Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Utaratibu wa sasa hivi ambao umeanza mwezi April 2021 hakuna stika ya bima na maelekezo yote yalitolewa kikao cha usalama barabarani na mawakala wa bima. Hivyo basi kosa ambalo umeandikiwa ni batili halipo,bima zote husoma online ninahisi huyo trafiki ni mgeni hajui utaratibu mpya.Mtafute ukaikatae hiyo faini ailipie mwenyewe
 
Manjagu wao hukomaa na Stika, mimi kuna kipindi nimeshawahi kuweka Stika feki wakati sina hata Bima Manjagu wakaingia kingi miezi sita mpaka nilipopata mlungula ndio nikanunua Bima Orijino.
 
Sasa makampuni yamebadili utaratibu kwann yeye alazimishe kutumia kanuni za zamani za kubandika stika na stika hazipo....

Ungemuuliza wakuu wako wa kazi hawajakwambia kuhusu utaratibu mpya au umeamua kuwa tapeli kwa kutumia vazi la uaskari....??!
Sheria iko listed kwenye machine, unakataaje
Tatizo ni hiyo sheria kwa nini haijatolewa

Ukipigwa faini ni lazima utailipa tu hata kama sio sawa
 
Wana JF

Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo. !

Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakua hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika

Waziri husika tunaomba uliangalie hili.
Wewe na askari wako hampo updated, kila kitu cha gari siku hizi kina digital copy, hata yeye askari akiamua kukagua bima ya gari lako , anahitaki namba tu kujua validity ya bima , ile ya kubandika kwenye kioo imepitwa na wakati hata askari wenyewe wanajua
 
Niwekee namba ya huyo Askari na control namba yake kesho atailipa hiyo fine kwa pesa yake ya mfukoni.. na kama alikulazimisha hongo andaa ushahidi kesho itakuwa mwisho wake wa kazi... pia usisahau kutuma namba ya gari lako... Askari kama wote wenye akili kama Yule mkuu wa mkoa aliyetumbuliwa wataenda kaa bench pamoja... ila kama ni uongo acha kusambaza taarifa za uongo na kupaka matope jeshi
 
Unatakiwa uprint, na uwe copy yake ndani ya gari kama kadi ya gari.
Ni sheria kubandika stika, kuwa na copy bila kubandika kwenye kioo ni kosa kisheria
 
Wewe na askari wako hampo updated, kila kitu vha gari siku hizi kina digital copy, hata yeye askari akiamua kukagua bima ya gari lako , anahitaki namba tu kujua validity ya bima , ile ya kubandika kwenye kioo imepitwa na wakati hata askari wenyewe wanajua

Mkuu askari alikagua BIMA kwa machine na kukuta gari kweli ilikua na bima
Tatizo ni kutokuibandika stika kwenye kioo, ni KOSA kisheria na lipo katika moja ya faini za magari kwenye zile machine walizonazo Traffic .!
 
Mkuu askari alikagua BIMA kwa machine na kukuta gari kweli ilikua na bima
Tatizo ni kutokuibandika stika kwenye kioo, ni KOSA kisheria na lipo katika moja ya faini za magari kwenye zile machine walizonazo Traffic .!
Kuna sheria zinabadilika automaticaly zamani kweli ilikuwa lazima akague sticker , na watu walikuwa wana foji sana hizi sticker , siku hizi stiker haina maana na haisadii chochote zaidi ya kuweka uchafu pale kwenye kioo,
Vitu vipo online
 
Kuna sheria zinabadilika automaticaly zamani kweli ilikuwa lazima akague sticker , na watu walikuwa wana foji sana hizi sticker , siku hizi stiker haina maana na haisadii chochote zaidi ya kuweka uchafu pale kwenye kioo,
Vitu vipo online
Sheria haijabadilika, Askari akiamua kukuandikia atakuandikia na utalipa.

Msipotoshe watu, Sheria bado ipo palepale.

Kinachopaswa kufanywa ni kubadili hiyo sheria
 
Siku hizi stika za kubandika kwenye kioo za Bima hazitolewi manake waliona mastika Mengi ni feki.
Wewe na huyo traffic wote mtakuwa vilaza
Insurance siku hizi inaangaliwa kidigitali
 
Sheria haijabadilika, Askari akiamua kukuandikia atakuandikia na utalipa.
Msilotoshe watu, Sheria bado ipo palepale.
Kinachopaswa kufanywa ni kubadili hiyo sheria
Mbona Bina wenyewe ndo wanatueleza utaratibu umebadilika?
Na stika hatupewi kwa kweli
 
Back
Top Bottom