Kukataa mimba, kutelekeza watoto na kuwanyima huduma au kutowahudumia — wanaume mnakwama wapi?

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Zamani ilikua ni furaha, heshma na sifa njema mwanaume kupata watoto, kuwalea kwa mahitaji na mafundisho bora lakini siku hizi mambo yamebadilika! Wanaume wengi wamekua na ka desturi kapya kabisaaa. Achana na kale ka kukataa mimba ambazo wanajua kabisa wao ni wahusika; Wanaume wengi wamekua wazito, wazembe na wakatili mno linapokuja swala la kuwahudumia watoto wao.

Kwa taratibu za kiimani na kidesturi mtoto ni wa mwanaume sio kwa ubini tuu; bali hata mfumo mzima wa kupata watoto mwanamke ni kama shamba zuri lenye rutuba na mwanaume ndio mkulima mwenye mbegu zake na yeye ndio anaamua akazipande kwenye shamba gani, azitunze ili apate matunda bora.

Leo nimekutana na kesi ya mwanaume mmoja hospitalini, mtu mzima kama baba kwangu anaumwa vibaya. Watoto zake na mke wake wameshakata tamaa ya kumuuguza sababu wameshatumia pesa nyingi sana na hawana tena uwezo. Ghafla wakaingia watu wawili mwanaume na mwanamke, wakamfuata kwenye kitanda na kuomba faragha waongee nae kwa muda, baada ya muda daktari akaitwa..... kumbe wale ni watoto wake aliwakimbia ila baada ya kupokea taarifa za kuugua kwa baba yao toka kwa mama yao ambaye anaishi hapa wamefanya mipango yote na sasa wamekuja kumchukua kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Yule baba amelia jamani, sijui kile kilio kilikua cha aibu? Cha majuto? Au cha uchungu maana kilikua kilio cha nguvu na kwikwi hadi watu wengine machozi yakawa yanawatoka.

Baba zetu, kaka zetu, watoto zetu tunzeni watoto wenu mnaozaa. Haijalishi ulimpata mtoto ukiwa katika hali gani ila kwa kuwa ni mtoto wako wajibika tuu kwa nafasi yako na Mungu atakubariki kwa nafasi yake.

Baba mchungaji Daniel Mugogo anakazia hapa

Mungu awabariki wanaume wote mnaotunza watoto zenu bila shurti

Mwanaume anayekimbia mtoto sio mwanaume kamili

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app

KWA karne hii wapo wengi tuu, Ukitizama vijana wengi Tunaingia kwenye mahusiano Bila kuchuja pros and cons za mahusiano ,Tunachotizama ni uhakika wa Uchi (Excuse my language) Hakuna chochote tunachokijua Mara paap Bila kutarajia ujauzito huu hapa .. Hali ambayo kijana hakujiandaa wala kuandaliwa ,Hali ya uchumi haieleweki solution inakuwa kukimbia au kukataa ujauzito/mtoto.

Swala hili lina hitaji utatuzi wa Hali ya juu .

Baba yangu alikufa kitambo Sana nikiwa na miaka minne ,life was good kipindi akiwepo , zimebaki kumbukumbu tuu za picha na stori kutoka KWA dada yangu , Ilibidi nijikuze mimi mwenyewe kwa kiasi Fulani, at my early 20s Niliteleza pahala , sikukataa ujauzito nimetake full responsibilities japo kuna changamoto zake Nazishinda na ninazidi kuwa strong kila siku.

Nimezungumza na vijana wengi waliooa wanasema hawajawahi pewa elimu yeyote kuhusu maandalizi ya ndoa ,malezi ya mtoto and so on..
Wengi Tunaingia vitabu KWA karne hii knowing nothing Tunaingia kupigwa za uso , inaumiza
 
Hakuna mwanaume ambaye ktk hali ya kawaida anapenda kutelekeza mtoto/watoto ila wanawake siku hizi wamekuwa pasua vichwa, kwa hiyo binafsi nimeona wanaume wengi wanatelekeza mama halafu mtoto anakuwa unintended victim!
 
Kusema wanawake siku hizi wamekua pasua kichwa halafu haohao wanaume wanazaa na pasua vichwa huoni kuna tatizo mahala?
Hivi unajua ni rahisi kumbaka mwanamke na kumpa mimba zaidi ya kumbaka mwanaume?
Anayeadhibiwa hapo ni nani? Ni pasua kichwa au yule mtoto wako asiyekua na hatia?

Wanaume tumieni tuu busara, kwenye hili la mtoto hamna EXCUSES
 
Na wanaume wanaolea watoto mpaka wanakuwa wakubwa halafu mama anawapa baba mwingine aliyehudumia anaambiwa sio wa kwake unawapa ushauri gani tatizo jamii imeamua kuwasikiliza wanawake na wanaume wengi ni watu wakukaa na vitu moyoni sio kuhadithia kila mtu ila kuna wanaume wamefanyiwa unyama kwenye suala la watoto kwa hyo mi nasema ngoma droo kazi iendelee.
 
Zamani ilikua ni furaha, heshma na sifa njema mwanaume kupata watoto, kuwalea kwa mahitaji na mafundisho bora lakini siku hizi mambo yamebadilika! Wanaume wengi wamekua na ka desturi kapya kabisaaa. Achana na kale ka kukataa mimba ambazo wanajua kabisa wao ni wahusika; Wanaume wengi wamekua wazito, wazembe na wakatili mno linapokuja swala la kuwahudumia watoto wao.

Kwa taratibu za kiimani na kidesturi mtoto ni wa mwanaume sio kwa ubini tuu; bali hata mfumo mzima wa kupata watoto mwanamke ni kama shamba zuri lenye rutuba na mwanaume ndio mkulima mwenye mbegu zake na yeye ndio anaamua akazipande kwenye shamba gani, azitunze ili apate matunda bora.

Leo nimekutana na kesi ya mwanaume mmoja hospitalini, mtu mzima kama baba kwangu anaumwa vibaya. Watoto zake na mke wake wameshakata tamaa ya kumuuguza sababu wameshatumia pesa nyingi sana na hawana tena uwezo. Ghafla wakaingia watu wawili mwanaume na mwanamke, wakamfuata kwenye kitanda na kuomba faragha waongee nae kwa muda, baada ya muda daktari akaitwa..... kumbe wale ni watoto wake aliwakimbia ila baada ya kupokea taarifa za kuugua kwa baba yao toka kwa mama yao ambaye anaishi hapa wamefanya mipango yote na sasa wamekuja kumchukua kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Yule baba amelia jamani, sijui kile kilio kilikua cha aibu? Cha majuto? Au cha uchungu maana kilikua kilio cha nguvu na kwikwi hadi watu wengine machozi yakawa yanawatoka.

Baba zetu, kaka zetu, watoto zetu tunzeni watoto wenu mnaozaa. Haijalishi ulimpata mtoto ukiwa katika hali gani ila kwa kuwa ni mtoto wako wajibika tuu kwa nafasi yako na Mungu atakubariki kwa nafasi yake.

Baba mchungaji Daniel Mugogo anakazia hapa

View attachment 2197930

Mungu awabariki wanaume wote mnaotunza watoto zenu bila shurti

ni wanaume wachache sana wanaotelekeza watoto ila ukweli tatzo kubwa lipo kwa akina mama. Wanawake mna maneno ya jeuri na kebehi linapokuja suala la kuhtalafiana hadi kutengana. Anaweza kukutukana matusi hadi ukajiuliza hawa watoto ni wa kwangu kweli. Halafu mna tabia ya kupandikiza maneno ya chuki ya kati ya mtoto na baba.
 
Hilo ni tatizo sana sana

Nimekaa vijiji vya kusini imekuwa kama kawaida yao lutohudumia lkn so shida kama ilivyo hapa Dar es

Watoto wengi na akina mama wengi wanachangamoto ya kutotunzwa na wanaume

Sasa nalea shule moja hapa Dar tena ya serikali ni shida tupu shida tupu sasa wanakumbana changamoto ya ulawiti toka kwa Baba zao hata maanko kisa kushindwa kulea watoto na mama yao.

It is very sad and painful indeed

Wanaume wajibikeni kisawasawa mmezaa wenyewe tekeleza wajibu hata Mungu tumuogope
 
sisi kwetu hatuachagi mtoto nyuma lakini kuna ukanda(siutaji) wao kuzaa na kuacha ni kawaida tuu.
 
The situation inakuwa mbovu mbaya pale unapogundua mpo wanaume wanne kwenye mimba moja!,hizi Hali zipo kweli tena Kuna njemba hapa mbili zimepewa mtoto halafu hawajui..😂
 
ni wanaume wachache sana wanaotelekeza watoto ila ukweli tatzo kubwa lipo kwa akina mama. Wanawake mna maneno ya jeuri na kebehi linapokuja suala la kuhtalafiana hadi kutengana. Anaweza kukutukana matusi hadi ukajiuliza hawa watoto ni wa kwangu kweli. Halafu mna tabia ya kupandikiza maneno ya chuki ya kati ya mtoto na baba.

Unaposema ni wanaume wachache wanaotelekeza watoto, chunguza hao wanaume wawatelekeza watoto wangapi? Na kwa wanawake wangapi?.
 
Hilo ni tatizo sana sana

Nimekaa vijiji vya kusini imekuwa kama kawaida yao lutohudumia lkn so shida kama ilivyo hapa Dar es

Watoto wengi na akina mama wengi wanachangamoto ya kutotunzwa na wanaume

Sasa nalea shule moja hapa Dar tena ya serikali ni shida tupu shida tupu sasa wanakumbana changamoto ya ulawiti toka kwa Baba zao hata maanko kisa kushindwa kulea watoto na mama yao.

It is very sad and painful indeed

Wanaume wajibikeni kisawasawa mmezaa wenyewe tekeleza wajibu hata Mungu tumuogope

Wanaume wanaume tunzeni watoto wenu
 
Sometimes wazazi wa binti husika huachangia mwanaume kutelekeza mtoto. Hasa ikitokea binti kapewa mimba bado anaishi kwao au ni mwanafunzi. Mtu unaomba mlizungumzie kifamilia wewe baba unataka kufunga jela mtia mimba mwisho jamaa anaamua kula kona mpaka soo iishe.

Btw siungi mkono kutelekeza uzazi wako uliousababisha. As a real Men we have to face and Embrace the consequences of our doings.
 
The situation inakuwa mbovu mbaya pale unapogundua mpo wanaume wanne kwenye mimba moja!,hizi Hali zipo kweli tena Kuna njemba hapa mbili zimepewa mtoto halafu hawajui..😂

Mwanamke mmoja wanaume wanne ni chaguo la mwanaume.
Ndio mjue kutulia njia kuu maana wale mnaopita nao, na wao wanapita na wengine
 
Kusema wanawake siku hizi wamekua pasua kichwa halafu haohao wanaume wanazaa na pasua vichwa huoni kuna tatizo mahala?
Hivi unajua ni rahisi kumbaka mwanamke na kumpa mimba zaidi ya kumbaka mwanaume?
Anayeadhibiwa hapo ni nani? Ni pasua kichwa au yule mtoto wako asiyekua na hatia?

Wanaume tumieni tuu busara, kwenye hili la mtoto hamna EXCUSES
Wote pasua bichwa tuu....🤣🤣🤣🤣
 
Sometimes wazazi wa binti husika huachangia mwanaume kutelekeza mtoto. Hasa ikitokea binti kapewa mimba bado anaishi kwao au ni mwanafunzi. Mtu unaomba mlizungumzie kifamilia wewe baba unataka kufunga jela mtia mimba mwisho jamaa anaamua kula kona mpaka soo iishe.

Btw siungi mkono kutelekeza uzazi wako uliousababisha. As a real Men we have to face and Embrace the consequences of our doings.

Ni kweli lakini wa kundi hili ni wachache sana
 
Mwanamke mmoja wanaume wanne ni chaguo la mwanaume.
Ndio mjue kutulia njia kuu maana wale mnaopita nao, na wao wanapita na wengine
Viumbe hivi vinapenda kupeana lawama lakini cha ajambu wanagegedana. Sasa sii tuamie moja tuu kuwa tugegedana na sio kulaumiana. Hamna wako peke yako jamani
 
Wanawake bana nchi tuwape bado ajira iwe 50/50 na bado tuwahudumie nyie na watoto. Hela zenu huwa mnapeleka wapi au ndio kule mnapopanua miguu muoshwe miguu na kupakwa kucha rangi!
 
Unaposema ni wanaume wachache wanaotelekeza watoto, chunguza hao wanaume wawatelekeza watoto wangapi? Na kwa wanawake wangapi?.

Mazingra ninayofanyia kazi hili swala huwa nakutana nalo sana wanawake wengi wanakuja na madai ya kutohudumiwa watoto lakini anapoitwa mwanaume mambo yanakuwa tofauti. Wanaume wengi wanaptia magum mengi kutoka kwa wenza wao lakini wanakaa kimya. Ushauri kwa wanaume wenzangu ukigombana na mke chukua wanao au weka mazingira ya kuwahudumia maana wengne wanatoa huduma kwa ajili ya watoto lakini zile huduma haziwafikii walengwa.
 
Back
Top Bottom