Kukiri kwa Sabaya Kumeaibisha CCM, Awamu ya 5 na Yeye Mwenyewe

Kukiri kwa Sabaya Kumeaibisha CCM, Awamu ya 5 na Yeye Mwenyewe

🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Wewe hujui Siasa uko Chadema kikanda tu

Mbowe aliombewa msamaha na Zitto Kabwe kupitia Kikosi Kazi cha Prof Mkandala na ndivyo sababu Zitto alitamba kwamba Yeye ndio mtu wa kwanza kujua kwamba Mbowe anaachiliwa kwa Masharti na DPP siku ile

Mbowe ni mkristo hakutaka Kuwa kama wale Wakoma 9 akaamua kwenda Ikulu direct Kumshukuru Rais

Mungu akubariki!
Ili uwe mwanasiasa ni lazima uwe na sifa zifuatazo zote ama 2/3 ya hizo sifa;

1 MNAFIKI,una ujua ukweli lkn unajitoa ufahamu (rejea ndiyo mzee).

2 MKATILI (rejea ya KOLIMBA,LISSU,Mengine ongezea)

3 MCHAWI NA MSHIRIKINA ( Rejea ule unga na koti kuning'inia BUNGENI,NDUGAI NA FIMBO YAKE PALE KONGWA).

ZITTO ndiyo alimuombea huyo aliyekuwa akitajwa kuwa ni gaidi ambaye hakukutwa hata na kichongeo cha kalamu ya risasi,lkn ni kwa7bu ZITTO anaamini huo upepo utamuweka mahala pazuri wakati wa siasa za majukwaani.
Lkn pia ile kesi ya maigizo ya KAOLE GROUP ili ivua nguo serikali yangu,nilitamani upande wa serikali uweke mpira kwapani mapema tu walipoanza kutoa ushahidi wale wauza mbege kwani ilikuwa wazi na dhahiri kwamba hiyo ni KESI YA MCHONGO,MAJAJI WA MCHONGO NA MASHAHIDI WA MCHONGO.

Sito shangaa 7YA AKITUNUKIWA TUZO KM ALIVYO TUNUKIWA RAMADHAN KINGAI.

Hii ndiyo Tz ninayo ifahamu mimi.

Mimi ni MSAFI hivyo SIPENDI SIASA kwakuwa ni MCHEZO MCHAFU.
 
Mbowe alikutwa na kesi ya kujibu kwamba yeye ni gaidi muuwaji
Watanzania wengi hawana uelewa kabisa na masuala ya sheria.

Case to answer maana yake ndo kesi inaanza kusikilizwa baada ya upande wa mashitaka kukamilisha ushahidi wao na mahakama kuona ushahidi una uzito wa kuendelea na kesi.

Lakini haina maana kwamba kukutwa na kesi ya kujibu maana yake umepatikana na hatia.

Unakutwa na kesi ya kujibu na bado unaachiwa huru baada ya kushinda kesi kutokana na ushahidi wako utakaoitoa.

Mbowe hana hatia hadi kufikia sasa tofauti na ndugu Sabaya mwenye hatia iliyopo kwenye kumbukumbu za mahakama.
 
Samehe 7×70
Ngumbaru km wewe huwezi kuelewa hiyo kauli.
Sabaya kakiri ni kwamba kakoma adhabu aliyopata.
Sasa kasamehewa wewe mungu unasema tutamtafuta uraiani?
Acha upumbavu wewe.
Nae ana wazazi familia watoto wanamtegemea.
Mijitu yenye roho mbaya km nyinyi walahi hamtakiwi kupumua
 
Kutoka kusema Sabaya ataozea jela hadi ameotia awamu ya 5 aibu?
Ameomba poo mbele ya mahakama unadhani kiubinadamu mahakama ingefanyaje maana ipo sheria ya plea bargain inaipa nguvu mahakama kumwachia mshtakiwa kwa masharti baada ya kutimiza masharti.
 
Sabaya amekiri mashitaka mawili peke yake,nayo ni
:
"Imeelezwa kuwa Lengai Ole Sabaya na wenzake, Januari 19, 2021 katika eneo la Masama Mbosho wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, bila kibali walivamia duka la Alex Evarest SwaI na kuchukua mali na kuzizuia na kujipatia kaisi cha fedha shilingi milioni 50.

Kosa la pili ni kuzuia upatikanaji wa haki ambapo Januari 19, 2021 katika maeneo tofautitofauti katika Wilaya ya Hai na Tulia jijini Arusha na maeneo tofauti ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama za kumfanya Alex Swai kuwa ametenda kosa la kukwepa kodi."

Yale mashitaka saba mliyoyapanga na Mkwe wenu DPP Kweka,yote ameyashinda kwenye ile rufaa yake.

Haya ni mashitaka yaliyogeuzwa kuwa plea bargain,kwa sabavu sio uongo kwamba yule Swai hakuwa mkwepa kodi pale Bomangombe.
Kwa maelezo hayo alitenda ujambazi.

Pia ikimbukwe kwamba aliomba afutiwe mashtaka ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha na uapnde wa serikali ukakubali ombi lake ndo maana akabakiwa na makosa hayo ambayo amekiri kuyatenda.

Sasa kama mtu amevamia duka la mtu akapora mali halafu ni kiongozi wa serikali huoni mleta mada yupo sahihi kusema ameitia aibu serikali iliyomteua pamoja na chama chake?

Inaonekana viongozi wa kariba yake wapo wengi hadi leo ila angalau wao wanatenda uhalifu kwa kificho tofauti na yeye alitenda ujambazi hadharani.
 
Ameomba poo mbele ya mahakama unadhani kiubinadamu mahakama ingefanyaje maana ipo sheria ya plea bargain inaipa nguvu mahakama kumwachia mshtakiwa kwa masharti baada ya kutimiza masharti.
Mbona wezi wa kuku hawatoki kwa plea bagain?

Hiyo ipo kwa ajili ya wanasiasa katika kuramba asali ili kuwahadaa wapumbavu wa nchi hii!
 
Mbona wezi wa kuku hawatoki kwa plea bagain?

Hiyo ipo kwa ajili ya wanasiasa katika kuramba asali ili kuwahadaa wapumbavu wa nchi hii!
Huyo mwizi wa kuku kwani ana akili ya kujua kwamba kuna njia nyingine ya kuchomoka kupitia plea bargain?

Yeye hana wakili anasimama mwenyewe kwahiyo obviously lazima alambwe mvua.

Sasa wanasiasa na watu wenye uwezo wa kuweka mawakili wasomi wanajua njia mbalimbali za kuchomoka kwenye kesi.
 
Huyo mwizi wa kuku kwani ana akili ya kujua kwamba kuna njia nyingine ya kuchomoka kupitia plea bargain?

Yeye hana wakili anasimama mwenyewe kwahiyo obviously lazima alambwe mvua.

Sasa wanasiasa na watu wenye uwezo wa kuweka mawakili wasomi wanajua njia mbalimbali za kuchomoka kwenye kesi.
Kwamba wezi wa kuku wote na wenye makosa ya aina hiyo wote nchi hii hawana akili za kuweka mawakili?
 
Kwamba wezi wa kuku wote na wenye makosa ya aina hiyo wote nchi hii hawana akili za kuweka mawakili?
Kwamba uibe kuku wa buku 10 uweke wakili kwa milioni kadhaa?

Mtu hadi anafikia hatua ya kuiba kuku huyu ni fukara wa kutupwa.

Wenye uwezo wa kuweka mawakili ni wesi na majambazi wakubwa sampuli ya kina Sabaya.

Sabaya aliweka mawakili watatu tena maarufu sasa huoni ni mwizi mkubwa.
 
Back
Top Bottom