Kukatika umeme Uwanja wa Mkapa: Serikali yawasimamisha watendaji kadhaa; yaomba radhi
Kwa Hali hii ya kukatika katika kwa umeme maeneo muhimu, Hiyo Treni ya Umeme ije na Power Bank
 
Nadhani umeninukuu vibaya,sikuwa na nia ya kusema football ni mchezo wa kijinga,I meant mambo ambayo ni basic needs za mtanzania kama ,maji,umeme,dawa....
Nimekupata ila michezo ni sekta muhimu sana ya uchumi hasa ukiangalia mapato, ajira na mambo mengine inayochangia katika uchumi na jamii kwa hiyo bado nadhani unaweza kuwa unakosea kuishusha hadhi yake kihivyo. Tungeacha janjajanja katika sanaa na michezo, sekta hizo zingeweza kuchangia zaidi huko tunakoona ndiyo kwa muhimu zaidi. Mafanikio ya Simba na Yanga msimu huu tu yameleta fedha za kigeni zaidi ya dola milioni 1.

Binafsi naamini haya matatizo ya umeme ni ya maksudi maana nimeongelea uwezekano wa kutokea hujuma katika mpira wetu muda mrefu kidogo.
 
Katibu mkuu wa Wizara ya Michezo amemtua Milinde Mahona kuwa kaimu meneja wa Uwanja wa Mkapa kuanzia leo

Uteuzi huo unafuatia Waziri Pindi Chana kuwasimamisha Kazi Watumishi 7 wa Uwanja wa Mkapa

Source: Ayo tv
 
Katibu mkuu wa Wizara ya Michezo amemtua Milinde Mahona kuwa kaimu meneja wa Uwanja wa Mkapa kuanzia leo

Uteuzi huo unafuatia Waziri Pindi Chana kuwasimamisha Kazi Watumishi 7 wa Uwanja wa Mkapa

Source: Ayo tv
Si mashahara bado unaingia
 
.... reactive than proactive! Hatufiki popote.
 
Wamesimamishwa KAZI na hawajafukuzwa KAZI.kuna watu wengi Tu huwa wanasimamishwa KAZI serikalini.unaenda unasoma magazeti mshahara unasoma.mpaka utakapopangiwa KAZI nyingine ama ufukuzwe kazi ikithibitika ulikiuka maadili ya utumishi WA umma
Ukisimamishwa Kazi huendi kazini ila mshahara unalipwa
 
Wamewasimamisha watendaji au wanyakyusa? [emoji1787]Naona majina hayo hata sielewi! [emoji23][emoji23]
 
331F4F91-0FE2-428D-B294-89727B16BF2D.png

Muktasari:

  • Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Pindi Chana amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumsimamisha kazi Kaimu meneja wa uwanja huo, Said Mtumbuka na wafanyakazi wengine sita kutokana na kukatika kwa umeme katika uwanja huo katika mechi ya kombe la shirikisho Afrika

Dar es Salaam. Kufuatia kukatika umeme uwanja wa Benjamin Mkapa jana usiku Jumapili Aprili 30, 2023 wakati wa mechi ya robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika, Kati ya Yanga na Rivers United kutokea Nigeria, Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo imemsimamisha kazi Kaimu meneja wa uwanja huo, Said Mtumbuka na wafanyakazi wengine sita.

Taarifa iliyotolewa jana Aprili 30 na wizara hiyo, imesema Waziri Dk Pindi Chana amemwagiza katibu Mkuu wa wizara hiyo hiyo, Said Yakubu kuwasimamisha watumishi hao wakiwamo pia aliyekuwa Mhandisi wa Umeme, Manyori Kapesa na aliyekuwa Afisa Tawala wa Uwanja huo, Tuswege Nikupala.

Aidha, rungu hilo pia limewapitia wafanyakazi wengine wa uwanja huo akiwemo, Gordon Mwangamilo, Gabriel Mwasele, Yanuaria Imboru na Dk Christina Luambano.

Taarifa hiyo pia imesema Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Said Yakubu amemteua Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa uwanja huo kuanzia Mei 1, 2023.

Pia, Katibu Mkuu atawasiliana na wadau wote kuwa mechi zote zitakazochezwa uwanjani hapo zipangiwe jioni na sio usiku katika kipindi hiki ambacho maboresho ya mfumo wa umeme na taa unaendelea.

Kwa upande wao Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kupitia taarifa yake rasmi iliyotolewa na kurugenzi yao ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma imesema haihusiki na kukatika kwa umeme katika uwanja huo.

“Tanesco inawataarifu kuwa uwanja wa Taifa unahudumiwa na vyanzo viwili vya umeme, Tanesco na majenerata ya uwanja huo. Katika mechi ya leo (Yanga na Rivers United) uwanja ulikuwa unahudumiwa na majenereta,”.

Pia, wamesema baada ya majenereta kushindwa kufanya kazi katikati ya mchezo ndipo walitumia umeme wa Tanesco na mechi ikaendelea

SPECIAL CREDITS:
1BF7A18A-3FFB-485F-9C7F-D03866364097.jpeg
 
Hao wafanyakazi wangekua na ndugu waziri wangeundiwa tume ya uchunhuzi kwanza Kisha kesi ingejifia.
Wizara inaomba radhi mashabiki wa soka nchini hususan wa timu ya Yanga kwa kadhia iliyojitokeza.

Wizara Inawaahidi Watanzania wote kwamba Itaendeea kufanya ukarabati mdogo na mkubwa ili Uwanja wa Benjamin Mkapa uendelee kutoa huduma na burudani stahiki kwa Watanzania pamoja na nchi jirani zinazotumia uwanja huo.
20405809-0B0B-477A-9707-35A72DE5303C.png
 
Back
Top Bottom