Zamani ilikua ni furaha, heshma na sifa njema mwanaume kupata watoto, kuwalea kwa mahitaji na mafundisho bora lakini siku hizi mambo yamebadilika! Wanaume wengi wamekua na ka desturi kapya kabisaaa. Achana na kale ka kukataa mimba ambazo wanajua kabisa wao ni wahusika; Wanaume wengi wamekua wazito, wazembe na wakatili mno linapokuja swala la kuwahudumia watoto wao.
Kwa taratibu za kiimani na kidesturi mtoto ni wa mwanaume sio kwa ubini tuu; bali hata mfumo mzima wa kupata watoto mwanamke ni kama shamba zuri lenye rutuba na mwanaume ndio mkulima mwenye mbegu zake na yeye ndio anaamua akazipande kwenye shamba gani, azitunze ili apate matunda bora.
Leo nimekutana na kesi ya mwanaume mmoja hospitalini, mtu mzima kama baba kwangu anaumwa vibaya. Watoto zake na mke wake wameshakata tamaa ya kumuuguza sababu wameshatumia pesa nyingi sana na hawana tena uwezo. Ghafla wakaingia watu wawili mwanaume na mwanamke, wakamfuata kwenye kitanda na kuomba faragha waongee nae kwa muda, baada ya muda daktari akaitwa..... kumbe wale ni watoto wake aliwakimbia ila baada ya kupokea taarifa za kuugua kwa baba yao toka kwa mama yao ambaye anaishi hapa wamefanya mipango yote na sasa wamekuja kumchukua kwenda kutibiwa nje ya nchi.
Yule baba amelia jamani, sijui kile kilio kilikua cha aibu? Cha majuto? Au cha uchungu maana kilikua kilio cha nguvu na kwikwi hadi watu wengine machozi yakawa yanawatoka.
Baba zetu, kaka zetu, watoto zetu tunzeni watoto wenu mnaozaa. Haijalishi ulimpata mtoto ukiwa katika hali gani ila kwa kuwa ni mtoto wako wajibika tuu kwa nafasi yako na Mungu atakubariki kwa nafasi yake.
Baba mchungaji Daniel Mugogo anakazia hapa
View attachment 2197930
Mungu awabariki wanaume wote mnaotunza watoto zenu bila shurti