Kulikuwa na uhalali gani kwa Chief Mkwawa kutambulika kama 'Shujaa?

Situation za Gaddafi na Saddam haziwezi kulinganishwa na Mkwawa wao wote waligeukwa na wananchi wao wenyewe na hakuna aliyekamatwa na mzungu

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Kwani ukigeukwa na wananchi wako ndio unashindwa kujiua? Kuna uhusiano gani kati ya kutojiua na kutokuungwa mkono na wananchi?
 
Mkwawa alishindwa vita vs German akaona hataweza vumilia humiliation mbele ya watu wake akaamua kujitoa uhai!hawa wengine waligoma kusoma alama za nyakati

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Hahahahaaaa eti walishindwa kusoma alama za nyakati karne hii ya 21 ya sayansi na teknolojia.
 
Una ufahamu mdogo sana..usiku mwema ASKARI
Infantry soldier kama kibaraka vile. Hata hatumuelewi. Linapokuja story chanya za waafrika anaponda hadi anataka kufiapo. Sijawahi ona wachina au wazungu wanaponda story zao. Tena wanadiliki hata kudanganya story ili waonekane wanaweza. Lakini muda ume wa prove wrong. Hadi sasa mwafrika ndo bado anaonekana anafanya vizuri physically and mentally. Hii utaiona kwenye sports na area nyingi tu. Ila kwa sababu wanao control dunia ni wahabeshi. Basi favour yote inaelekea kwao. Kuna blacks wengi wanafanya the best ila wanafunikwa.
Hatukatai. Waafrika tuliteleza katika point fulani ya maisha kwa sababu ya roho nzuri za kukaribisha wageni na kuwaheshimu. Sasa tumejifunza kitu kimoja kwamba kumbe roho mbaya inahesabiwa kua akili kwenye dunia ya sasa.
 
Mbona Saddam Hussein hakujiua? Ina maana himaya ya wahehe ya miaka hiyo ya zamani ilikuwa na siri nzito kuzidi Iraq ya mwaka 2003?...
Jibu hapo ni ndio. Unaweza kufahamu pia kww urahisi tu; vita ya iraq usa imepiganwa wakati teknolojia ikiwa wazi kabsa, pili, ni vita ambayo haijazidi miaka 3. Vita ya mkwawa vs ujerumani imepiganwa kwa takribani miaka 8; wajerumani walikuwa na teknolojia kubwa zaidi kuliko mkwawa, unàweza kurejea tu chanzo cha jina Tosamaganga inatosha kujua ufinyu wa teknolojia ya mkwawa vs ujerumani.
 
Yaleyale ya OKonko..kujinyonga baada ya watu wake kusema si kila cha mzungu ni kibaya.
 
Suala la kujitoa roho halina uhusiano wowote na hii justification yako mkuu. Kujiua ni uamuzi wa mtu unaohitaji risasi moja au mbili tu kukatisha uhai bila kujali usasa ama uzamani wa teknolojia.
 
Sio kila jambo ni la kusifia mkuu. Challenges lazima ziwepo
 
Infantry Soldier! Salute mkuu.
Naomba nami pia nichangiepo tafadhali.

MKWAWA MKWAVINYIKA BIN MUNYIGUMBA! SHUJAA AU MUOGA?

Ushujaa haumaniishi kuwa Utaishi au Utakufa!

Shujaa ni Matendo au Hiba ya Mtu aliyefanya jambo la Ujasiri na Uzalendo kwa Watu wake au Asili yake kwa gharama ambayo hailipiki.

Tuanzie Nchini kwetu, tuna siku ya Mashujaa - Kifupi huwa tunawakumbuka Askari wetu waliokufa na waliosaidia nchi yetu kupigana na kulinda mipaka yetu dhidi ya Fashisti General Amin (Kagera War 1978 -79).

Duniani kote huwakumbuka Mashujaa wao - hasa wale waliopoteza maisha,kuuwawa au kujiua kwa ajili ya Maslahi mapana ya Nchi zao.

Makao Makuu ya Shirika la Ujasusi la CIA - Langley Upo Ukuta wa Mashujaa wanaotambulikana kwa nyota tu na majina yao hubakia siri milele na familia zao hupewa hadithi za uongo juu ya vyanzo vya vifo vya wapendwa wao , na wengine huambatana na majina hasa wale ambao walijihusisha na Overt Operations.

Nyota Huchongwa na Kuwekwa katika Ukuta huo wa Heshima kuwaenzi mashujaa. Ni Maafisa walipoteza maisha katika Mission mbalimbali kwa ajili ya Maslahi mapana ya USA, wengine waliuwawa,kujiua na pengine kutoroka na kuishia kuuwawa cha msingi ulionesha kupambana au kufurukuta na ulifanya hivyo kwa heshima ya Nchi yako au Rais/Mfalme/Taasisi.

Mkwawa Alikufa KISHUJAA, ni Shujaa wa Afrika - Hakukubali Kuchukuliwa Mateka na kama viongozi wengi tu ambao pia walipoona wanaelekea kushindwa walifanya vivyo hivyo. (They defied Surrendering) and became Martyr.

Mwingine ni Cheif ISIKE -
Huyu Chief wa Wanyamwezi yeye alijilipua kwa Baruti pamoja na familia yake yote Wakafa, lakini chanzo ni pambano makali kati yake na Wadachi.

Bwana Heri na Cheif Hassan Makunganya hawa waliwapinga wajerumani na kupamabana nao lakini wao hawakujiua walikamatwa na Kunyongwa, Je Kunyongwa na Wajerumani au Kujinyonga wewe mwenyewe kipi ni Ushujaa.

Mkwawa na Isike walifanana katika hoja Moja - Walichukia hata kumuona Mzungu (mgeni) ,Kukamatwa na Mzungu ilikuwa ndio Ishara ya Uoga na Dhaliliko kubwa kwao, hivyo walijiapiza kamwe hawatakuja kukamatwa wala kunyongwa na Wadachi.

Shujaa Mwingine ni Mchg. John Chilembwe wa Malawi - yeye alijua kabisa hawezi kupigana na Wazungu hata kwa masaa 24! Lakini alihakikisha anawaonesha kuwa hawezi kufa kama kondoo lazima aoneshe kuwa na yeye ni Mwanaume - Ingawaje mwishoni aliamua kutimua mbio kuelekea Msumbiji wakamfuatilia na Kumuua.

Yupo Pia Mwenye Machemba Bin Mchakama wa Wayao - yeye aliwaandikia Barua ya Kuwatisha wajerumani kiasi kwamba hawakuamini kama ameandika akiwa anajua alichoandika - Maana alimalizia kwa kusema Kama mnanguvu za kutosha njooni mnitoe!.Aliposikia wanakuja alijaribu kupambana nao,mwisho alipoona mambo magumu akatimkia Msumbiji.

Shujaa ni Yule anayethubutu kupambana, anayeonesha amepambana haijalishi atashinda ama la! Chilembwe alikuwa na msemo wa "Strike a blow and Die"

Mwisho Samson The Great! huyu myahudi akiwa kipofu na mfungwa wa kusaga ngano Gaza,naye alipambana na adui za Israel na kuishia kufa na kuwauwa Wafilisti wengi kuliko aliowahi kuwauwa akiwa huru na anaona.

Wafia Dini wa Uganda! Walipambana na Kabaka Mwanga II na kuishia Kuchomwa kama mishikaki - lakini walitetea Imani yao hawakubadili Msimamo wao Kama Hamisi HK.

WHOEVER STRIKES A BLOW AND DIE FOR THE GREAT CAUSE, IS A HERO.
Asante.
 
Mkuu, labda itoshe tu kusema ya kuwa unaifahamu vema sana historia ya Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…