Mwanaume anayekimbia mtoto sio mwanaume kamili
Sent from my TECNO KA7 using
JamiiForums mobile app
Kati ya mimba na watoto walotelekezwa, Tunaweza kupata idadi ya mimba zilizokatakiwa na watoto kutelekezwa sababu mamama zao walitembea na wanaume wengi?
Ngoja niwape scenario then mseme "Ubaya wa wanaume uko wapi?""
Nina mabinti wawili mmoja naishi nae na mwengine yupo kwa mama ake.
1. Mtoto wa kwanza
Nilikutana na mama ake mjni Daslamu..!!
Kwenye harakati zangu za kutafuta maisha.
Mapenzi yakanoga binti akapata mimba.
Katikati ya mimba nikagundua Mimi, bosi wake wa kazini, na Mchungaji wake wotee tunamla.
Tena hata akiwa na mimba tulikuwa tuna mla.
Nilivyo pekua zaidi nikagundua mimba yake alinipa Mimi kwasababu ndio nilikuwa single.
Nilikata huduma fasta na nikahama.
Hakujua nilikohamia.
Maisha yalienda mtoto akazaliwa.
Yule dada alimtafuta dada angu na kumtumia picha ya mtoto, aisee alikuwa anafanana na Mimi copy right...!!!
Shangazi zangu wakapata habari na ukweli wa story.
Wakaomba watumiwe michoro ya mikono, walivyoizoom michoro ya mikono kwenye kiganja cha mtoto wakasema "Hii damu yetu" + na hii sura mlivyofanana HUNA HAJA YA KUPIMA DNA.
Ilibidi nimkubali na nianze kumtunza mtoto kwa makubaliano akifika miaka 5 namchukua.
Mtoto akiwa na miaka 3 mama ake aliolewa akaniachia na yeye kaenda kuanza maisha na mumewe.
WHAT IF TUSINGEFANANA UNADHANI NINGEMKUBALI?
NISINGETOA HATA 10 YA MALEZI, WANGELEA BOSI NA MCHUNGAJI.
2. Mtoto wa pili.
Nilikutana na mama ake na mapenzi yakaanza.
Kuna siku alikuja kwangu ijumaa tukafanya, akasepa na kurudi juma3.
Juma3 alivyokuja alikuwa amechokaa na Kazi akaomba alale tuu siku nzima.
Katikati ya kulala nikaona sms nyingii zinaingia.
Ile kuangalia simu yake nikagundua ijuma alilala na Mimi, jumamosi na mjamaa mwengine, na jumapili na mwengine na Mimi karudi Tena juma3.
Kwenye sms za kawaida ilionyesha tupo wanaume wa 3 tuna muhudumia.
Ila kiuhalisia sikujua exactly figure TUPO WANGAPI.
Hawa wawili ni vile nilikutana na ushahidi kwenye simu.
Aliamka, ile kumuuliza ni ugomvi then akaondoka kwa hasira.
Ikapita wiki kadhaa bila kuwasiliana na Mimi, akanijuza "Nina mimba"
Hata siku jibu nilikata simu na kukaa kimyaa na kumblock.
Mtoto akazaliwa.
Akawa anasisitizaa hii mimba ni yangu, swala likaenda ustawi, yeye na dada ake wakakomaa "mtoto wangu", huku Mimi NABISHAAA na kuelezea niliyoyakuta kwenye simu yake.
Ustawi ukatoa solution "tupime DNA".
DNA ikapimwa na majibu yakatoka "Mtoto ni wangu"
Kwasasa namlea. Na mtoto anakuja sanaa kwangu siku za likizo.
Akija anaishi na mwenzake maana wotee ni watoto wangu.
Huyu nae namtaka kutoka kwa mama ake japo mama ake amekuwa mbishi.
JIULIZE.
Kwenye kesi kama hizi "Kuna ubaya wa mwanaume kukataa mimba?"
Hivi kama ningekuwa sina uwezo wa kilipia DNA unadhani NINGEMKUBALI mtoto?
Hakuna mwanaume anayemkataa mtoto BILA SABABU ila Kuna SABABU ZINAFANYA TUWAKATAE HAO WATOTO.
Tunakulala wanaume zaidi ya mmoja, KWANINI MIMBA IWE YANGU NA ISIWE YA HAO WENGINE?
#YNWA