Kukata Mawasiliano na Familia: Miaka Haina Habari

Kukata Mawasiliano na Familia: Miaka Haina Habari

Gunner11

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2021
Posts
16,680
Reaction score
31,804
Imenishangaza kuona mtu anaondoka kwao, gafla anakata mawasiliano.

Inapita hata miaka bila wao kujua yuko wapi, anafanya Nini.

Ujasiri wa namna hii sio wa kawaida.

Ila pia inanifanya nifikiri kuhusu familia, malezi, tamaduni na utandawzi.

Kweli zama zimebadilika.
 
Sawa ila, hao unaowaacha inakuwa kama umewasaliti. Imagine mzazi kakulea mpk umekuwa alaf unakuja kusikia walisha mzika au wewe umepatwa shida. Mm naona bado inabidi kuwa nao hata kama from a distance
mpaka mtu anaamua kujitenga let say kwa kipindi cha miaka 20 bila kurudi home ujue kuna sababu tena nyingi


Familia zina mambo mengi sana
 
kujitenga esp kwa kijana anae jitafuta kuna faida nying na hasara nyingi kikubwa ni mtu kujitambua na kuelewa anatafuta nini,, ila kijana akijisahau Kidogo hivi hasa kwenye haya majiji au miji mikubwa ndo tunawapata wakina anko T wengi au kisura wa mbeya,,, bora hata mdada anaweza kuangukia Me akamuweka ndani na maisha yakasonga
 
Imenishangaza kuona mtu anaondoka kwao, gafla anakata mawasiliano.

Inapita hata miaka bila wao kujua yuko wapi, anafanya Nini.

Ujasiri wa namna hii sio wa kawaida.

Ila pia inanifanya nifikiri kuhusu familia, malezi, tamaduni na utandawzi.

Kweli zama zimebadilika.
Gentleman,
ikiwa unaendelea vizuri na maisha yako au na familia yako nadhani hakuna shida sana,

ingawa familia nyingi zenye uhasama miongoni mwa ndugu, ndio wana tabia hizo sana :BASED:
 
Sababu kubwa ni maumivu ya anaeondoka aliyo yapata, hapa ndipo linapokuja jambo kubwa linalohusu malezi na mahusiano ya watoto na wazaziwao.
Maumivu hufanya chochote kama alie umizwa hajaiona thamani yake.
downloadfile.png
 
Mimi mdogo wangu aliondoka siku lowasa anajiudhuru uwaziri mkuu. Juzi hata hajamaliza wiki ndio amemtafuta baba. Alichofanya alikariri namba ya baba kichwani hadi leo,. Ukweli tumesikia mengi.mara kawa jambazi amepigwa risasi kafa na mengine mengi
 
Mkuu mara nyingi ndugu wa kiafrika ni toxic sana hasa kwa mtu aliyesoma, Mategemeo ni makubwa kuliko uhalisia, personally faida za kujitenga kwangu ni nyingi zaidi kuliko kuwa karibu na ndugu wenye kejeli na mashindano yasio na msingi na kukulinganisha na wengine kusiko na maana.

Utulivu ni muhimu sana kwa anaejitafuta, utapata nafasi ya kujaribu na kukosea bila kelele na mtu.

Maisha ni yako personally mkuu, kama unajitambua na unajua unataka nini, na mafanikio yatakuwepo tu as long as you are genuine enough to your plans.

Tusipangiane maisha, ujamaa umetuharibu watanzania.
 
kujitenga esp kwa kijana anae jitafuta kuna faida nying na hasara nyingi kikubwa ni mtu kujitambua na kuelewa anatafuta nini,, ila kijana akijisahau Kidogo hivi hasa kwenye haya majiji au miji mikubwa ndo tunawapata wakina anko T wengi au kisura wa mbeya,,, bora hata mdada anaweza kuangukia Me akamuweka ndani na maisha yakasonga
Hakuna faida yoyote, si me Wala ke, ushajiuliza ukifa Kwa kishitukiza inakuwaje? Usha ona maiti za manispa zinavo zikwa?
 
Back
Top Bottom