SoC04 Kujiajiri kwa mafanikio makubwa kunategemea shauku ya mtu mwenyewe kupenda kujiajiri kutoka ndani ya moyo wake

SoC04 Kujiajiri kwa mafanikio makubwa kunategemea shauku ya mtu mwenyewe kupenda kujiajiri kutoka ndani ya moyo wake

Tanzania Tuitakayo competition threads

La3

Member
Joined
Jul 29, 2022
Posts
17
Reaction score
17
Kujiajiri ni uwezo wa kuwa na chanzo cha kipato na kukiinua kutoka chini na kukiendeleza.
Kujiajiri ni kuzuri sana kama mtu mwenyewe amependa.

Sasa hapa hatutazami vijana wasomi tu, tunatazama vijana wote kwa ujumla (wasomi na ambao sio wasomi)
Kuwa msomi hakumaanishi anaweza kujiajiri.

Sasa mabadiliko yafuatayo ni lazima yafanyike kwenye eneo hili la kujiajiri ili vijana wetu wapate shauku ya kupenda kujiajiri;

1. Walimu wa ujasiriamali vyuoni ni lazima wawe na mradi hata mmoja wa mfano wa kuigwa Ili wafuzu kupata ajira ya ualimu wa ujasiriamali.

Katika suala la kujiajiri ujasiriamali hauepukiki;
Elimu ya ujasiriamali inapaswa kuwa nadharia na vitendo.
Sasa baada ya elimu ya nadharia darasani wanafunzi waende kwenye elimu ya vitendo,;
Hivyo basi sehemu ya kwanza na ya muhimu kwenda kufanyia mafunzo kwa vitendo ni kwenye mradi wa ujasiriamali wa mwalimu husika wa somo.
Kabla ya kutembelea miradi mingine kwa mafunzo zaidi.

kwa hiyo kuna ulazima wa kuwaondoa kazini wahadhiri wa kozi ya ujasiriamali na kozi nyingine za biashara vyuoni ambao hawana mradi hata mmoja wa mfano wa kuigwa.
(Hawa hawana sifa ya kufundisha masomo hayo, ni sawa na kufundishwa malezi ya watoto na mchungaji aliyefeli kulea watoto wake kimaadili).

Ili vijana wahamasike kupenda kujiajiri basi;
Sifa ya peke wanayotakiwa kuwa nayo walimu wa somo la ujasiriamali ni ;
Kuwa na mradi wa kijasiriamali angalau mmoja wa mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wake watakapoenda kutembelea mradi husika kwa mafunzo.

Kuajiri wahadhiri hawa wenye miradi yao binafsi na wanaolipa kodi kwa wakati kunaweza kuchangia mafanikio kwenye eneo hili la kujiajiri kwa sababu itawatia morali vijana kupenda kujiajiri hata kama wakiajiriwa.

Pia wanasiasa mfano; (wabunge, , mawaziri n.k) wanalipwa mishahara kwa kodi zetu na wanahamasisha vijana wetu kujiajiri wakati wao wameajiriwa. Hawa wote hawana haki wala hadhi ya kutuhamasisha kujiajiri.
Ili wapate hiyo sifa ya kuweza kuhamasisha wengine kujiajiri ni lazima wao wenyewe wajiajiri na hizo nafasi zote ziwe ni za kujitolea bila malipo, mapato yao yategemee shughuli zao walizojiajiri.

2. Mitaji
Changamoto ya vijana wengi kushindwa kujiajiri ni mitaji.

Nini kifanyike?
Zamani zile toka enzi na enzi urithi kutoka kwa wazazi ilikuwa ni ardhi.
Lakini Miaka kadhaa iliyopita wazazi walikuwa wakisikika wakisema urithi wa mtoto ni elimu kwa sababu ya uchache/ ufinyu wa ardhi.
Pia nafasi za ajira zilikuwepo za kutosha kwa sababu wasomi hawakuwa wengi sana kama Sasa.
Sasa mambo yamebadilika, hali ni tofauti, tatizo la ukosefu/uhaba wa ajira ni kubwa.
Pia changamoto hii inaongezeka kadri siku zinavyozidi kwenda mbele na ndio maana;
Leo hii ni kawaida nafasi 10 za ajira kugombaniwa na watu 1000.
Na ni tatizo la dunia nzima.
Kwa hiyo wazazi ni lazima wamuandalie mtoto urithi wa elimu pamoja na kumuandalia urithi wa mtaji wa kuanzia ujasiriamali (kujiajiri)

Soma kwa utulivu, hapa naongea na wazazi wa sasa na wale wa vizazi vijavyo;
Mfano kule Njombe, Iringa, Lushoto-Tanga, au Mbinga Ruvuma;
wazazi wanaweza kuwaandalia shamba la miti ya mbao, milunda, nguzo za umeme au miti ya parachichi angalau ekari moja au mbili kwa kila mtoto kama mtaji wa kuanzia badala ya kurithisha shamba tupu.
Mradi uwekezwe tangu akiwa elimu ya ngazi ya chini mfano hata darasa la kwanza.
Pamoja na kwamba vijana hawapaswi kufikiria urithi kutoka kwa wa wazazi;
Urithi wa mitaji ni kwa vijana wote, wapo waliosoma veta, chuoni na wengine hawajasoma kabisa.

Kama ardhi ni haba, basi wapande miti hiyo ili vijana wakihitimu chuo na wakakosa ajira ikatwe miti kiasi kadhaa na kuuzwa Ili kumpatia mtaji kijana wao.
Na sio wakihitimu chuo tu, hata wale ambao hawajasoma, watapata morali ya kupenda kujiajiri baada ya kupewa mitaji.

Kule Mbozi-Songwe, Mbinga-Ruvuma, Kilimanjaro au Kagera wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba la kahawa ekari moja kwa kila mtoto kama mtaji wa kuanzia

Kule Singida na Tabora wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba lenye mizinga kadhaa ya nyuki kama mtaji wa kuanzia kwa vijana wao.
Waandalieni urithi wa ardhi iliyoongezewa thamani kwa ufugaji wa nyuki.
Aamue yeye kuendeleza au auze aanzishe biashara nyingine.

Kule Makete-Njombe kuna wakinga wamewekeza mashamba ya miti Kwa ajili ya mitaji ya kibiashara kwa watoto na wajukuu.

Na vijana wengi wa makete wamepata mitaji kutokea kwenye mashamba hayo.
Hii imewahamasisha vijana wengi wa kikinga kupenda biashara na ujasiriamali.
Wazazi pia wawekeze kwenye soko la hisa.

NB; Kila mtu anayeleta watoto duniani kwa sasa anawajibika kufikiria kuandaa urithi wa elimu na mtaji wa kuanzia maisha.

3. Sapoti kutoka serikalini.
Ni kweli serikali imejitahidi kufanya vizuri katika kuwapatia vijana mikopo kwa vikundi mbalimbali;
Lakini ni muhimu ikalegeza na kuruhusu kijana mmoja mmoja kuweza kuchukua mkopo, sababu wanapokuwa kundi, ni rahisi mmoja wao kutoroka na kiasi cha fedha ambacho wamekopa kwa pamoja kama kikundi, anawaweka wenzake matatani.

4. Vijana wanaweza kujiajiri katika maeneo mengi, hasa ambao wana elimu au ujuzi nayo ni nzuri zaidi,
Mfano fundi umeme, fundi Bomba, fundi ujenzi

5. Mtu anapojiajiri anatakiwa atambue kwamba ana jukumu la kutengeneza ajira kwa wengine. unapaswa kutumia akili zaidi kuliko walioajiriwa.

6. Vijana wasiache asili yao;
Kwa mfano watu wanaotokea jamii za kifugaji ni vema wakajiajiri katika sekta ya mifugo.
Mfano wamasai, wasukuma, wanaweza kujiajiri kwenye ufugaji wa ng'ombe wa kisasa na kufanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawatokei kwenye jamii za kifugaji.

Kwa vijana wanaotokea jamii za wavuvi wajikite kwenye ufugaji wa kisasa wa samaki.
Ninaamini wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawatokei kwenye jamii za wavuvi n.k.
Hawa wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawatokei kwenye jamii za wafanyabiashara

Sio lazima wote tukimbilie biashara.

1715416113854.gif
 
Upvote 2
Walimu wa ujasiriamali vyuoni ni lazima wawe na mradi hata mmoja wa mfano wa kuigwa Ili wafuzu kupata ajira ya ualimu wa ujasiriamali.
Sawa, na pia tunaweza kuwa na walimu/waratibu wachache saana wa kudumu wa ujasiriamali (awe/asiwe na mradi haijalishi) lakini walimu wengi wawe wa ajira za muda. Anaalikwa mjasiriamali mwenye mafanikio anaelekeza analipwa chake huyoo anasepa kwenda kufundisha chuo kingine.
Maombi ya kufundisha na kuwapata wa kufundisha yataratibiwa na hao waalimu wa kudumu.

NB; Kila mtu anayeleta watoto duniani kwa sasa anawajibika kufikiria kuandaa urithi wa elimu na mtaji wa kuanzia maisha.
Umeelekeza vema sana aya kadhaa hapo juu kwa suala la mitaji. Wazo zuri

Lakini ni muhimu ikalegeza na kuruhusu kijana mmoja mmoja kuweza kuchukua mkopo, sababu wanapokuwa kundi, ni rahisi mmoja wao kutoroka na kiasi cha fedha ambacho wamekopa kwa pamoja kama kikundi, anawaweka wenzake matatani.
Shida ni moja, maendeleo ya kudumu zaidi yapo katika ushirikiano. Kwa kufanya hivyo tutaondoa eneo bora kabisa la vijana kujifunza ushirikiano wa kujenga makampuni yao. Titatue changamoto ya uaminifu badala ya kuondoa jukwaa la watu kujifunza kushirikiana katika uzalishaji.

6. Vijana wasiache asili yao;
Kwa mfano watu wanaotokea jamii za kifugaji ni vema wakajiajiri katika sekta ya mifugo.
Mfano wamasai, wasukuma, wanaweza kujiajiri kwenye ufugaji wa ng'ombe wa kisasa na kufanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawatokei kwenye jamii za kifugaji.

Kwa vijana wanaotokea jamii za wavuvi wajikite kwenye ufugaji wa kisasa wa samaki.
Ninaamini wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawatokei kwenye jamii za wavuvi n.k.
Hawa wana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kuliko wale ambao hawatokei kwenye jamii za wafanyabiashara
Umeiweka vema. Ahsante ndugu
 
  • Thanks
Reactions: La3
Sawa, na pia tunaweza kuwa na walimu/waratibu wachache saana wa kudumu wa ujasiriamali (awe/asiwe na mradi haijalishi) lakini walimu wengi wawe wa ajira za muda. Anaalikwa mjasiriamali mwenye mafanikio anaelekeza analipwa chake huyoo anasepa kwenda kufundisha chuo kingine.
Maombi ya kufundisha na kuwapata wa kufundisha yataratibiwa na hao waalimu wa kudumu.

Umeelekeza vema sana aya kadhaa hapo juu kwa suala la mitaji. Wazo zuri

Shida ni moja, maendeleo ya kudumu zaidi yapo katika ushirikiano. Kwa kufanya hivyo tutaondoa eneo bora kabisa la vijana kujifunza ushirikiano wa kujenga makampuni yao. Titatue changamoto ya uaminifu badala ya kuondoa jukwaa la watu kujifunza kushirikiana katika uzalishaji.

Umeiweka vema. Ahsante ndugu
Asante
 
kwa hiyo kuna ulazima wa kuwaondoa kazini wahadhiri wa kozi ya ujasiriamali na kozi nyingine za biashara vyuoni ambao hawana mradi hata mmoja wa mfano wa kuigwa.
(Hawa hawana sifa ya kufundisha masomo hayo, ni sawa na kufundishwa malezi ya watoto na mchungaji aliyefeli kulea watoto wake kimaadili)
Hahahahaaaaaah 😅😅😆 ilaa
Kama ardhi ni haba, basi wapande miti hiyo ili vijana wakihitimu chuo na wakakosa ajira ikatwe miti kiasi kadhaa na kuuzwa Ili kumpatia mtaji kijana wao.
Na sio wakihitimu chuo tu, hata wale ambao hawajasoma, watapata morali ya kupenda kujiajiri baada ya kupewa mitaji.

Kule Mbozi-Songwe, Mbinga-Ruvuma, Kilimanjaro au Kagera wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba la kahawa ekari moja kwa kila mtoto kama mtaji wa kuanzia

Kule Singida na Tabora wazazi wanaweza kuwaandalia watoto shamba lenye mizinga kadhaa ya nyuki kama mtaji wa kuanzia kwa vijana wao.
Waandalieni urithi wa ardhi iliyoongezewa thamani kwa ufugaji wa nyuki.
Aamue yeye kuendeleza au auze aanzishe biashara nyingine.

Kule Makete-Njombe kuna wakinga wamewekeza mashamba ya miti Kwa ajili ya mitaji ya kibiashara kwa watoto na wajukuu.

Na vijana wengi wa makete wamepata mitaji kutokea kwenye mashamba hayo.
Hii imewahamasisha vijana wengi wa kikinga kupenda biashara na ujasiriamali.
Wazazi pia wawekeze kwenye soko la hisa.
Umeeleza vizuri kwenye kupata mitaji ya mara moja tu.

Hapo haujagusia gharama zinazoendelea na bado kuna kuanguka na kuhitaji kuinuka tena mara kadhaa, je hiyo mitaji itatoka wapi?

Sapoti kutoka serikalini.
Ni kweli serikali imejitahidi kufanya vizuri katika kuwapatia vijana mikopo kwa vikundi mbalimbali;
Serikali sijui tuibane kwenye kuhakikisha mazingira ya kiuchumi na kisera yanakuwa imara, maana vijana wengi wanajitahidi kuanza na kujikusanya kupata mitaji lakini mwisho wa siku wakidondoka kuinuka inakuwa ni kazi
 
Back
Top Bottom