Kujipost mitandaoni Kila siku napo ni utumwa

Kujipost mitandaoni Kila siku napo ni utumwa

Bora huyo wa kujipost.

Kuna mtu anajaza memez za video nyingiiiiiiii..

Ukiangalia kwa mbali unaweza dhania ni moja kumbe ziko buku.

Halafu baadaye anaanza kublock au kufuta namba za watu ambao hawaangalii status zake.

Mimi kiukweli, 'mute' option imejaa kwa viumbe kama hao. 🙂
 
Kuna watu hawezi kupitisha siku bila kujipost mtandaoni. Anajaza status weeee utasema analipwa na WhatsApp.
Hana siri kila kitu hadharani kwenye mitandao, yaani huna hata haja ya kupeleleza habari zake , ukizitaka tu unazipata mtandaoni.

Akiachwa, akiwa na huzuni, akiwa na furaha vyote ni kupost tu kwenye mitandao.

Amekuwa kama msanii Kila hatua ya maisha yake lazima watu waijue. Wasanii wanapata pesa angalau, sasa mwenzetu unapata nini!?, Zaidi ya like na comments ambazo hazina faida yoyote Ile katika maisha yako.

Huu ni utumwa vilevile. Kataa kuwa mtumwa wa mitandao.
Wengine wanasumbuliwa na ulimbukeni! Wengine wanajiuza! Wengine wanataka kuhurumiwa na kutaka kusaidiwa!
 
Back
Top Bottom