Kulikoni Waziri Liberata Mulamula! Au Ameparura Mahali?

Dr. Patricia Laverley amekwenda kumpokea Rais kule kama representative wa African development Bank Tanzania; kumbuka hao African Development Bank ndio walimualika kwenda Ghana kumpatia tunzo!
Kama ni hiyvo, basi rais wetu alitakiwa apokelewa na rais wa ADB!
 
Ni kitambo sasa tangu tumuone akiwa bega kwa bega na Rais Samia kwenye ziara za kimataifa, kama inavyopaswa kuwa.

Na Pia katika shughuli zingine za kidiplomasia, ndani ya nchi kama tulivyokwishazowea. kumuona.

Mara ya mwisho hadharani, kama sikosei ilikuwa ni kwenye ziara ya Rais Samia kwenda kuhutubia Baraza la umoja wa Mataifa nchini Marekani.

Huyu ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania.

Kidiplomasia anawajibika kuwepo kwenye shughuli zote za Kiserikali, zinazohusiana na Diplomasia na mahusiano ya kimataifa. Pale anapokuwepo Rais kwenye ziara za nje ya nchi.

Hata huyo JK...kilichompatia uzoefu na hadi kuwaaminisha watanzania kwamba angeweza kuongoza nchi hii.
Alianzia huko huko kwenye ziara za Mzee Mkapa (R.I.P).

Liberata Mulamula alianza kwa kasi na kuwa na vyombo vya habari mara nyingi,akiitolea taarifa mbalimbali Serikali kupitia Wizara yake na matukio husika.

Lakini kuanzia kwenye Royal Tour, hatukumuona tena na badala yake tulimuona Bwana Hassan Abbas na wengineo akiwemo Zuhura Yunus.

Hali imeendelea hivyo na hata ziara zilizofuatia hivi karibuni.
ikiwemo ya Uganda na sasa huko Ghana.

Tunaomba mwenye kujua nini kilichomsibu waziri wetu.
Atuwekee hadharani, kwa sababu huyu ni kiongozi wa umma na anapaswa kuwepo kwenye eneo lake la kazi kwa mujibu wa sheria na katiba.
Kwani lazima aende yete tu??
 
Uongeaji wake yule mama haueleweki anacheka cheka tu hovyo.
Nakomelea msumari, upo sahihi kabisa, sijawahi kumuelewa kabisa ...chekacheka nyingi hata kwa mambo yasiyojulikana
 
EeeHeee, kwani ni wewe peke yako mnufaika na mambo ya ainahiyo mkuu?
Wengine hayo mambo hatuyasemi.

Hili tuliachie hapa, linatosha.
Kama wewe ulifanya na ARL na huyasemi hata kama context ya mjadala inayahitaji basi ni vizuri sana, lakini yasingekushangaza. Kuonyesha kuyashangaa mwanzoni ni wazi kuwa ulikuwa huyajui ila sasa unataka kujipandisha kuwa na wewe ni mmoja wa wanaofanya research na Pentagon kupitia Labs zao. Nadhani wewe una tatizo fulani na Kichuguu tu, na niliwahi kukuambia kuwa utapata tabu sana kama hiyo ndiyo ajenda yako.
 
Ni kweli; wakati Covid inaanza, kulikuwa na mkanganyiko sana, na hivyo Kabudi akafanya hayo makosa ya kuamini shortcut. Hilo ni kosa lake moja tu kati ya mengi mazuri aliyofanya katika kuproject interests za Tanzania.
Sasa lawama anabebeshwa Kabudi?
Haya si ndiyo maajabu ya nchi yetu? Kuna watu hata ukiwaambia hili ni koreo, wao hawakubali, watasema ni kijiko kikubwa!

Mtu utaanzia wapi kujustify upumbavu mkubwa uliokuwa unafanyika Tanzania kuhusu ugonjwa huo!

Halafu katika pumzi hiyo hiyo, leo hapa, kwenye mada hii hii, tunadai tumefanya "Research" na ARL? Ni utafiti wa namna gani huo, unaofanywa na watu wanaoonekana kuamini matendo ya viongozi ambao walikuwa wakienda kinyume kabisa na 'facets' zote za kitafiti?
Au ini aina ya utafiti wa kukusanya taarifa zilizochapishwa magazetini? Lakini ninaamini hata huo unahitaji kuwa na taratibu za kisayansi juu yake.
 
Kama wewe ulifanya na ARL na huyasemi hata kama context ya mjadala inayahitaji basi ni vizuri sana, lakini yasingekushangaza. Kuonyesha kuyashangaa mwanzoni ni wazi kuwa ulikuwa huyajui ila sasa unataka kujipandisha kuwa na wewe ni mmoja wa wanaofanya research na Pentagon kupitia Labs zao. Nadhani wewe una tatizo fulani na Kichuguu tu, na niliwahi kukuambia kuwa utapata tabu sana kama hiyo ndiyo ajenda yako.
Kilichonichekesha ni jinsi ulivyoyawasilisha. Hapana, sikufanya na ARL, kuna taasisi nyingi nyingine huko huko zinazofanya tafiti za kisayansi hasa!
 
Sasa lawama anabebeshwa Kabudi?
Haya si ndiyo maajabu ya nchi yetu? Kuna watu hata ukiwaambia hili ni koreo, wao hawakubali, watasema ni kijiko kikubwa!

Mtu utaanzia wapi kujustify upumbavu mkubwa uliokuwa unafanyika Tanzania kuhusu ugonjwa huo!

Halafu katika pumzi hiyo hiyo, leo hapa, kwenye mada hii hii, tunadai tumefanya "Research" na ARL? Ni utafiti wa namna gani huo, unaofanywa na watu wanaoonekana kuamini matendo ya viongozi ambao walikuwa wakienda kinyume kabisa na 'facets' zote za kitafiti?
Au ini aina ya utafiti wa kukusanya taarifa zilizochapishwa magazetini? Lakini ninaamini hata huo unahitaji kuwa na taratibu za kisayansi juu yake.
Ndiyo maana nimesema una matatizo kwani hata huangalii kuwa post hiyo ilikuwa inajibu nini na hujui kuwa niliandika nini jinsi Magufuli alivyosimamia ugonjwa huo. Habu some thread hii ujue watu wasiokuwa biased wanavyoangalia mambo.

Mimi professionally ni injinia, sasa sijui unategema ni injinia gani anaweza kuaminiwa na ARL kufanya research ya kukusanya ripoti za magazeti.
 
Injinia aliyeng'ang'ania uwanja wa ndege wa Chato, anaweza kufanya lolote.
Unaweza kuwa injinia ukawa mtafiti wa kukusanya taarifa tu zilizochapishwa, kwani hilo nalo ni la ajabu?
 
Unazidi kuonyesha weakenesses zako kwenye mijadala hapa.
 
Marekani alipoivamia Iraq kwa kuzusha uongo wa silaha za maangamizi hatukusikia diplomat yeyote akijiuzulu.

Diplomats wa marekani hawana integrity?!
Hawana hata chembe. Wangekuwa na integrity angalau kidogo tungesikia angalau mmoja wao anatubu au kuomba radhi kwa ule uongo wa wazi.
 
Saivi ziara za mama anapokelewa na MADIWANI wa nchi anapoenda, so Balozi Mulamula kaona akaushe tu maana atashusha heshima yake amemuacha maza apuyange mwenyewe, yeye kama ni ng'ambo kakaa saana, wakati huo maza akiwa home.
Hata mwanzoni nilidhani mama kadharauliwa mpaka kupokelewa na MADIWANI Ghana ila baadae nikagundua hakua only head of State alieenda kwenye mkutano ule. Rais mwenyeji hawezi kwenda kupokea wageni wote.
 
Kama kagonga 60 si apumzike ale pensheni
nchi maskini zote Mazee huwa hayana akili yanaogopa maisha kuliko hata sisi vijana wakati muda wao umeisha kwa mujibu wa biblia 70 au 80 tu mtu kwishney !!

huwa mazee yaliyoajiriwa serikalini hayakubali kustaafu matokeo yake siku moja yakiwa ofisini yakapata habari mbaya huanguka ghafla na kufa kwa presha!!
 
Kwanza yeye havai shuka kichwani, pili sio rahisi kwa wanawake kukaa pamoja bila kusiutana au hata kuoneana wivu ikiwa ni pamoja na kunyang'anyana mabwana
Unajua unaongelea wanawake wenye umri gani? SSH ana 62 na Balozi Mulamula yuko 66. Uwe na adabu kidogo basi dogo!!!
 
Hata mwanzoni nilidhani mama kadharauliwa mpaka kupokelewa na MADIWANI Ghana ila baadae nikagundua hakua only head of State alieenda kwenye mkutano ule. Rais mwenyeji hawezi kwenda kupokea wageni wote.
usiwe na akili za kijinga za kurudi nyuma za kimaskini kama wazee wetu za kuficha ficha na kufunika funika uchafu ndo maana wamezeekea nchi maskini ili kijana akili zako ziwe sharp kama kisu kikali nakushauri uwe unakubali ukweli na kunyoosha! iko hivi Bimkubwa wamemdharau wakaleta VICOBA kumpokea FULL STOP! kama alikuwa muhimu kwanini Rais wa Ghana akapokee wengine? ina maana waliopokelewa na Rais ndo wa maana kwake!!

Ndugu zangu mfumo dume wa kiafrika utajionesha siku zote Mama hakupokelewa na Rais wa Ghana wakaja kumpokea WATENDAJI KATA sababu ni Rais mwanamke, Biden hakuwa na stori nae sababu ni Rais mwanamke!!

ukimsikiliza Mh Rais Samia utagundua ni Genius
 
Ni kitambo sasa tangu tumuone akiwa bega kwa bega na Rais Samia kwenye ziara za kimataifa, kama inavyopaswa kuwa.

Na Pia katika shughuli zingine za kidiplomasia, ndani ya nchi kama tulivyokwishazowea. kumuona.

Mara ya mwisho hadharani, kama sikosei ilikuwa ni kwenye ziara ya Rais Samia kwenda kuhutubia Baraza la umoja wa Mataifa nchini Marekani.

Huyu ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania.

Kidiplomasia anawajibika kuwepo kwenye shughuli zote za Kiserikali, zinazohusiana na Diplomasia na mahusiano ya kimataifa. Pale anapokuwepo Rais kwenye ziara za nje ya nchi.

Hata huyo JK...kilichompatia uzoefu na hadi kuwaaminisha watanzania kwamba angeweza kuongoza nchi hii.
Alianzia huko huko kwenye ziara za Mzee Mkapa (R.I.P).

Liberata Mulamula alianza kwa kasi na kuwa na vyombo vya habari mara nyingi,akiitolea taarifa mbalimbali Serikali kupitia Wizara yake na matukio husika.

Lakini kuanzia kwenye Royal Tour, hatukumuona tena na badala yake tulimuona Bwana Hassan Abbas na wengineo akiwemo Zuhura Yunus.

Hali imeendelea hivyo na hata ziara zilizofuatia hivi karibuni.
ikiwemo ya Uganda na sasa huko Ghana.

Tunaomba mwenye kujua nini kilichomsibu waziri wetu.
Atuwekee hadharani, kwa sababu huyu ni kiongozi wa umma na anapaswa kuwepo kwenye eneo lake la kazi kwa mujibu wa sheria na katiba.
Ulimteua wewe?
 
Back
Top Bottom