati gani unanunua hati fungani hizo..
 
Na hii una kua unaipata maisha, au kuna muda maalumu. Na je unaweza ukawa unaongeza kila unapopata pesa nyingine ili kukuza faida? Maswali mengi nivumilie hii kitu naiskiaga tu.
 
Umeongea point mkuu...Ila sikiliza ma experts pia
 
Kujenga sio tatizo /kununua gar tatizo n pale unapojenga wakat ambao hauna stable income,hauna vyanzo vya uhakika vya kipato (specifically passive income)

Ukiwa na kipato cha uhakika,nyumba inasimama kwa miez 2 tu tena n nyumba sio kupanga matofali hizi mtu anajenga miaka 5 haijaisha anahamia huku fundi anapiga plasta [emoji28]

Nashaur hv,watu tuhakikishe tuna vipato endelevu na vya uhakika,ukishafkia uhuru wa kifedha utajenga na kuish popote na muda wowote

Binafsi ukinipa nyumba ya100M na investment inayonipa profit ya 1M monthly consistently nachkua hyo investment


Kujenga nyumba ya kuish kwa mkopo/‘mshahara n seriously mental problem.

Ama mtu unanunua kiwanja alaf ukiumwa au ukiuguliwa unakiuza [emoji28]
 
Kwa ujumla, mawazo ya wananzengo yanafanyakazi kulingana na mahali na hali ya maisha ya familia wanakotokea.

Mawazo yote ni mema na mazuri (Kujenga au kufanya biashara/investment/kuwa na gari kabla ya kujenga n.k) ilimradi yanatupeleka kwenye DHUMUNI/LENGO la MWISHO la mhusika=Maisha bora.

Maisha ni kuchagua na kwa kuwa tumeumbwa kila mmoja kwa madhumuni tofauti hapa duniani, wengine wawe MATAJIRI na wengi sana wawe MASIKINI.

Kila mmoja ashikilie kile anachokiamini na atafika kule atakako.
 
ARIRHI NI FACTOR MOJAWAPO YA UCHUMI ILA KAMA HUNA KITU UNAIFANYIA NI KAZI BURE...unaweza kufanya chochote kikakupa fedha....kuna eneo nilinunua nikaona nijenge fensi... nimepotezxa hela nina niaka kumi ninalo halijawahi nipa hata sent...hopu pekee niliyonayo labda nikiuza nitapata mtonyo wa maana ila hakuna jipya fedha niliyoiwekeza hapo ningejenga guest au nyumba za wapangaji mjini ningekuwa na maokoto kiaina.. kwa hio ardhi sio aset hadi pale utakapoiuza au kukuingizia hedha... kuwekeza kwenye ardhi nisawa na wanaowekeza kwenye mazao kwalengo la kupata faida tunaiita capital gain(sio biashara)mzee wangu kishimba alinifundisha miaka hio kuweka stock ya mchele so biashara....nunua then uza ukipanda unapanda nao ukishuka unashuka nao unaangalia faida tu.....tusijifariji na kumiliki naeneo yasiyokuwa na chochote ukifanyacho fuga hapo au fanya chochote..
 
looser mind set..... chakata hoja...
 
..ni kweli mkuu ukiweza plot unayonunua fanyia kitu kinachokuingizia pesa...ila kuwa na plot ni faida zaidi ya kuweka bank..pesa inayokaa bank tu kama akiba inaliwa na inflation na depreciation..pesa unayoiweka kwa plot inapambana na inflation na depreciation hasa maeneo strategic...matumizi ya plot hasa yenye title deed inaweza kuwa mengi ikiwepo kulima mazao kama mboga-mboga kibiashara hasa kwa kutumia greenhouse technology, kukodishia watu kwa busness kama kuosha magari, kufyatua tofali, gulio, etc; pia unaweza kuchukua hati yako ukaenda bank ukakopea mkopo na kufanya mambo mengine!

..kwenye eneo la mkopo kama plot umepata sehemu strategic na plot imekaa muda ikapanda bei unaweza kuchukua mkopo mkubwa na kununua bonds ambayo labda zina rate kubwa kuliko interest rate ya mkopo..then malipo ya bond yakawa yanalipa mkopo hadi muda wa kurudisha deni la bank unaisha na wewe unabaki na pesa&interest ya bond na plot yako...mfano plot ina thamani kuanzia 200m hii ukiichukulia bond ya 25yrs yenye rate ya 12.56% kwa sasa unaweza kabisa kulipa mkopo ambao labda umepata kwa bank au saccos wenye rate chini ya 10%.
 
schools, in economics, taught us that house is an asset, but Robert Kiyosaki, in his book told that a house is a liability, which is which!
 
schools, in economics, taugh us that house is an asset, but Robert Kiyosaki told in his book that a house is a liability, which is which!
 
Mdau sijui uko kwenye sekta ipi (umeajiriwa/biashara) dhumini kubwa la kujenga ni kuwa makazi au biashara sasa kama upo kwenye biashara dhamana (security) ni muhimu Sana hasa kama unataka kukuza mtaji wa biashara yako. Kwa namna gani unaweza kutunza pesa mfano upate zabuni ya 500m utasave kwa muda gani kiasi hicho zaidi ya kutumia taasisi za fedha kama benki kuhusu malengo ya benki nafikiri hauko sahihi huo ni mtazamo wako hasi juu yao mbona wengi wamefanikiwa kwa kuzitumia taasisi za fedha na kukuza biashara zao​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…