Castr
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 39,203
- 79,500
Kuna rule inaitwa financial fair play.Kwann walikiwa wanafanya hivyo sasa?
Idea ni kwamba timu itatumia inachoingiza.
Yaani mfano viingilio, manunuzi ya jezi, udhamini, mauzo ya wachezaji n.k. ndiyo vinatakiwa kua chanzo cha kipato watachotumia.
Sasa hii ni kuzuia timu zenye wamiliki wenye pesa wasitoe pesa zao mfukoni na kudhamini vilabu vyao.
Timu kama City ukilinganisha na United au Arsenal au Liverpool haiwezi kuvutia udhamini wa wadhamini wakubwa, haiwezi kuuza jezi nyingi na haiwezi kujaza uwanja. So inabidi waonyeshe wameuza kwa bei kubwa mchezaji na ni uongo, inabidi waonyeshe wamedhaminiwa pesa nyingi na ni uongo.