Kujenga Rahisi ukipiga hesabu za kwenye makaratasi ingia Site sasa Ndio utajua hujui hapo

Kujenga Rahisi ukipiga hesabu za kwenye makaratasi ingia Site sasa Ndio utajua hujui hapo

Gharama gani zote hzo mbona hazielewek,boma la vyumba vitatu halitakiw kuzid 10mil hapo umepaua kabisa,
 
Nimeiuliza chat gpt

Mfano nahitaji nyumba ya vyumba vitatu, kimojawapo kiwe master bedroom, kuna jiko, store na public toilet cheapest option nitatumia tofali ngapi? Akajibu 2000 ila niweke 5% wastage so 2500.

Nikajibu fanya cheapest estimations zaidi ya hii, akajibu tofali 900, ila unabadilisha aina ya msingi na msingi utachomoza 0.5 meter kutoka ardhini. Weka 5% wastage so ni tofali 950.

Naungana na wanaosema unaweza ukamjengea nyumba fundi
 
Screenshot_2024-12-24-21-48-42-502_com.openai.chatgpt-edit.jpg
 
Hayo makadirio ya fundi,
Unaweza jikuta unajenga nyumba Yako, afu fundi nae anajenga ya kwake.

Mpaka Siku unahamia, nae fundi anahamia kwake.
Alifanyiwa rafiki yangu mchezo na Contractor alikuwa mwanamke....alikuja stuka baada ya kupiga stori na kusema "dah namalizia nyumba yangu bwana, sasa hivi nafanya blundering, fundi kaniambia zinahitajika gypsum board SITINI NA TANO" hapo tulishtuka wote pale, anakuja kugundua fundi yule naye alikuwa anapandisha ya kwake, so alipigwa material mengi sanaa toka ujenzi unaanza ana alikuwa mbali na site. Hatari mkuu DeepPond
 
Sitasahau mimi na fundi wangu tulikaa tukapiga hesabu kila kitu gharama ilikuja m9 na laki4 tu
Maajabu ni kwamba nyumba hadi inamalizwa kuezekwa na hapo bado madirisha vigaena makorokocho kibao hesabu inasoma m23 na ushee nikaachia hapo kuandika na sitakaa niandike kitu kwenye ujenzi. Msimamizi ni mimi mwenyew
wewe kama mimi mkuu... nilianza naandika niliacha baada ya kuezeka. Yani boma na kuezeka ilikuwa milioni 19 pamoja na mashimo mawili ya choo. hapo ndipo niliacha kuandika rasmi. nahisi sasa hivi skimming, wiring, grills, milango na gypsum, na plumbering huenda nishafika thelatini na kitu
 
Back
Top Bottom