Kumbe BongoFleva inalipa!! Diamond Platnumz anaingiza Milioni 200 kwa mwezi kwa matangazo tu

Kumbe BongoFleva inalipa!! Diamond Platnumz anaingiza Milioni 200 kwa mwezi kwa matangazo tu

Sawa Mkuu nakubaliana na wewe ila hii ipo tofauti kwa Bilionea Dayamondi....Uwezo wa Kujenga Mansion la hatari anao lakini nashangaa hajajenga bado!! Ukiachana na nyumba za kuwavua watu za mil 20 au 25 au Nyumba ya Mama yake Madale ya kukaa yeye naona hana,nina amini uwezo wa Kujenga anao labda anajenga kimya kimya.
Hivi mkuu huo mjengo wa Madale ni mjengo wa maana sana au ya kawaida tu.

Maana hata picha yake sijawahi iona. Kuna ule mjengo alimnunulia Zari South, uko vizuri.
 
Mbona haushangai wahindi kibao wana maviwanda na investments nyingi tu hapa bongo lakini wanaishi nyumba za kupanga za NHC?

Acha story za vijiweni mkuu ,wahindi wanakaa NHC kwasababu biashara zao zipo hapo hapo town ila wana beach plots kibao mbweni na kigamboni.....Angalia Jumapili wanavyoenda kwenye mijengo yao kula upepo!!! Mkikaa vijiweni mnaongopeana sana!! Subash Mwenyewe alikuwa na Mijengo kibao town.
 
Mbona hata Diamond alipopanga nikaribu na office yake ya Wasafi media
 
Lakini mkuu hiyo ishu ya kupanga ni kweli au propaganda ?kweli diamond hadi leo hajajenga? Kama hajajenga kuna something wrong
Wabongo akili zetu tumezimarginalize kwenye ishu ya kujenga kwamba ndo indicator ya maendeleo ya mtu......huyu mwamba ana nyumba sehemu hapa Dar....juzi kati kanunua hoteli mikocheni,kanunua nyumba kunduchi. Ni kweli anaishi nyumba ya kupanga katika location ya kistaa
 
unamaana hana nyumba, gari pesa nk inamaana zile Show zote ni feki L, TV Radio fake, Wcb ni fake wasanii waliochini tae ni midori au mimi ndio sielewi

Basi kwamantiki hii Tz hakuna mwenye pesa
Hivi unafikiri ile mitonyo yote inayotolewa kwenye show zake mkwanja wote unaingia kwenye mfuko wake?

Kuna watu wengi wako behind waliowekeza kupitia jina lake kwasababu ya umaarufu wake ambao kwenye swala la mgao wakisha jisevia wao zinazobaki wanarusha juu, hizo ndio anadaka diamond
 
wanaume na midevudevu yenu mnabishania pesa ya mwanaume mwenzenu mara oooh"hana nyumba kapangisha, alisema atanunua rozi rozi mpaka leo hajanunua, etc" seriously!!!? 😂😂😂🙌🚮

Mwenye pesa hana tantalila au longo longo ,Mwenye pesa unaona tu actions zake! Tunachosema hapa ni kuwa huyo bwana mdogo kutufanya sie mapoyoyo na uongo uongo wake,kama pesa anazo atulie ni zake sio kupayuka payuka tu anaingiza sijui mili 220 kwa mwezi,hivi anajua mili 200 kwa mwezi?
 
Hivi kwanini hakununua nyumba za 900 itapendeza. Na bado analipa kodi
 
Swali ni,analipa kodi..?,analipa Sumatra,osha,amrefu,Nemki etc?
 
Mkwe wangu alistaafu mwaka jana na alikua senior officer serikalini akaramba mafao ya mil 500
Hii ni sawa na miezi miwili tu ya huyu chizi
Kweli maisha hayajawahi kuwa fair
Ila milioni 500 ni nyingi,atakufa vizuri,,mimi nilipostafuu nililipwa jumla milioni 18
 
Lakini mkuu hiyo ishu ya kupanga ni kweli au propaganda ?kweli diamond hadi leo hajajenga? Kama hajajenga kuna something wrong
Ni kweli amepanga lakini sio kwamba hana nyumba! Usisahau ana ile nyumba ya Madale ambayo alikuwa anaiita State House lakini baadae akamwachia mama ake. Nadhani anachokwepa, kujenga nyumba nyingine ya status yake itabidi imtoke pesa sana; sasa mtu ukishakuwa na mawazo ya kibiashara, unaona uwekeze 1B au hata 500M kwenye kujenga, si bora hiyo pesa u-invest kwenye biashara kisha ulambe faida yake! Ni kama Wahindi tu!
 
Msanii wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema kila mwezi huingiza Sh200 milioni kutokana na kuingia mikataba na kampuni mbalimbali kuwa balozi wa bidhaa zao.

Akizungumza katika kipindi cha TheSwitch kinachorushwa na redio ya Wasafi leo Alhamisi Januari 28, 2021, Diamond amesema fedha hizo ni mbali na zile anazoingiza kupitia muziki.

Amebainisha kuwa anaingia mikataba na kampuni na amekuwa akifanya hivyo kwa kila kampuni inayohitaji huduma yake.

“Endosment zangu mimi mshahara wangu kwa mwezi si chini ya milioni 200, na tunasaini mikataba kila siku. Ninaingiza kwa wiki Sh55 milioni kwa siku Sh7 milioni kwa saa moja Sh300,000 na kwa sekunde Sh6,000.”

Amesema mwaka 2021 fedha anazozipata katika eneo hilo huenda zikaongezeka kwa kuwa anatarajia kuwa balozi wa vitu vingi zaidi kwa kuwa ameamua kufanya muziki kuwa kazi na biashara.

View attachment 1689019
=====

Ina maana hii ni kwa endorsement za matangazo tu
Usanii unalipa ndio maana maccm hayaachi usanii kila wakati wa uchafuzi mkuu
 
unamaana hana nyumba, gari pesa nk inamaana zile Show zote ni feki L, TV Radio fake, Wcb ni fake wasanii waliochini tae ni midori au mimi ndio sielewi

Basi kwamantiki hii Tz hakuna mwenye pesa
Na kwa tafsiri yake, hata zile endorsements za Pepsi, Luc Belaire, Coral Paints, ile ya ku-Bet; zote hizo ni fake bila kutaja endorsements za miaka ya nyuma! Hata ile habari waliyotoa YouTube wenyewe kwamba amefikisha Views 1B na yenyewe itakuwa ni habari fake kwahiyo haina haja ya kujua kwenye hizo views kaingiza dola ngapi!! Lakini yote kwa yote, watu hatufahamu kwamba hata duniani wanamuziki wanaingiza pesa nyingi sana kupitia endorsements, na Mond ana bahati ya kupata endorsement ya kampuni kubwa kubwa.
 
Jamaa wanaandika utumbo kama hawana ubongo yani
 
Hivi unafikiri ile mitonyo yote inayotolewa kwenye show zake mkwanja wote unaingia kwenye mfuko wake?

Kuna watu wengi wako behind waliowekeza kupitia jina lake kwasababu ya umaarufu wake ambao kwenye swala la mgao wakisha jisevia wao zinazobaki wanarusha juu, hizo ndio anadaka diamond
Nonsense Hata billgate kuna watu kibao nyuma yake sisi tunaangalia anapata ngapi
 
Back
Top Bottom