Kumbe ACT-Wazalendo wamepanga nyumba ya Maalimu Seif

Yaani ACT kimegeuka kuwa CHAMA cha mchongoo.hii inchi inazama.mh.zitto umeanza kuchonga mzinga mapemaa saaana Aiseeeee.
 
Tindo uko sahihi lakini je ni wangapi nje ya chama wanajua vipaumbele vya CHADEMA? Kama CCM kipaumbele chao ni kujenga ikulu nyingine kubwa Dodoma huku kukiwa na udumavu mkubwa wa huduma za msingi za kijamii CHADEMA inaweza kuwa na mtazamo tofauti na hilo
Mengine yote ni ishu za kawaida za maisha kila mmoja anapambana kivyake kujiongezea kipato
 
Yaani ACT kimegeuka kuwa CHAMA cha mchongoo.hii inchi inazama.mh.zitto umeanza kuchonga mzinga mapemaa saaana Aiseeeee.
Baada ya vyama vya TLP, NCCR, CUF kushtukiwa na wananchi kwa unafiki na usaliti wao, CCM wanaiandaa ACT kuchukua nafasi.
 

Suala la ofisi yenye hadhi ya CDM halina mjadala kwenye kipaombele. Ni kweli kuna vipaombele vingi hilo sikatai, lakini ofisi yenye hadhi ni jambo la lazima wala sio suala la vipaombele. Kwenye hili wala hunitoi kaka na story za vipaombele. Ofisi nzuri ni taswira ya chama au taasisi yoyote ile.
 
Baada ya vyama vya TLP, NCCR, CUF kushtukiwa na wananchi kwa unafiki na usafiri wao, CCM wanaiandaa ACT kuchukua nafasi.

ACT ilikuwa project ya CCM wakati wa kina JK kupambana na CDM. Hukumbuki ACY ikiwa na mwaka tu uchaguzi wa 2015 ilisimamisha wagombea wa ubunge na udiwani nchi nzima ikiwa haina vyanzo vyovyote vya mapato vinavyoeleweka. Na baada ya uchaguzi ule zikafungwa zote?

Waasisi wa ACT ni JK, Membe, Mwigulu, Nape, January nk. Ndio maana ilikuwa rahisi Membe kugombea urais kupitia ACT. Kilichosaidia ni Maalim Seif kumtosa Membe maana alijua ni kama Lowassa na kumkubali Lisu. Ukifuatilia vizuri utakuta kabisa pesa za ACT zinatoka CCM, na anapewa Zito kwa mission maalum, hao Wapemba wameingizwa mkenge na Zito bila kujua nini kinaendelea. Na Wapemba wakiona hizi kelele wanadhani ni ugomvi binafsi wa Zito na CDM bila kujua wanatumika.
 
zombi la lumumba umetumwa
 
OK naomba kwenye hili tukubaliane kutokubaliana
 
Mkuu Tindo sio Lumumba ila mtazamo wake kwa muda mrefu sana ni CDM kuwa na HQ yenye hadhi.

Nashukuru kwa kukiri msimamo wangu kwenye hili kwa muda mrefu. Kama tungejenga ofisi kipindi cha Magufuli mikutano ilipozuiwa, huku tukiwa na ruzuku kubwa, leo hii akina Mnyika wasingeingia kwenye maelezo ya kupanick baada ya ACT kufungua ofisi yao. Na hili la ofisi yenye hadhi ya CDM, halitaiacha taswira yetu vyema hadi tujenge. Kuna msemo usemao "kawaida ni kama sheria"
 
Tuko pamoja mkuu na mimi ni miongoni mwao tunaotaka HQ yenye hadhi ya chama kikuu cha upinzani.


 
utajua hujui

Mwala, ukivuka miaka 35 kama hujaoa ama kuolewa, jamii nzima itakushangaa na hata kukushinikiza uoe/uolewe. Sio kwamba ni lazima kuoa, ila hiyo ndio kawaida inayogeuka kuwa sheria isiyoandikwa. Hili la ofisi ya CDM yenye hadhi halitofautiani na hilo, mbali ya vipaombele vingine utakavyokuwa navyo. Huo ndio uhalisia wenyewe, hayo maneno mengine ya kihuni unayotumia hapa unaonekana punguani tu kutokana na ukongwe wako hapa jukwaani, na ufuasi wako kwa CDM.
 
Tindo umekua mpingaji sana wa chama lakini kumbuka ofisi zile kwetu sisi zinatosha sana Wala hatuna halaka ya kua na maofisi ya kifahali namkumbuka hata hao maccm wamejenga ofisi za pale chimwaga Kwa Kodi zetu wenyewe kipindi Cha msoga style je miaka yote walikua wapi? Au haya ni Kwa Chadema pekee? Tuwe tunaangalia kotekote
 

Sahihi kabisa mkuu, na iwe kweli, tuko tayari kuchanga kadiri ya uwezo wetu, na hela iende kwenye shughuli husika na sio kwingine na kwa sababu yoyote ile. Tunatoa credit za bure kwa jambo lililokuwa na lililondani ya uwezo wetu! Aibu iliyoje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…