MBONA MKALI HIVYO,NADHANI NIMEJARIBU KUTENGEZA INITIAL CLUE TORWADS A SOLUTION,KUFUATANA NA JINSI SWALI LILIVYOULIZWA.WEWE UMESOMA BWANA,..NADHANI SIKU ZOTE HUWA UNAJIBU ULICHOULIZWA.
SABABU KWA UJUMLA
1.Physiologica;inaweza kuwa kawaida kama hakuambatani na maradhi au pindi hamna malalamiko toka kwa wenzi unao ishi nao,kama wenzio wana malalamiko ambayo yatageuka kuwa kero kwako binafsi,basi tayari huo ni ugonjwa na una matibabu yake.
2. Pathological process; mara nyingi ni matokeo ya ugonjwa/magonjwa ambayo hupelekea tendo la kukoroma,nayo hutofautiana kufuatana na umri.Hata watu wazima kuna wengine utakuta walikuwa hawana historia ya kukoroma,lakini GHAFLA ukubwani wanakumbwa na ugonjwa huo.[mfano ni baadhi ya wagonjwa wa ukimwi,ingawa sio wote,na sio lazima kuwa kila mwenye hali hiyo basi awe ni mgonjwa wa ukimwi lakini huonekana kwa (some HIV and someof the CANCER PATIENTS)]
3.Congenital;Huanza kuonekana pale tu baada ya kuzaliwa,kisababisho kinaweza kuwa ni URITHI[ hereditary]kutoka kwa waliomtangulia au kama sio urithi basi ni tokeo la hitilafu za kimuundo
zilizotokea kipindi cha uumbaji wa mtoto, wakati akiwa bado yupo tumboni mwa mama yake [fetal development]
4 Drug induced;Husababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa,ambazo mbali na kutibu ugonjwa hutowa matokeo ambayo hayakutarajiwa medically known as adverse drug reactions [An unwanted effect caused by the administration of a drug] Hali hii huweza kutokea ghafla au taratibu.
5 Traumatic or corrosive injury;Ikitokea kwenye larynx au trachea huweza pia kusababisha.Unywaji wa sumu pindi watu wanapotaka kujiua ,sumu wavutayo wafanyakazi kwenye baadhi ya viwanda n.k. ambayo ina uwezo wa kusababisha kusinyaa kwa larynx au trachea[capable of causing their stenosis or narrowing]
6. Post thyroidectomy ;Hutokea baada ya kufanyiwa opration ya kuondoaTezi THYROID.Sababu moja wapo ni kuumizwa,au kukatwa kwa recurrent laryngeal nerve wakati wa kuiodoa hiyo tezi[thyroid]
SABABU ZIPO NYINGI MNO NA NDIO MAANA NIKAANZIA NA SUALA LA UMRI KWANZA,..ILI TUWEZE KUTOA USHAURI WA WAPI PA KUANZIA..KAMA NITAZUNGUMZIA YOYE HAYO juu ,NA KUTOA USHAURI WA TIBA NADHANI NITAKUA SIJAJIBU SWALI,NA WALA SITAELEWEKA.