Kuku wa kuoka pamoja na mboga mboga

Kuku wa kuoka pamoja na mboga mboga

*****Mahitaji*****

1)Kuku 1
2)kitunguu maji 1 kikubwa
3)Pilipili boga (hoho) 1
4)Kitunguu saumu na tangawizi 1tsp
5)mbatata 5 (viazi) ndogo
6)Spices upendazo
7)nyanya zilosagwa 4-5
8)giligilani
9)chicken broth mix(sio lazima)
10)ndimu 1
11)chumvi.
12)bilinganya 3 ndogo

*****Namna ya kuandaa*****

1)katakata vegetable zote weka pembeni.
2)Weka kuku chumvi na spices unazopendelea.
3)weka kuku kwenye tray juu yake weka vegetables na katia giligilani kwa juu.
4)Mimina nyanya ulosaga
5)unaweza kuongezea chumvi kwa juu na pilipili manga (mtama).
6)Funika foil na bake kwa lisaa limoja au hadi iwe imewiva.


Maasalam [emoji8].View attachment 1160628



View attachment 1160632View attachment 1160634
usipende Kula Kula.
 
*****Mahitaji*****

1)Kuku 1
2)kitunguu maji 1 kikubwa
3)Pilipili boga (hoho) 1
4)Kitunguu saumu na tangawizi 1tsp
5)mbatata 5 (viazi) ndogo
6)Spices upendazo
7)nyanya zilosagwa 4-5
8)giligilani
9)chicken broth mix(sio lazima)
10)ndimu 1
11)chumvi.
12)bilinganya 3 ndogo

*****Namna ya kuandaa*****

1)katakata vegetable zote weka pembeni.
2)Weka kuku chumvi na spices unazopendelea.
3)weka kuku kwenye tray juu yake weka vegetables na katia giligilani kwa juu.
4)Mimina nyanya ulosaga
5)unaweza kuongezea chumvi kwa juu na pilipili manga (mtama).
6)Funika foil na bake kwa lisaa limoja au hadi iwe imewiva.


Maasalam [emoji8].View attachment 1160628



View attachment 1160632View attachment 1160634
Nafungua huu uzi af simu naiacha mezani kwa makusudi, ili mama watoto ajiongeze[emoji16][emoji16]
 
Hapana coconut cream/milk,unachemshaje sasa
Navofanya mimi kwny mashed potatoes
Nachemsha viazi and salt kdogo sufuria 1
Na milk and butter sufuria ingine
Mda wa kumash ndo nachanganya and serve straight

Ss sijajua coconut milk uchemshe na viazi kabisa au separate
 
Navofanya mimi kwny mashed potatoes
Nachemsha viazi and salt kdogo sufuria 1
Na milk and butter sufuria ingine
Mda wa kumash ndo nachanganya and serve straight

Ss sijajua coconut milk uchemshe na viazi kabisa au separate

I guess coconut ukiipika itaondoa ule u creamy na ladha yake.

cadey wewe si unamix mwisho pamoja na ingredients nyengine?
 
I guess coconut ukiipika itaondoa ule u creamy na ladha yake.

cadey wewe si unamix mwisho pamoja na ingredients nyengine?
Ndiyo mimi namix mwishoni nikimaliza kuponda,wakati naanza kuponda ndo naweka butter na ingredients nyingine nikimaliza naweka iyo coconut cream namix basi inakuwa tayari,kama ni coconut milk kwa sababu ni nyepesi huwa nikimaliza kuponda narudisha jikoni moto wa chini namix nakoroga mpaka nipate uzito ninao hitaji then na serve LadyRed
 
farkhina 😆😆 ilikuwa for breakfast served with chapati
6B4B11DC-E077-4B1F-99F7-5A0C623C31AC.jpeg
 
Pilau caribbean style



Mahitaji

* 1 kg ya nyama ya kuku iliyosafishwa na kulowekwa (marinated) kwa viungo kwa saa moja

* 1 kikombe 1 cha njegere

* 1 kikombe 1 cha tui la nazi

* Vikombe 2 vya brown rice au basmati au mchele wa kawaida uliosafishwa vizuri

* Vikombe 3 vya maji au chicken broth

* 2 tbsp sukari ya brown

* 2 tbsp mafuta ya kupikia

* Karoti 1

* 1 vitunguu maji,swaumu,tangawizi

* Nyanya 1-2 zilizokatwa

* 1 tbsp mdalasini,binzari nyembamba (ikiwa inahitajika)

* Pilipili 2-3 za kunukia zilizokatwa au nzima

* Chumvi

11F75A15-1D6E-4CAF-93B0-70D18E49A2DF.jpeg


Mahitaji ya ku marinated kuku

* coriander safi (giligiliani), (iliyokatwa ndogo ndogo)

* majani ya parsley , (iliyokatwa ndogo ndogo, majani tu)

* Vitunguu 6 hadi 8 vitunguu, (peeled ,kukatwa ndogo ndogo)

* 1 tsp chumvi

* 1 tbsp ya binzari nyembamba (ground cumin)

* paste ya swaumu na tangawizi
404C1E73-BA58-41C4-AEB9-60F11892F3F2.jpeg





1.washa jiko moto wa chini ,Weka mafuta kwenye sufuria kubwa (napenda kutumia sufuria ya chuma) na ongeza sukari ya brown kwenye mafuta na koroga hadi iwe nzuri na giza (kama unatengeneza shira ya kashata vile ) ikipanda na kutoa povu (bubbling) ni tayari

2.kuwa makini isiungue ,itasababisha chakula kuwa kichungu

3. mafuta na sukari vikiwa tayari,weka nyama yako kwa uangalifu kwa sababu iyo caramel (shira) itaruka na kukuchoma vibaya sana (ninatumia mfuniko kama ngao yangu) koroga nyama na ufunike vizuri na wacha ichemke kwa takriban dakika 10 na koroga kila baada dakika chache. Kuelekea mwisho wa dakika kumi ikiwa nyama sio brown kama unavyotaka ongeza mdalasini wa unga na binzari nyembamba ya unga

4. Sasa ongeza moto kwa dakika chake koroga mpaka nyama ikauke vizuri isiwe na mchuzi chuzi

5.ongeza veggies zako (vitunguu, swaumu,Tangawizi,karoti na nyanya,hoho napenda pia kuongeza tsp ya fresh grean seasoning kijani kwa ladha ya ziada),koroga bila mwiko (sauté) kwa dakika chache, kisha ongeza mchele wako na njegere na koroga kila kitu vizuri ili mchele uchukue ladha zote sawasawa

6. Ongeza supu yako ya kuku au maji ,tui la nazi ,chumvi na pilipili nzima ,koroga (stir)

7. funika punguza moto chini kabisa, na wacha kwa dakika 30 (Ukiamua kumaliza kwenye oveni hakikisha unawasha Kabla kwa digrii 350,utapika katika oveni kwa muda sawa wa dakika 30)

8. Mara baada ya kuiva unaweza ku serve na salads, au kipande cha avocado na sauce ya pilipili

9. tahadhari wakati wa kuwekapilipili nzima inaweza kupasuka,kwa hivyo use at your own risk. Lakini wakati mwingine huwa naweka tu kipande wakati ninapoongeza vitunguu kwenye sufuria.kama una watoto ni vizuri kuongeza tu sauce ya pilipili baadaye kwenye sahani kwa wanao tumia .
515C56C2-14B1-4DDC-9636-C40C53665810.jpeg


farkhina LadyRed
 
Back
Top Bottom