Kumbe Abushiri wa Tanga aliyepigana na wajerumani na kunyongwa hakuwa na maana yoyote

Kumbe Abushiri wa Tanga aliyepigana na wajerumani na kunyongwa hakuwa na maana yoyote

Hujui unachokiongea, Utumwa
ulikuwa ni unyama, binadamu alifanywa kama punda
Mtu anatolewa ujiji kigoma mpaka Pwani kwa miguu wakiwa wamefungwa mikono na shingoni kwa miti wengi walifia njiani
Vijiji vilikuwa vinavamiwa na nyumba kuchomwa moto wakati wa kukamata watumwa

Watumwa wengi walifia baharini kwa kuuawa na Waarabu au magonjwa
Wengi pia walifia shambani kutokana na kazi za shurba

Kumuuza binadamu mwenzako kama mtumwa hata kama sio wa kabila lako ni unyama wa hali ya juu, sijui ni akili gani unatumia kuhalalisha huo ujinga
Unaweza kuprove hili kwa Academic source kwamba hichi kilifanyika? Sitaki Story za Mtaani bali Msomi yoyote wa Historia mwenye kitabu kinachokubalika na Wasomi?

Hivi unafkiri Machief wakubali hivi hivi kuteswa na waarabu halafu Ghafla aje Mzungu wapigane nae?

Sikatai Utumwa ilikua ni Biashara mbaya ila mambo mengine yameongezwa tu Chumvi na hayana Evidence yoyote.

Mambo sijui mtumwa alitobolewa akawekwa mnyororo sijaona ushahidi wa Ki Academic na hata Common sense haingii akilini sababu utamshusha thamani.
 
Shuleni tulifundishwa habari ya Abushiri wa Tanga kupigana na wakoloni wa kijerumani. Alitajwa kama shujaa mpigania uhuru kumbe hamna lolote. Kumbe jamaa alikuwa anamiliki mashamba makubwa na watumwa. Kifupi alikuwa anapigania nafasi ya kuendelea kukandamiza wengine. Hakuwa na maana kabisa.
View attachment 2644629

Hawa jamaa wanataka kutuleta katiba mpya. Very Interesting. Nani atakuwa bwana na nani atakuwa mtumwa?
 
Biashara ya Watumwa na kumiliki watumwa kumekuwepo tangu kale sana. Hata biblia ina verse zinazohusu watumwa!
 
Naona Mnaanza kutukana mababu zenu.kuhusu utumwa hakuna mtemi au chief aliekua anauza watu wake.bali walikua wanauza mateka wa vita ingawa wote ni wa Africa
 
Kuna watu wamepigania hii nchi jaman. Kuna yule mwamba mpka jina lake likapewa mkoa (songea) jamaa alikua fighter kwenye vita ya maji maji mpka kuja kudakwa na wajeruman.wakataka kumtumia kama kibaraka ila akagoma,cku tatu akagoma kula cku ya nne wajeruman wakaenda kumnyonga ,
Ajabu kamba ilikatika,wakanyonga tena.kamba ikakatika,wakAnyonga mara ya tatu kamba ikakatika wakaona wampige risasi....
 
Unaweza kuprove hili kwa Academic source kwamba hichi kilifanyika? Sitaki Story za Mtaani bali Msomi yoyote wa Historia mwenye kitabu kinachokubalika na Wasomi?

Hivi unafkiri Machief wakubali hivi hivi kuteswa na waarabu halafu Ghafla aje Mzungu wapigane nae?

Sikatai Utumwa ilikua ni Biashara mbaya ila mambo mengine yameongezwa tu Chumvi na hayana Evidence yoyote.

Mambo sijui mtumwa alitobolewa akawekwa mnyororo sijaona ushahidi wa Ki Academic na hata Common sense haingii akilini sababu utamshusha thamani.
Duh..hivi hujui kuwa biashara ya utumwa ilivyokuwa ikifanyika ? Vipo vitabu vingi tu sema ni hardcopy
 
Duh..hivi hujui kuwa biashara ya utumwa ilivyokuwa ikifanyika ? Vipo vitabu vingi tu sema ni hardcopy
Pamphlet ama vitabu? Mkuu binadamu sisi tulivyo huwezi ukanichukua mimi utumwa ukanitesa ukanipeleka sehemu ukanifanyisha kazi, usinilipe etc nikakutii tu Haiwezekani.

Ndio maana weusi wengi waliopelekwa Marekani kinguvu waliasi na kupigana vita. Kuna vita vingi mno.

Hii ni website ya Taifa? Wameelezea vizuri sana nakushauri soma

Kwanza ufahamu mkuu Utumwa ulikua ni Mfumo kama mifumo mingine Ubepari, Jamaa Feudal etc.

Utumwa ulifanywa na watu wote Na kulikua na njia maalum za kuwapata.

Zamani Hakukua na Jela prisoners of wars waliuzwa kama watumwa, wenye madeni sugu waliuzwa etc, na ulikua pia unaweza nunua Uhuru wako, Pia watumwa hawakuwa treated vibaya kama historia inavyopotoshwa, watumwa wengi hasa toka Africa walitumika kama war Mercenaries na walipata vyeo vikubwa tu.

So ulikua ni Mfumo wa maisha kama mifumo mingine kulikua na watu weusi wanamiliki watumwa wa kiarabu, warabu wenye watumwa wazungu etc.

Historia ya Utumwa ilikuja Kubadilika baada ya Kugunduliwa America na kuwa target watu weusi hapo ndio ilikua kamata Kamata na watu kuonewa.

Kwa akili zetu fupi unatumia time line ya sasa kuwa Judge ila kwa wakati wao walikua ni Mashujaa na waliwatendea haki wanaowaongoza kwa kupigana hadi kufa,

Watawala wa Ki Zamani walikua makatili kwa Makabila ya Nje ila makabila yao walikua mstari wa Mbele kuyapigania.

Unafikiria Mkwawa, Bushiri, Kinjikitile na wengine walishindwa kuchukua 10% toka kwa Wakoloni na kuuza Makabila yao? Waliweza kufanya hivyo ila wakaamua bora kufa kuliko kusaliti watu wao. Kitu hichi hukipati popote sasa hivi nchi hii.
Unalopoka sana, unayajua madhara ya utumwa wew? Umezaliwa juzi tu na kusoma vijitabu vilivyochakachua historia alafu huoni madhara ya utumwa? , rudi vijijin huko kuna wazee wanahistoria kamili jinsi wazazi wao walivyobakwa+kulawitiwa adharani, kuuwawa na wengine kukatwa viungo vya mwili ikiwa kama adhabu, wengineo kunajisiwa na wanawake kutolewa mimba bila kusahau kuhasiwa kwa wanaume ili kuzuia uzao wao kuongezeka.

pili toka nje ya box kuna vitabu na nyaraka nying zinazofichua maovu ya wakoloni na utumwa kiujumla.

Jambo alilotendewa muafrika ni baya ambalo hakuna jamii yoyote hapa duniani imewahi kutendewa, according to the real history.

Tuliyofanyiwa watu weusi kama wangefanyiwa wazungu+waarabu ungeona ambavyo wangepromote na kuzusha mengi ili wapate fidia na attention ya dunia, mfano kwa wale wayahudi feki waliozusha kuteswa na hitra na kuuwawa wayahudi mili6 kumbe hawakuzidi hata mia6, lkn unaona wanavyozusha propaganda za kuonewa kuwa walikuwa matesoni na utumwani blah blah nyingi zisizo na ushahid, lkn muafrika kafanyiwa unyama mwingi na ushahidi upo je kuna nguvu yoyote ya kujitetea dhidi ya hao wahuni?

Someni historia jmn watu weupe ni washenzi wa kila kitu hapa dunian no matter wamekusaidia nn lkn ushenz wao uko pale pale.
 
Kuna watu wamepigania hii nchi jaman. Kuna yule mwamba mpka jina lake likapewa mkoa (songea) jamaa alikua fighter kwenye vita ya maji maji mpka kuja kudakwa na wajeruman.wakataka kumtumia kama kibaraka ila akagoma,cku tatu akagoma kula cku ya nne wajeruman wakaenda kumnyonga ,
Ajabu kamba ilikatika,wakanyonga tena.kamba ikakatika,wakAnyonga mara ya tatu kamba ikakatika wakaona wampige risasi....
Vita ya majimaji historia yake inapotoshwa sana. Walipigana watu wa pwani. Watu wa Songea waliingia mwishoni kabisa.
 
Kuna watu wamepigania hii nchi jaman. Kuna yule mwamba mpka jina lake likapewa mkoa (songea) jamaa alikua fighter kwenye vita ya maji maji mpka kuja kudakwa na wajeruman.wakataka kumtumia kama kibaraka ila akagoma,cku tatu akagoma kula cku ya nne wajeruman wakaenda kumnyonga ,
Ajabu kamba ilikatika,wakanyonga tena.kamba ikakatika,wakAnyonga mara ya tatu kamba ikakatika wakaona wampige risasi....
Zous,
Huyu uliyemtaja jina lake ni Abdulraufu Songea Mbano lakini wanahistoria wamefuta jina la ''Abdulraufu'' wanamwita Songea Mbano.

Kaburi lake lipo peke yake Mahenge Songea kwenye makumbusho ya Vita Vya Maji Maji pembeni ya kaburi la halaiki ambalo majemadari wenzake wa vita hivyo wamezikwa.

Kuna historia ya kusikitisha sana ya kunyongwa kwao.

Majemadari hawa walikuwa Waislam na hukumu ya kuuliwa kwao ilipopitishwa na Wajerumani alikuja mmeshionari kutoka Peramiho akawaambia kuwa ikiwa watakubali kubatizwa hawatanyongwa.

Hii ilikuwa ghilba waliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo kisha wakawanyonga.
Orodha ya majina yao ipo hapo Mahenge kwenye mnara wa kumbukumbu.

Katika hawa majemadari kuna mwanamke pekee aliyenyongwa huyu wanamwita kwa jina moja ''Mkomanile'' lakini jina lake la Khadija Mkomanile.

Wanahistoria wamefuta jina lake la Khadija.

1685851132801.png

Majemadari walionyongwa wa kwanza kulia waliosimama n Abdulraufu Songea Mbano
1685851269675.png

Nduna Abdulraufu Songea Mbano

Pamphlet ama vitabu? Mkuu binadamu sisi tulivyo huwezi ukanichukua mimi utumwa ukanitesa ukanipeleka sehemu ukanifanyisha kazi, usinilipe etc nikakutii tu Haiwezekani.

Ndio maana weusi wengi waliopelekwa Marekani kinguvu waliasi na kupigana vita. Kuna vita vingi mno.

Hii ni website ya Taifa? Wameelezea vizuri sana nakushauri soma

Baba...
Nimeingia katika hiyo website.

Sijui kwa nini wenyewe wameweka nembo ambayo inaashiria ni website ya serikali ya Jamhuri ya Tanzania.

Nimeipitia kwa haraka na nimeona makosa katika ukweli na lugha.
 
Aisee kumbe tulifundishwa upumbavu mtupu kumbe lilikuwa dubwana la hovyo tu.
Wadiz,
Ukifika Mkwawa Museum Kalenga utakuta historia ya urafiki kati ya Abushiri na Mtwa Mkwawa.

Utakuta bunduki ambayo Abushiri alimpa Mkwawa na ndiyo bunduki iliyomsaidia Mkwawa kuanza kutengeneza bunduki nyingine yeye mwenyewe.

Hii ndiyo bunduki Mkwawa aliitumia katika vita vya Wahehe na Wajerumani.
Mkwawa na Abushiri walifanya biashara pamoja.

Abushiri ndiye aliyemsilimisha Mtwa Mkwawa akawa Muislam na Mkwawa akachagua jina la Abdallah.

Abushiri hakuishia hapo alimfundisha Mkwawa kusoma na kuandikwa kwa hati za Kiarabu hadi akajua.

Barua za Mkwawa zipo hapo Mkwawa Museum.

Baada ya kusilimu Mkwawa akawa hampi mtu uongozi katika himaya yake hadi kwanza amekuwa Muislam.

1685853317157.png

1685853373579.png

Barua alizokuwa akiandika Mtwa Abdallah Mkwawa
Inategemea unaitazamaje historia ya Abushiri na umeisoma kutoka vyanzo gani?

Je ni kweli Abushiri alikuwa anafanya biashara ya utumwa?
Je kuna ushahidi wowote kuwa Abushiri alifanya biashara hii na Mkwawa?

Ngome ya Mkwawa ilishambuliwa kwa kupigwa mizinga kutoka upande wa Tosamaganga na leo hapo limejengwa kanisa kubwa na maarufu.

Hakuna uwezekano kuwa hii ni kumbukumbu kwa kuanguka kwa Mtwa Abdallah Mkwawa?

Kuwa wanahistoria wanaotafsiri hili kama moja ya kusafisha njia ya kuingiza ukoloni kwani wamishionari walifuatiwa nyuma na wakoloni.

Lakini kuna wanahistoria wanatazama athari ya kusilimu kwa Mkwawa na matokeoa yake.

Je Uislam ulienea baada ya kifo cha Mkwawa au ulishindwa kukua?

Manispaa ya Iringa ina misikiti 25 yote inasaliwa Sala ya Ijumaa na mkoa mzima una misikiti 80.

Baadhi ya wanahistoria wanajiuliza nini ilikuwa athar ya kusilimu kwa Chief Mkwawa?

Ingekuwaje kama Mkwawa angekufa mpagani?

Laiti Abushiri angekuwa ''dubwana la hovyo'' (ovyo) asingeweza kuwa na usuhuba na Mtwa Mkwawa kiasi cha kumtia katika Uislam na kumfunza kusoma na kuandika.

Wazalendo hawa wawili wote wameacha historia kubwa ya vita vyao na Wajerumani.

Pamphlet ama vitabu? Mkuu binadamu sisi tulivyo huwezi ukanichukua mimi utumwa ukanitesa ukanipeleka sehemu ukanifanyisha kazi, usinilipe etc nikakutii tu Haiwezekani.

Ndio maana weusi wengi waliopelekwa Marekani kinguvu waliasi na kupigana vita. Kuna vita vingi mno.

Hii ni website ya Taifa? Wameelezea vizuri sana nakushauri soma

Mbona utumwa inafahamika kwa kila mtu anayejua historia kuwq ni biashara ya ukatili
Vitabu vingi tu vinaeleza, hii website sijapata muda wa kuisoma yote, lakini sijaona waliosema watumwa walikuwa treated vizuri
Kuna kitabu cha simulizi kutoka kwa mtumwa mwenyewe akieleza ukamataji, usafirishaji, uuzwaji sokoni ilivyokua na jinsi biashara hiyo ilivyookomeshwa
Biashara ya utumwa imekomeshwa miaka mwishoni mwa karne ya 19, so kuna watumwa na watoto wa watumwa wengi tu waliokuwa hai na kueleza masaibu yake
Ama kwako huyo atakua mwongo?
 
Unalopoka sana, unayajua madhara ya utumwa wew? Umezaliwa juzi tu na kusoma vijitabu vilivyochakachua historia alafu huoni madhara ya utumwa? , rudi vijijin huko kuna wazee wanahistoria kamili jinsi wazazi wao walivyobakwa+kulawitiwa adharani, kuuwawa na wengine kukatwa viungo vya mwili ikiwa kama adhabu, wengineo kunajisiwa na wanawake kutolewa mimba bila kusahau kuhasiwa kwa wanaume ili kuzuia uzao wao kuongezeka.

pili toka nje ya box kuna vitabu na nyaraka nying zinazofichua maovu ya wakoloni na utumwa kiujumla.

Jambo alilotendewa muafrika ni baya ambalo hakuna jamii yoyote hapa duniani imewahi kutendewa, according to the real history.

Tuliyofanyiwa watu weusi kama wangefanyiwa wazungu+waarabu ungeona ambavyo wangepromote na kuzusha mengi ili wapate fidia na attention ya dunia, mfano kwa wale wayahudi feki waliozusha kuteswa na hitra na kuuwawa wayahudi mili6 kumbe hawakuzidi hata mia6, lkn unaona wanavyozusha propaganda za kuonewa kuwa walikuwa matesoni na utumwani blah blah nyingi zisizo na ushahid, lkn muafrika kafanyiwa unyama mwingi na ushahidi upo je kuna nguvu yoyote ya kujitetea dhidi ya hao wahuni?

Someni historia jmn watu weupe ni washenzi wa kila kitu hapa dunian no matter wamekusaidia nn lkn ushenz wao uko pale pale.
Mbona si kazi Ngumu mkuu lete Ushahidi, waarabu wanapendwa ukanda wote wa Pwani na waarabu siku zote hawakai pamoja, unakuta kijiji kimoja Kuna Familia moja tu ya Kiarabu, Angalia Tanzania nzima walivyotawanyika, ingekua hawa jamaa ni makatili wamgeshauliwa siku nyingi tu. Hii historia mkuu ina ukakasi sana na kukosekana vitabu vya Academic kuiprove inaonesha ukakasi wake ulivyo
 
Baba...
Nimeingia katika hiyo website.

Sijui kwa nini wenyewe wameweka nembo ambayo inaashiria ni website ya serikali ya Jamhuri ya Tanzania.

Nimeipitia kwa haraka na nimeona makosa katika ukweli na lugha.
Mzee wangu nashukuru, unaweza ukatu point vitabu vizuri vinavyoelezea hii issue?
 
Mbona utumwa inafahamika kwa kila mtu anayejua historia kuwq ni biashara ya ukatili
Vitabu vingi tu vinaeleza, hii website sijapata muda wa kuisoma yote, lakini sijaona waliosema watumwa walikuwa treated vizuri
Kuna kitabu cha simulizi kutoka kwa mtumwa mwenyewe akieleza ukamataji, usafirishaji, uuzwaji sokoni ilivyokua na jinsi biashara hiyo ilivyookomeshwa
Biashara ya utumwa imekomeshwa miaka mwishoni mwa karne ya 19, so kuna watumwa na watoto wa watumwa wengi tu waliokuwa hai na kueleza masaibu yake
Ama kwako huyo atakua mwongo?
Kitabu gani mkuu? Na Hio website wala haisemi wamekua treated vizuri tu, bali inaelezea vitu ambavyo vina Make sense.

Mfano kwenye Mashamba walipewa eneo la kujikimu, siku kadhaa analima shamba la master na siku kadhaa analima shamba lake na anaweza akauza mazao yake kupata hela ya matumizi yake. Still ni mfumo wa kinyonyaji ila Binadamu anaweza vumilia.

Tofauti na chumvi ambazo zinaongeawa as if hao Watumwa walikua ni ma robot.
 
Mzee wangu nashukuru, unaweza ukatu point vitabu vizuri vinavyoelezea hii issue?
Baba...
Nifahamishe ''issues'' unazotaka kuzijua.

Ikiwa najua vitabu nitakuelekeza na pia naweza hata mimi nikakueleza baadhi ya mambo katika hizo ''issues.''

Halikadhalika kuna elimu kubwa sana mitandaoni unaweza kufanya ''search.''
 
Back
Top Bottom