Kumbe hata Ulaya hakuna Uhuru wa kutoa Maoni, Wanaounga mkono Hamas na kuikosoa Israel wanapigwa rungu

Kumbe hata Ulaya hakuna Uhuru wa kutoa Maoni, Wanaounga mkono Hamas na kuikosoa Israel wanapigwa rungu

Kuna wahuni wa kiarabu ulama so dawa ni kuwapiga home and away.
 
Kwa nini wavamie?
Madai ya hiyo nchi kuwa ni yao na sio ya Wayahudi mbona hayazingatiwi?
Leo hii, wewe ukianza kusema Comoro ni nchi ya Watanzania, nani atazingatia?

Ufahamu kuwa hakujawahi kuwepo nchi inayoitwa Palestina, hata kabla ya Umoja wa mataifa kuundwa.

Katika ramani ya Ulimwengu wa kale, Wayahudi walimiliki nchi ya Kanani ambayo kwa sasa inajumuisha eneo lote la Israel, eneo lote la Wapalestina, na baadhi ya maeneo ya Lebanon, Jordan na Syria.

Kabla ya Yesu, eneo hilo lilikuwa na Israel kingdoms 2, moja ikiitwa Israel, na ya pili ikiitwa Judea. Na hawa wanaoitwa Wapalestina, kiuhalisia ni Wayahudi walioishi eneo la Judea, jina linalotokana na Yuda, mtoto wa kwanza wa Yakobo.

Hawa Wapalestina na Wayahudi ni ndugu wanaofarakanishwa na Iran. Bila Iran, haya yanayotokea yasingekuwepo. Iran ndiye shetani anayewamaliza Wapalestina na Wayahudi.
 
Bila shaka mkoa Pouwa Kabisa.

Nilidhani ni hukuhuku kwetu Mambo ya kupigana rungu la mdomo, kuzibana na kukabana makoo ili Watu wasizungumze labda kuhusu jambo fulani.
Wanaharakati na wapiga domo husemaga nchi yetu na nchi za Afrika hakuna Demokrasia ikiwemo uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

Lakini kumbe hata Ulaya mambo ya kupigana rungu la mdomo yapo. Vita inayoendelea huko Mashariki ya Kati baina ya Israel na Palestina (Hamas) imezifanya nchi za Ulaya kuichana Demokrasia kwa wale ambao wanaiunga Mkono Palestina (Hamas).

Wanahubiri kile wasichokifanya. Na hiyo ni dalili ya Unafiki.
Habari za Karim Benzema na wachezaji wengine walioiunga mkono Hamas( maana yake kuipinga Israel) wamejikuta katika kunyimwa haki zao za kujieleza kama nchi hivyo zinavyojiita nchi za kidemokrasia.

Je hiyo ndio demokrasia?

Kama wanaruhusu mtu kushabikia au kufanya ushoga kwa nini iwe shida mtu kuwa upande wa Hamas? Kama wao wanashabikia Israel kwa nini wawazuie wanaoshabikia Hamas? Je hiyo ndio demokrasia?

Jioni njema
Tu na Le wasikie
 
Na wale wapiganaji wa ANC waliotaka kupewa haki na uhuru kwa nchi iliyokuwa na Ubaguzi na ukandamizaji, wazungu waliwaita magaidi pia. Sisi kama nchi msimamo wetu tangu awali ni kuwaunga mkono Palestina kuondoa ukandamizaji na kuleta uhuru kama tulivyokuwa upande wa ANC. Msilete unafiki, kwamba Afrika kusini ni sawa lakini Paleatina hapana? Kaa sababu ni Waislamu? Haki ni haki tu
Tanzania haijawahi kuunga mkono kundi lolote la kigaidi. Tanzania haijawahi hata mara mpja kuiunga Hamas au Hizbollah. Tanzania iliwaunga mkono Wapalestina na PLO.
 
Hadithi tu hizi
Huyo sijui Ishmael au Isaka unamfahamu?
Vijisababu tu. Kama tukifuata hizo historia eti enzi za mitume sijui nani alimuoa nani! Basi itabidi wamarekani nao warudishe nchi ya asili ya wahindi wekundu. Israel ameikalia kimabavu Palestina na wakati anakaribishwa hakukuwa na hizi stori za Ishmael wala mchi ya ahadi
 
Kushabikia watu wanabaka, wanateka, wanachinja, wanaua wanawake na watoto lazma uchukuliwe hatua, hamna uhuru wa kuunga mkono magaidi wanaotangaza kuua wayahudi na wakristo
 
Leo hii, wewe ukianza kusema Comoro ni nchi ya Watanzania, nani atazingatia?

Ufahamu kuwa hakujawahi kuwepo nchi inayoitwa Palestina, hata kabla ya Umoja wa mataifa kuundwa.

Katika ramani ya Ulimwengu wa kale, Wayahudi walimiliki nchi ya Kanani ambayo kwa sasa inajumuisha eneo lote la Israel, eneo lote la Wapalestina, na baadhi ya maeneo ya Lebanon, Jordan na Syria.

Kabla ya Yesu, eneo hilo lilikuwa na Israel kingdoms 2, moja ikiitwa Israel, na ya pili ikiitwa Judea. Na hawa wanaoitwa Wapalestina, kiuhalisia ni Wayahudi walioishi eneo la Judea, jina linalotokana na Yuda, mtoto wa kwanza wa Yakobo.

Hawa Wapalestina na Wayahudi ni ndugu wanaofarakanishwa na Iran. Bila Iran, haya yanayotokea yasingekuwepo. Iran ndiye shetani anayewamaliza Wapalestina na Wayahudi.
Wacha uongo. Kabla ya 1948 hakukuwa na nchi inaitwa Israel. Soma historia vizuri uielewe. Eneo lote lile liliitwa Palestine.
Na hiyo baada ya kupewa hifadhi akaanza kuchukua maenwo kwa nguvu akisaidiwa na Waingereza na marekani kijeshi.
 
Na wale wapiganaji wa ANC waliotaka kupewa haki na uhuru kwa nchi iliyokuwa na Ubaguzi na ukandamizaji, wazungu waliwaita magaidi pia. Sisi kama nchi msimamo wetu tangu awali ni kuwaunga mkono Palestina kuondoa ukandamizaji na kuleta uhuru kama tulivyokuwa upande wa ANC. Msilete unafiki, kwamba Afrika kusini ni sawa lakini Paleatina hapana? Kaa sababu ni Waislamu? Haki ni haki tu
Well said! 👏
 
Unafikiri kukosoa kwa kutoa maoni ndo utaweza kukomboa nchi iliyokaliwa kimabavu? Kama ni hivyo basi tusingekuwa tumepata uhuru mpaka leo! Akina mkwawa unafikiri walivyokuwa wanapigana na wajerumani walikuwa "magaidi"?
Unalinganisha vitu tofauti kabisa.

Akina Mkwawa walikuwa wanapambana na Wajerumani waliotoka kwao huko Ujerumani na kuja kuikalia Tanganyika, wakichuma rasilimali na kuzipeleka kwao Ujerumani.

Swali:
Waisrael walitoka kwenye nchi yao ipi wakaenda kuikalia Palestina?

Hivi ikitokea wazazi wako walikuwa wanamiliki ardhi Tarime, ambako ni asili yenu. Lakini katika kutafuta maisha, wakaondoka wakaenda kuishi Dar kwa miaka mingi. Baadaye kiongozi mmoja mhuni akaanza kuwaua wahamiaji wote waliopo Dar, kisha wewe na ndugu zako ili kuokoa maisha yenu mkaamua kurudi kwenu Tarime, mkafika mkaona watu wamegawana maeneo yenu na kuyafanya yao, nanyi kwa hekima mkaamua kuongea nao ili kuyapata maeneo yenu ya asili, na maeneo mengine mpaka mkaamua kuwalipa pesa hao wavamizi. Mkakaa kwa amani. Wakatokea majirani shetani wakaanza kuwachochea hao watu mliowakuta kwenye maeneo yenu, eti wawafukuze ninyi kwa maana hamstahili kuwepo Duniani. Na baadaye majirani hao wakaunda vikundi vya kigaidi ili viawaue ninyi, utafanya nini?

Nimejaribu kuweka kwa lugha nyepesi ili uweze kuelewa.
 
Tanzania haijawahi kuunga mkono kundi lolote la kigaidi. Tanzania haijawahi hata mara mpja kuiunga Hamas au Hizbollah. Tanzania iliwaunga mkono Wapalestina na PLO.
Soma tena maelezo yangu. Ukiunga mkono PLO lakini huungi mkono Hizbollah ni sawa na kusema kwenye mseto unakula wali lakini choroko zinakuletea allergy!
PLO ni political wing ya Hizbollah
Unafikiri kule Mazimbu wapiganaji wa ANC walikuwa wanafundishwa nini? Amka.
 
Unaruhusiwa kutoa maoni yako lakini siyo kushabikia ugaidi au majanga ya kiasili. Ugaidi na majanga ya kiasili, ni calamities ambazo hazitakiwi kupata ushabiki. Una uwezo wa kukosoa au kutoa mawazo yako juu ya namna ya kuyashughulikia lakini siyo kuyashangilia.

Kuwashabikia magaidi na wewe unakuwa sehemu ya magaidi. Na kama ikidhihirika kuwa wewe ni sehemu ya magaidi utashughulikiwa kama magaidi wenyewe.
Mkuu hujui usemalo kwa muktadha huu! Ujumbe muhimu ni kuwa kupitia tukio la Hamas limewakumbusha ulimwengu maadhila wanayo pitia Wapalestina chini ya mabavu ya Israel!
 
Unalinganisha vitu tofauti kabisa.

Akina Mkwawa walikuwa wanapambana na Wajerumani waliotoka kwao huko Ujerumani na kuja kuikalia Tanganyika, wakichuma rasilimali na kuzipeleka kwao Ujerumani.

Swali:
Waisrael walitoka kwenye nchi yao ipi wakaenda kuikalia Palestina?

Hivi ikitokea wazazi wako walikuwa wanamiliki ardhi Tarime, ambako ni asili yenu. Lakini katika kutafuta maisha, wakaondoka wakaenda kuishi Dar kwa miaka mingi. Baadaye kiongozi mmoja mhuni akaanza kuwaua wahamiaji wote waliopo Dar, kisha wewe na ndugu zako ili kuokoa maisha yenu mkaamua kurudi kwenu Tarime, mkafika mkaona watu wamegawana maeneo yenu na kuyafanya yao, nanyi kwa hekima mkaamua kuongea nao ili kuyapata maeneo yenu ya asili, na maeneo mengine mpaka mkaamua kuwalipa pesa hao wavamizi. Mkakaa kwa amani. Wakatokea majirani shetani wakaanza kuwachochea hao watu mliowakuta kwenye maeneo yenu, eti wawafukuze ninyi kwa maana hamstahili kuwepo Duniani. Na baadaye majirani hao wakaunda vikundi vya kigaidi ili viawaue ninyi, utafanya nini?

Nimejaribu kuweka kwa lugha nyepesi ili uweze kuelewa.
Wayahudi walikuwepo tena walikuwa nchi nyingi ikiwemo Syria, Lebanon, Egypt, Iraq etc . Ni minority group kwa mashariki ya kati. Narudia tena, hakukuwa na nchi inaitwa Israel. Wala Wayahudi hawakuwa na kipande cha ardhi kinaitwa "nchi"
Walikaribishwa Palestine kupea hifadhi baada ya kuwa wanakataliwa kila sehemu.
Palestina pia kama walivokuwa kina mkwawa wanapigana kudai ardhi na mamlaka yao yaliyoporwa.
 
Tanzania tunawaunga mkono Palestine chini ya uongozi wa PLO. Hatuwaungi mkono Hamas

Hata kule SA tulikuwa tuna wsi ha mkono ANC na sio wale waliotangaza wazi kuangamiza Makaburu wote
Hatujawahi kutamka kuwa hatuwaungi mkono Hamas!
 
Unafikiri kukosoa kwa kutoa maoni ndo utaweza kukomboa nchi iliyokaliwa kimabavu? Kama ni hivyo basi tusingekuwa tumepata uhuru mpaka leo! Akina mkwawa unafikiri walivyokuwa wanapigana na wajerumani walikuwa "magaidi"?
Atamke hadharani tumsikie kuwa Akina mkawa walikuwa magaidi!
 
Nanukuu
Kama wanaruhusu mtu kushabikia au kufanya ushoga kwa nini iwe shida mtu kuwa upande wa Hamas?

Hapa umelinganisha makundi mawili tofauti I
Hamas kwa mtazamo wangu ni magaidi
Na mashoga ni was..ge
 
Back
Top Bottom