LadyRed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 9,636
- 11,483
Yummyyy👏🏽👏🏽👏🏽Pilau caribbean style
Mahitaji
* 1 kg ya nyama ya kuku iliyosafishwa na kulowekwa (marinated) kwa viungo kwa saa moja
* 1 kikombe 1 cha njegere
* 1 kikombe 1 cha tui la nazi
* Vikombe 2 vya brown rice au basmati au mchele wa kawaida uliosafishwa vizuri
* Vikombe 3 vya maji au chicken broth
* 2 tbsp sukari ya brown
* 2 tbsp mafuta ya kupikia
* Karoti 1
* 1 vitunguu maji,swaumu,tangawizi
* Nyanya 1-2 zilizokatwa
* 1 tbsp mdalasini,binzari nyembamba (ikiwa inahitajika)
* Pilipili 2-3 za kunukia zilizokatwa au nzima
* Chumvi
View attachment 1162360
Mahitaji ya ku marinated kuku
* coriander safi (giligiliani), (iliyokatwa ndogo ndogo)
* majani ya parsley , (iliyokatwa ndogo ndogo, majani tu)
* Vitunguu 6 hadi 8 vitunguu, (peeled ,kukatwa ndogo ndogo)
* 1 tsp chumvi
* 1 tbsp ya binzari nyembamba (ground cumin)
* paste ya swaumu na tangawizi
View attachment 1162364
1.washa jiko moto wa chini ,Weka mafuta kwenye sufuria kubwa (napenda kutumia sufuria ya chuma) na ongeza sukari ya brown kwenye mafuta na koroga hadi iwe nzuri na giza (kama unatengeneza shira ya kashata vile ) ikipanda na kutoa povu (bubbling) ni tayari
2.kuwa makini isiungue ,itasababisha chakula kuwa kichungu
3. mafuta na sukari vikiwa tayari,weka nyama yako kwa uangalifu kwa sababu iyo caramel (shira) itaruka na kukuchoma vibaya sana (ninatumia mfuniko kama ngao yangu) koroga nyama na ufunike vizuri na wacha ichemke kwa takriban dakika 10 na koroga kila baada dakika chache. Kuelekea mwisho wa dakika kumi ikiwa nyama sio brown kama unavyotaka ongeza mdalasini wa unga na binzari nyembamba ya unga
4. Sasa ongeza moto kwa dakika chake koroga mpaka nyama ikauke vizuri isiwe na mchuzi chuzi
5.ongeza veggies zako (vitunguu, swaumu,Tangawizi,karoti na nyanya,hoho napenda pia kuongeza tsp ya fresh grean seasoning kijani kwa ladha ya ziada),koroga bila mwiko (sauté) kwa dakika chache, kisha ongeza mchele wako na njegere na koroga kila kitu vizuri ili mchele uchukue ladha zote sawasawa
6. Ongeza supu yako ya kuku au maji ,tui la nazi ,chumvi na pilipili nzima ,koroga (stir)
7. funika punguza moto chini kabisa, na wacha kwa dakika 30 (Ukiamua kumaliza kwenye oveni hakikisha unawasha Kabla kwa digrii 350,utapika katika oveni kwa muda sawa wa dakika 30)
8. Mara baada ya kuiva unaweza ku serve na salads, au kipande cha avocado na sauce ya pilipili
9. tahadhari wakati wa kuwekapilipili nzima inaweza kupasuka,kwa hivyo use at your own risk. Lakini wakati mwingine huwa naweka tu kipande wakati ninapoongeza vitunguu kwenye sufuria.kama una watoto ni vizuri kuongeza tu sauce ya pilipili baadaye kwenye sahani kwa wanao tumia .
View attachment 1162377
farkhina LadyRed
Japo the sukari part lol