Kuliko kuchomwa moto wa Milele ni Vyema na haki Mungu akatufanya watumwa. Tuwatumikie watakatifu huko mbinguni

Kuliko kuchomwa moto wa Milele ni Vyema na haki Mungu akatufanya watumwa. Tuwatumikie watakatifu huko mbinguni

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Mimi kila nikitazama mbele sioni kama nitatoboa na hatimae kuingia paradiso.

Nimekaa nikafikiria na kuwaza sana Mungu atakuwa na faida Gani iwapo atatuchoma moto wa Milele?

Na vipi tulio tiyari kufanywa watumwa tuwatumikie tu hao watakatifu wake?

Kwakweli kutuchoma moto hapana manabii pelekeni mawazo yetu haya aambiwe afikirie mara2 zaidi.

Adhabu ya moto Haina manufaa wala faida yoyote kwake.

Mwisho
 
Mleta mada kumbuka watenda dhambi kamwe hawatoenda mbinguni.
Inasemekana siku ya kiama hesabu zitafanywa yeah atakuja kuchukua watu wake walio wema bila hata chembe ya dhambi na kuenda nao mbinguni kwa Baba

Kisha watenda dhambi watachukuliwa na shetani na kwenda kuchomwa moto wa milele huko jehanamu
 
Najua hilo lakini Mungu anaweza kutubadilisha badala ya kuendelea kuwa watenda mabaya tukawa watenda mema tupu
 
Vipo wapi thibitisha
Mambo mengi yanayohusu Mungu ni ya imani zaidi. Huwezi kuyathubitisha kwa kisayansi. Endapo unaamini juu ya uwepo wa Mungu aliyeziumba mbingu na ardhi, basi unatakiwa pia kuamini maneno na maelekezo yake yaliyopo kwenye maandiko matakatifu. Ukitaka kuthibitisha kila kitu alichoelekeza Mungu kibinadamu, basi utapata taabu sana!
 
Hapa sio kanisani , haya sio mahubri, hii ni forum huru , ukiweka jambo humu sio lazima kila mtu aliamini bila kuhoji.
 
Mungu ambaye alikuwa na uwezo wa kuumba binadamu wema tu, watakao mtii na kumwabudu siku zote, Lakini akashindwa kufanya hivyo, Badala yake akaumba binadamu wenye uwezo wa kutenda mabaya na dhambi ili aje awachome moto. Mungu huyo ni Katili, Mpumbavu na Mwendawazimu.

Huyo Mungu anastahili KUFURUSHWA huko alipo maana hajielewi kabisa.
 
Vipo wapi thibitisha
Sio lazima nikudhibitishie kwa sababu
Najua hilo lakini Mungu anaweza kutubadilisha badala ya kuendelea kuwa watenda mabaya tukawa watenda mema tupu
Mkuu watu bilioni ngapi sijui tunaenda kujazana mbinguni kufanya nini na nasikia hata Mungu mwenyewe kamwe hatuwezi kumuona hata tukiwa huko mbinguni
 
Najua hilo lakini Mungu anaweza kutubadilisha badala ya kuendelea kuwa watenda mabaya tukawa watenda mema tupu
Mungu muweza wa vyote, alishindwaje kuumba binadamu wema tu, watakao tenda mema siku zote na wakati wote?

Ni Either Mungu huyo si Muweza wa vyote au Hayupo.

Kuwepo kwa Mungu Muweza wa vyote kwenye Dunia yenye maovu na binadamu watendao mabaya kunaleta Logical Contradiction.
 
Mimi sitakulazimisha uamini uwepo wa Mungu bro
Wewe endelea tu kuwa atheist
"Sio hadithi mkuu.Mungu,paradiso, shetani na jehanamu vyote vipi.
Na Siku moja kiama kitatokea na huo ndo utakuwa mwisho wa Dunia"

Hivi unakumbuka kweli ulicho ni reply? Kama sio Hadithi tu thibitisha kuwa sio Hadithi , Sitaki blabla tu.
 
Back
Top Bottom