Kula mgahawani na kupika mwenyewe kipi kinamaliza pesa kwa upande wako?

Kula mgahawani na kupika mwenyewe kipi kinamaliza pesa kwa upande wako?

Uzuri wa kujipikia unapata kiporo cha kula asubuhi,ila mi napenda zaidi kujipikia na siku nikishinda home hasa weekend napika msosi kama ifuatavyo

Asubuhi
Nanunua samaki wa elfu 3 sangara namkata vipande 4 vitatu nakaanga

Kichwa natengeneza mchemsho wa viazi na samaki for breakfast

Mchana

Napika wali ambao nakula mchana,usiku na kesho asubuhi
Mboga ni wale samaki niliokaanga

NB: Huwa ninanunua stock ya kutosha mchele,mafuta,viazi vitunguu mi nakua na gharama tu ya mboga mwezi nzima

Kupika unaenjoy na unakula msosi wa kushiba

Sent using Jamii Forums mobile app
Msosi wa nyumbani mtamu kama unajua kupika lkn, halafu usafi asilimia nyingi kwa uhakika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupika ndo mpango mzima.... Japo ndo hivo majukumu yanakaba Ila napendelea sana kupika kwa mikono yangu, nakua huru kujipikia chochote kile nnachotaka, kwa viungo vyovyote nnavojiskia, na tumbo linashiba ile ile inavyotakiwa tofauti na ambavyo nashiba Nikila mgahawani
 
Mimi naishi mwenyewe. Sina jiko wala plan ya kuweka jiko anytime soon.

Muda ni pesa. Kupika mwenyewe maana yake nifanye manunuzi, preparation, nipike, nioshe vyombo. Hayo ni masaa kadhaa.

Hivi sasa kengele ya tumbo ikigonga, naelekea barabarani, naagiza, nakula, nalipa, napotea. 30 minutes kama wait staff wako vizuri.

Plus options zangu za msosi haziko limited to vile ninavyojua kupika tu.

Kula kwenye migahawa is more economical kama muda wako ni pesa.
 
Jamani mi nikila nje lazima tumbo lijibu, na ni sehemu classic tu, tumbo linavimba, minyoo kibao....sijui ni hamira zile

Ninakula tu basi na mara chache sana sana!

Labda kwa mwezi mara moja!

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah aisee.

Unatakiwa ukale sehemu zenye kueleweka mtafute Mother Confessor ana kahotel kake naskia wafutwa mpska jasho la mdomo baada ya kuls ns wahudumu.
 
Ni kweli kabisa. Kwa kifupi hakuna formula kuwa kupika (X) au kula mgahawani (Y), basi tendo X ni ghali zaidi ya Y. Kuna factors nyingi za kuzingatia. Vitu kama location, unapika/kununua chakula gani na mko watu wangapi vinaweza kubadili kabisa cost. Hata amount ya chakula unachopika vile vile.
Mkuu kwenye mlinganyo wako(huo) umesahau variable taste/Radha ya chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimewaza sana kwa nini zamani ilikuwa maandazi matatu unashiba mpaka mchanaa?

Alafu wakati ule ndo michezo mingi na chakula ndo kinatumika sana tumboni,ila ukubwani huku mtu na kszi za kukaa ofisini anapiga misupu mchana michipsi.

Mimi saivi nimerudia utaratibu wangu wa zamani.
Ratiba yangu asubuhi ni 500 tu.kwa sababu zamani mia tatu ilinitosha sana seuze saivi.

Na kula kwangu mpska nihisi njaa.

Aisee nainjoy sana.

Kuna mambo mengi ya kufanya zaidi ya kula.
Sasa ukishakula hiyo 500 njaa c ni nusu saa tu, hakuna unacho enjoy unajiumiza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ghettoni sijuwi kupika yaani najua ugali tuu (udaga)..
Nakulaga migahawani tuu. mwenye kujua kupika anifundishe plz
 
Ukiwa na friji unaweza pika hata mboga ya siku ya tatu ,na kama una kila kitu ndani friji inakusaidia vitu mboga isiharibike,lakin kama huna friji ni gharamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
In any case home nitakula usiku tu, mchana kutwa niko mtaani. Sasa hussle yote hio chakula cha usiku? Muda nao ni pesa,kwa Mama ntilie cheaper kwangu.
Hivi JF kuna mtu hana jokofu?
 
Kwa Ulaya kula mgawani ni uhujumu uchumi binafsi.
Hahaha kesi yake haina dhamana.
Lakini kupika mwenyewe ni time consuming na ni very expensive. Kwanza unanunua vitu vingi zaidi ya unavyovihitaji, Utanunua chumvi nyiingi, Sukari nyiingi, na hata unga na mchele mwingi, mafuta ya kula mengi. bado zile wabongo tunaita MBOGA hahahaha. Nyama au Samaki, nyiingi. Ukianza kupika unatumia umeme au gas unalipa bili kuubwa bila sababu. mi nadhani kujipikilisha ndio gharama, na unajihujumu bila kujua. Ingawa unapata self gratification ya kula unachopenda.
ukila nje kwanza huli mara kwa mara, pili unakula kwa kiasi au kidogo na una save muda wa kuosha vyombo, pili una save bill ya umeme, halafu untakula balanced diety an utakula milo tofauti tofauti.
Acheni kupika mwezi mmoja muangalie gharama za kula nje na kupika utagundua kupika ni gharama sana.
 
Nilikuwa namuona maza kuanzia saa 10 mpaka saa 1 yeye yupo jikoni.hiko chakula sasa hatarii.ngoma mchuzi mzito mpaka tunauita mchudhi mdhittoo..ukibinua bakuli mchuzi haumwagiki umegandaa kwa futa la nazi.
weee acha bhaaaaa😋
 
Back
Top Bottom