Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Kwema Wakuu,
Najua hili litawafikia sababu JF ni Platform kubwa. Nyinyi Azam TV ndio mmepewa haki ya kuonyesha Mpira wa Ligi yetu pendwa ya NBC Premier League. Sisi Subscribers wenu tuna haki ya kupata Matangazo hayo katika ubora wa hali ya juu bila ukakasi. Yaani Sisi kwa kununua ving'amuzi vyenu automatically tunakua tumeingia makubaliano (implied contract ) kua mtatuonyesha mpira katika ubora wake.
Goli lililofungwa baada ya Kona ya Shomari Kapombe lilikataliwa kwa madai kua Mpira huo ulizungukia kwanza nje (curve) kabla kisha ukarudi ndani. Mpaka mpira unaisha Azam wameshindwa kuonyesha hiyo "Curve". Hata Watangazaji wenyewe wamebaki na kigugumizi maana hakuna Video kuthibitisha mpira uli curve nje ya mstari.
Solution hapa ilikua ni kuwepo kamera kwenye kila kona (kibendera) lakini kwa ubahili wa Azam wameshindwa kuweka. Ina maana Simba jana wangeweza kusema Refa aliwahujumu kumbe maamuzi ya Refa yalikua sahihi.
Au tuseme ingekua ndio Coastal Union wamefunga lile goli likakataliwa ingeweza kudhaniwa Simba anabebwa. Hii yote ni sababu Azam wameshindwa kuweka Kamera za kutosha Uwanjani.
Nawaza ni kiasi gani tunalipia ving'amuzi ambavyo kila kukicha vinapanda bei, na Kamera ni kiasi gani kwa kampuni kama Azam kushindwa kuweka kila pembe ya uwanja. Hii si sawa, na ni unyonyaji mkubwa tunafanyiwa.