Kumbe hii miaka yote Man City anatudunda alikuwa anatumia njia za wizi wizi

Kumbe hii miaka yote Man City anatudunda alikuwa anatumia njia za wizi wizi

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
11,191
Reaction score
35,870
170100.jpg
 
Ndo maana kina de bryne, fernandinho, Sane, sterling, jesus sasa hivi yanacheza mpira wa hovyo kwasababu ni malipo ya huu "uwizi". Na lili likocha lao pep baguzi kumbe jizi tu.
😁😁😁😁
 
Hii kesi mwisho wake ni mbaya sana kwa city, hii kesi ukiangalia ni masuala zaidi yakimapato na matumizi yake pamoja na uwazi ila uwanjani jamaa walipata walichostahili tofauti na ile calciopolli scandal ya Italy ambapo Luciano moggi director wa Juventus kipindi kile alikuwa anaonga marefarii ili kupata favourable treatments ila city uwanjani walipata ushindi halali ila wame breach financial conduct
 
Hoja ya mashabiki wa city ni utasikia kwani si tuliwafunga uwanjani.

Unagundua hawa watu hata hawaelewi kitu.

Hivi kipindi hichi ambacho city inamuuza Savinho kwa 85M ni kipindi cha wao kumnunua Haaland kwa 60M? Inaingia akilini?
Fafanua hiyo aya ya mwisho mkuu nopate kujifunza, sijaelewa
 
Fafanua hiyo aya ya mwisho mkuu nopate kujifunza, sijaelewa
City ilimnunua Savinho kutoka Troyes kwa 30M.

Kipindi chote alichokaa City amefunga magoli 7. Amekaa miaka 2.

City imemuuza Savinho kwenda Spurs kwa 85M.

Ila Haaland, goalscorer wa viwango vya dunia, City ilimnunua kwa 60M.

Kabla Haaland hajaenda City alikua amecheza mechi 89 na kufunga magoli 86.

Huo ni mfano wa transfers ambazo City imezifanya. Angalia kwa Marmoush n.k.

Hiyo inaingia akilini?

Hii ndiyo inaonyesha wanaripoti taarifa za uongo ili kubalansi vitabu. Hizi taarifa za uongo ndiyo zinafanya wana advantage ambayo hawakutakiwa kua nayo.

Newcastle ina wamiliki wana mpunga mnene ila wamelazimika kuuza Bruno, Tonali, Gordon, siyo kwa kupenda. Ni rules, hizo rules ndiyo City ilikua inazizunguka kwa uongo.
 
Jipya jingine lililoibuliwa na hii tume ni kwamba wanaingia mkataba na sponsor halafu sponsor analipa sehemu ya kiasi kinachoonekana kwenye mkataba halafu kingine wanalipa wenyewe City.

Yaani mfano wanaingia deal na Azam TV la Bilioni 10, Azam TV wanatoa Milioni 20 halafu Bilioni 9 na Milioni 980 zinalipwa na City wenyewe.

So kwenye vitabu wanaonyesha wamedhaminiwa Bilioni 10 na Azam TV kumbe ni uongo.
 
Kwann walikiwa wanafanya hivyo sasa?
 
Back
Top Bottom