Kula mgahawani na kupika mwenyewe kipi kinamaliza pesa kwa upande wako?

Dah sisi home nazi ndio kila kitu,nazi tamu bwana halafu nazi haikarahishi na kila unavyoiweka nyingi ndio utamu unazidi
 
Daah tambi [emoji13][emoji20] chakula hii sipendi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inategemea unaishi wapi! Kwa hizi nchi za watu huku dunia ya kwanza kula kwenye mgahawa ni gharama sana! Kupika ni cheap cause mavyakula yapo kibao supermarkets kwa bei ya chini sana + nishati ya kupikia iwe ni gas au umeme ni very cheap.
 
Kuna mama ntilie flan kila siku anakuja na maji alojisugulia miguu kisha anayapikia!nyie endeleen kula mahotelin na maj y kuoshea mait na makohoz ya wod y TB.cheap is expensive

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu hili jambo karibia wengi tuliopitia ubachela na hatukuwa tunaishi na wazazi basi tumelipitia sana.

Kipi kinamaliza sana pesa ?
Kula mgahawani unatakiwa kuwa na makadirio na bajeti ya hali ya juu sana ya pesa. kuna uzuri na ubaya wa kula mgahawani ila inategemea na aina ya mgahawa vilevile, kuna mama nitilie, kuna BBQ, kuna restaurants na kuna maeneo ya chakula kama BAR...

UZURI: Unapata chakula kwa muda huohuo pamoja na kwamba kinaweza kisiwe kama kile unachotaka, huna muda wa kuosha vyombo kwa wavivu inawapa tabu sana na maisha yanaenda.

UBAYA: Unakula chakula ambacho wameweka viungo unavyovijua na vingine hujui, wengine huweka hamira kitu ambacho wengine hawapendelei, wengine hupika usivyotaka yani yale mapishi, wengine hukulaimisha ule ilimradi wapate hela yako tu, unaweza ukala uchafu ambao hujawahi kula maisha yako yote. ndoto zako zinaweza zikafifia mara kwa mara kisa huwa unakula mgahawani...

Kupika nyumbani au kujipikia ni kuzuri vilevile zingatia unapokwenda kununua mahitaji yako je wanataka hela tu au wanakuuzia chakula ambacho kiko safi na sahihi kwa afya yako.
 
Ni kweli mkuu sisi kwa maisha tuliyoishi Ulaya na bei za kule bora tu kujipikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hesabu na mazingira uliyopo. Km una friji inaweza kuwa nafuu na salama kupika mwenyewe. Ukichemsha maharage nusu kg Tshs.2000 unatumia milo mpaka minne. Utayachemsha kwa mkaa wa 1000. Ukinunua unga kilo 1 1000 ni wastani wa Milo 3 kwa mwanaume. Baada ya hapo unanunua majani fungu la 300 milo 2. Kuna unafuu na ubora km so mvivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mhhhh! Ukweli kula kwenye mgahawa kuna kutumia fedha nyingi zaidi! vijana wa sasa msidanganyike, mimi ni kijana wa zamani umri wangu ni = 50+ ukiniona uwezi amini, pamoja na kwamba ninaye wife, ila mala kadhaa wife anapokuwa mbali nami kutokana na majukumu yetu ninajipikia mwenyewe home. Chakula cha kujipikia ww huwa kinakuwa na lishe bora+Usafi n.k. niliacha kula kwenye mahoteli na migahawa baada ya kugundua ya kwamba humo kwenye vyakula vyao baadhi yao wanatumia maji yaliyochanganywa na maji ya k*m* ili kuvuta wateja na madawa mengineyo ya kienyeji, wengine huwa wana mix na amira ili chakula kiwe kingi.hata ukibisha huo ndiyo ukweli.
 
Mimi napika mwenyewe na nikiwa busy nakula mgahawani.
Ndani nina kila kitu
Mchele
Unga
Mafuta
Mkaa
Gas
Siku sijisikii kula mtaani,naweza nunua mchicha fungu moja tu la 200,nyanya za 200 na kitunguu cha 100 kwa gharama ya sh 500 nakula ugali wangu safi kabisa na mchicha na kachumbari pembeni,huku nimepachika maharage ya jioni robo mia 500 ambayo yatabaki hadi kesho asubuhi na wali uliobaki vilevile.
Maisha ni namna unavyopangilia ratiba zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupika Geto ni gharama kama Huna friji kwamba ukinunua nyanya za buku lazima utumie zotee... Ukinunua nyama nusu huwezi tumia kwa siku hata nne...!! Lakini kama una friji na vitu unanunua kwa jumlaa aisee kununua Chakula ni Gharamaa sanaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
In any case home nitakula usiku tu, mchana kutwa niko mtaani. Sasa hussle yote hio chakula cha usiku? Muda nao ni pesa,kwa Mama ntilie cheaper kwangu.
Hivi JF kuna mtu hana jokofu?

Tupo Mkuu
 
Kabisaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…