Kuku wangu wa mayai wamegoma kutaga wanaelekea week ya 19

Usifuate yale makaratasi ya motivational speakers, naongea kama animal production scientist. Kwa umri huo angalau ungekuwa umeshaanza kuokota mayai kidogo kidogo. Chakula cha layers hakifanani na cha broilers kiasi kwamba kitawanenepesha. Wape chakula cha kutosha kuandaa mwili kwa ajili ya production.
 
Kuku wana stress yawezekana housekeeping yako ni mbovu.
Waite madaktari wa kuku wakupe msamiati wenye mashiko.
 
Stress 😬
 
Kwa kuku 1000 ni sawa sawa kabisaaa tena umejitahidii sanaa mnoo.....mimi nilifila 19m miezi 6 wakaanza kutaga
 
Kwa kuku 1000 ni sawa sawa kabisaaa tena umejitahidii sanaa mnoo.....mimi nilifila 19m miezi 6 wakaanza kutaga
Ngoja tuendelee kupambana naamini watataga maana wote wanaonyesha dallili za kutaga ngoja niwe mvumilivu mpaka week ya 22/24 nione.
 
sawasawa kazana wakianza kutaga uwe unakijana wakukusanya mayai haraka kila saa uko bandani kisha funga cage nenda sido kuna watalamu wanajua kuchomelea vizuri cage wanaweza kukundia cade imara kabisa na za kisasa
 
Kwanza ongeza, jambo la kwanza ongeza chakula kwa kuku maana wiki ya 18 wanatakiwa kula gm 85, 90,95, hivyo alafu wape vitamini hasa zile nzuri za maji .
Jambo jingine jitahidi kuanzia sasa ratiba ya chakula iwe saa 12 kamili asubuhi usharika kila kitu bandani maji na chakula kwa 70 au 60 % then 30 au 40% wapewe jioni iwe ratiba. Kama uwezi kuamka saa 11 sahau biashara ya kuku wa mayai maana inabidi uwatrain hivyo ili kupata matokeo mazuri .kuhusu chakula kama una mtaalamu unaweza tengeneza cha kwako ili kucut cost
 
Sawa mkuu.
 
Wauzaji wavifaranga utasikia, Hawa wataanza kutaga miezi mitatu na nusu!! Hao wanamsababishia mfugaji presha na ushirikina,
Ila bajeti ya kuku wakifikisha miezi minne ni hatari, kwa hao kuku 1000, ka laki kanaweza kupotea kwa wiki
 
Laki kwa week labda wawe wanakula pumba tupu, mfuko tu mmoja wa layers ni elfu 59. Kuku elfu 1 wanakula zaidi ya mifuko 21 kwa mwezi. Kwahio hapo nizaidi ya laki 3 kwa week.
 
consider underfeeding kama sababu

kwa kawaida, kuku wa umri huo wanakula 110gm - 115gm kwa siku sawa na kilo 115 kwa kiwango cha chini tena maeneo ya joto kama daresalaaam

pia angalia kiasi cha mwanga unacho wapatia, kipindi cha wiki ya 16,17,18 tunashauri kuongeza mwanga kwa kuku kutoka masaa 12 mpaka masaa 16, hivyo unatakiwa uwe unazima taa saa4 usiku, lkn unatakiwa uwe unaongeza taratibu taratibu.

Kama utataka maongezi zaidi njoo pm, tubadirishane mawazo
 
Juzi nimeokota yai la kwanza, Jana nimeokota manne.
 
sawasawa kazana wakianza kutaga uwe unakijana wakukusanya mayai haraka kila saa uko bandani kisha funga cage nenda sido kuna watalamu wanajua kuchomelea vizuri cage wanaweza kukundia cade imara kabisa na za kisasa
Juzi nimeokota yai Moja la kwanza, Jana nimeokota manne. Hii ni week ya 19.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…