Kujipost mitandaoni Kila siku napo ni utumwa

Kujipost mitandaoni Kila siku napo ni utumwa

If it makes them happy, let them be. Humu duniani kila mtu ana kitu cha kustaajabisha anafanya, whether kwa uwazi au kwa kificho. Kwa akili za kawaida unashangaa, mtu anatikisa makalio akijirekodi na kutuma..ila ndio hivyo tena.

Kuna watu humu Internet ikikata kwa dk5 tu wanakuwa wehu, wanachanganyikiwa kabisa, huo nao si ukichaa!
 
Mi naonaga aibu nikiona mtu anajipost anaimba imba na anakosea hayo maneno sometimes, na ikiwa ndo mutu ya 30+ nahisi aibu kinyama sijui aibu ya nini wakati hainihusu...... Ila huwa nahisi aibu sana.
umeolewa
 
Kuna "EX" anaumizwa hapo...
Aisee hii ni maajabu. Ni mke wa mtu na ana watoto kabisa. Kila siku ni kuvaa nguo za kislayqueen za kubana tako halafu fupi mapaja yote njee,matiti njeee. Anaposti msambwanda wake status whatsapp, Instagram na mitandao yote......na Mume yupo, sijawahi kumuelewa
 
1. Kuwa mtumwa wa watu, bila kupata likes na comments unaona Bado siku haijaenda vzrii.
2. Kukosa Amani moyoni, siku ukiwa huna smart unahaha.
3.Mambo Yako kuwa hadharani hivyo hata wabaya wako rahisi kukupata na kukudhuru.
sema wewe unaweza ukaona flani anazidisha posts ila mimi nisione hivyo
 
Kuna watu hawezi kupitisha siku bila kujipost mtandaoni. Anajaza status weeee utasema analipwa na WhatsApp.
Hana siri kila kitu hadharani kwenye mitandao, yaani huna hata haja ya kupeleleza habari zake , ukizitaka tu unazipata mtandaoni.

Akiachwa, akiwa na huzuni, akiwa na furaha vyote ni kupost tu kwenye mitandao.

Amekuwa kama msanii Kila hatua ya maisha yake lazima watu waijue. Wasanii wanapata pesa angalau, sasa mwenzetu unapata nini!?, Zaidi ya like na comments ambazo hazina faida yoyote Ile katika maisha yako.

Huu ni utumwa vilevile. Kataa kuwa mtumwa wa mitandao.
Kwa wanawake ile ni njia ya kujiuza, kukumbusha wateja kuwa bado wapo, wasisahaulike.
Ukivutiwa unazama inbox mnayajenga chap
 
Kuna kashemu kangu ka kike kameolewa na kana mtoto mmoja wife kakapita kama miaka 15 hayo ndo mambo yake ameshaelekezwa sana lakini wapi
yaani hata kumpikia mtoto chakula waaap!
Katoto kenyewe hakajafika hata miaka
2 nikukashindilia masoda naskia.
 
Kujipost, Kuna post zingine za biashara huwezi kuacha kupost.
Yaani ukiwa beach unatupia vipicha, mara unaamka asubuhi " wadau ndo naamka" nani kakuuliza🤒
Kuna demu mmoja kipindi niko chuoni, akiamka asubuhi tu anaweka status inayosomeka "Good Morning World"
Nikajua huyu tayari chupa inapooza kwa kasi
 
Back
Top Bottom