Wana JF
Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.
Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo. !
Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakua hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika
Waziri husika tunaomba uliangalie hili.