Kujenga ukiwa tayari una familia si mchezo

Kujenga ukiwa tayari una familia si mchezo

Dah nawashauri vijana kama uneweza kujenga ukiwa Bado hujaanza familia itakua Bora Sana kuliko kusubiri wakati majukumu yamekua mengi dah inasumbua Sana inaweza ata kuchukua miaka 10 kukamisha nyumba kila kitu
Ahsante sana mkuu kwa kutukumbusha sisi vijana ambao hatujao kufanya jambo hili mapema hata la nyumba ya vyumba vitatu then napiga pembeni ya nyumba vyumba viwili vya nje kama madarasa kwa ajili ya wageni nakuwa nimemaliza,hadi hapo kipato changu kitakachokuja kuwa imara Cha kupiga mjumba mkubwa
 
Kama watoto wenyewe ni wake sasa. Kwa uchepukaji ule unaweza kuta mshkaji alikuwa analelea wajuba.

Ni sawa na umnunulie gari mkeo afu wajuba wanaompa hela za mafuta ndio anawaona wana thamani... Mimi ndo maana sipendi kumiliki bastola...
[emoji38][emoji38] tukiwaza ayo bosi hatutafanya kitu xaxa
 
Dah nawashauri vijana kama uneweza kujenga ukiwa bado hujaanza familia itakua bora sana kuliko kusubiri wakati majukumu yamekua mengi dah inasumbua Sana inaweza ata kuchukua miaka 10 kukamisha nyumba kila kitu.
Itategemeana na source of fund/pesa kwa wengine wapo kwenye familia wanajenga na wengine wapo kwenye familia. Unaweza kutokuepo kwenye familia na ukashindwa kujenga endapo Huna chanzo cha kuaminika cha pesa
 
Dah nawashauri vijana kama uneweza kujenga ukiwa bado hujaanza familia itakua bora sana kuliko kusubiri wakati majukumu yamekua mengi dah inasumbua Sana inaweza ata kuchukua miaka 10 kukamisha nyumba kila kitu.
Inategemeana na familia yako, kama mume na mke wote mna kipato, haiwezi kusumbua.

Ila pia kama unajenga kabla ya juoa wakau usimalize kabisa ili wife naye awe sehemu ya project..

Hii inasaidia sana wakati wa majanga kama kifo, mara nyingi ndugu wakaisha jua mke hakushiriki basi kuna uwezekano mkubwa akafukuzwa na watoto kupata shida.

Ushauri wangu, weka mazingira mazuri ya ujenzi na na ikiwekena fanya mambo yote ya msingi ila usimalize kabisa..

Utanishukuru siku moja
 
Inategemea ila Bora ujenge kabisa kabla ya kuona kwasababu itakupa muda wa wewe kujiweka imara kiuchumi mfano umejenga una miaka 30 unaoa unamiaka 32 unajua inakusaidia mpaka unafika miaka 40 unakua mbali Sana kiuchumi kama unadiscipline ya pesa nzurii
 
Mkuu jenga nyumba ndogo, alafu balance watoto wasifuatane sana, pia usizae zaidi ya watoto watano
Watoto watano ? Mi nikadhani usizidishe watatu mkuu, unless una pesa nyingi, ukiwa na watoto watatu kuna kipindi itafika ada za watoto kwa mwaka ni 6M hapo hawajala hawajafanya kitu kingine chochote
 
Watoto watano ? Mi nikadhani usizidishe watatu mkuu, unless una pesa nyingi, ukiwa na watoto watatu kuna kipindi itafika ada za watoto kwa mwaka ni 6M hapo hawajala hawajafanya kitu kingine chochote
Kweli mkuu huyuu jamaa anasema tu five child sio MCHEZO kwanza msosi tu wa kila siku kwa kipato kidg wee sio kitoto
 
Kwa mshahara kweli ni changamoto, jikaze upate mtaji ufanye na biashara mkuu wewe sio mtumishi wa serikali milele.
Tatizo mtumishi wa umma anacho waza ni kujenga pekee na kusubr kufa..hafikirii hata future za watoto wake hapo baadae. Ni ubinafsi wa hali ya juu mnoo.
 
Kutawanya nguvu ni jambo linalo wapiga wengi na kufanya hata madogo wayaone makubwa.

FOCUS kwenye moja na usiruke ukurasa japo Story inaweza kukuchanganya kama kuona ukifananisha na kusoma.

FOCUS- AWARENESS- STICK TO THE PLAN-EMBRACE THE STORM
 
Back
Top Bottom