Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Issue sio kutokua na BIMA, issue ni sheria inayokutaka lazima ubandike stika ya BIMA hata kama unayo ndani ya gari traffic ana haki ya kukuandikia faini
Mkuu mbona umekomalia kuwa kuna sheria yq kubandika stika ya bima? Sheria wanayoitumia trafiki ni ile ya kushindwa kuweka alama za utambulisho ndo wanakuchanganyia na bima hapo. Hakuna sheria inalazimisha kuweka stika ya bima

Na kwa sasa stika hazitumiki tena. Huyo alikua na yake tu

Sema ndo hivyo trafiki akitaka kukuanfikia kuna sheria nyingi zimekaa kiuchochoro anapitisha makosa mengine kwenye vifungu vya jumla jumla
Ukweli hyo sheria ipo, inataka sticker ibandikwe mahala ambapo panaonekana. Lakini nadhani traffic nae ni kilaza regardless of sheria, kuna mabadiliko ambapo sasa hivi sticker hazitolewi ni kama zimekuwa digitalized kwa hyo inaonekana online.

Kutokua na sticker sio kosa lako ila la serikal kutobadilsha hyo sheria. Mtata kama mimi hiyo fine atalipa hiyo traffic mwenyewe.
 
Usitetee usivyovijua
jambo nyeti siwezi andika namie nionekane nimeandika maana hili ni jambo la elimu, so nilichokandika ni kile ninachokifahamu baada ya kusoma hiyo sheria ya usalama barabarani ka unajua zaidi unaweza nielimisha maana sijajiwekea mpaka wa kupokea
 
Mkuu askari aliverify uhai wa BIMA kupitia machine na kukuta kweli BIMA ni halali, Sheria aliyotumia yeye kunipiga fine ni kuwa sijabandika stika kioo cha mbele upande wa kushoto.

Hii ni sheria imeorodhoshwa kwenye machine zao.
Sijakataa na sijui kama umenielewa ! Ni sheria lakini iliyopitwa na wakati Askari mwerevu asingekupiga fain
Mfano sheria ya kunyonga watuhumiwa , marais karibia wote wamekua wakikwepa sana kutia saini kwa sababu ya busara
 
sheria ya usalama barabarani inataka ubandike tena kioo cha mbele kushoto ha haaaa tusome sheria japo tunapokuwa tumeama vizuri la sivyo tutapigwa sanaaa
Ilipitwa na wakati hiyo sheria
 
Issue sio kutokua na BIMA, issue ni sheria inayokutaka lazima ubandike stika ya BIMA hata kama unayo ndani ya gari traffic ana haki ya kukuandikia faini
Nitaitoa wapi hiyo stika Bima wenyewe wanatoa karatasi la A4 tu?
 
Tatizo ni kubandika stika ya BIMA kwenye kioo, NI sheria kabisa na yeye alinionyesha inakutaka kubandika stika.
Hiyo sheria ilikua sahihi wakati stika zinatolewa. Sasahivi hazitolewi, utabandika stika gani?
 
Umepigwa kwa ubwege wako... mimi kama nmeshakata bima na nina tembea na ile document ya kulipia ..hakyanani ntaenda kulala polisi mimi binafsi kioo cha gari ni cheupe pee maana hakina stika hata moja sio ya nenda kwa usalama wala ya nn...
Tuko pamoja mkuu. Kama askari anataka kuhakiki, ni jukumu lake kuingiza registration number ya gari T123 XYZ kwenye machine yake itampa status ya BIMA. Kama hilo linawapa shida kulifanya, wasitusumbue sisi. Wapeleke maoni yao kwa walioleta huo utaratibu.
 
Wana JF,

Leo nlisimamishwa na traffic, akakagua kioo na kukuta sina stika ya BIMA, alivyoniuliza nikamwambia BIMA nshakataa mtandaoni, na kwenye system ya TIRA MIMS inaonyesha gari tayari nina BIMA.

Ila kilichonishangaza zaidi ni kuwa huyu jamaa aliniandikia faini, kosa langu ni KUTOKUBANDIKA STIKA YA BIMA kwa kioo cha gari. Kwa kweli hili limenishangza sana kwamba sasa tuna uwezo wa kukata bima kwa simu, na kupata bima yako instantly .! Ila sheria za traffic bado zinatubana kwamba ni lazima ubandike stika ya bima kwenye kioo!

Sijajua ni nani mwenye jukumu la kubadilisha hii sheria ila ni moja ya sheria ya kijinga sana kuendelea kuwepo, maana kunakuwa hakuna maana ya vifaa vya traffic kuunganishwa moja kwa moja na mfumo wa TIRA kama bado sheria inataka nibandike stika.

Waziri husika tunaomba uliangalie hili.
Tena sio tu kubandika tu popote kama wabishi wengine wanavyobandika kwenye vioo vya pemebeni,ni kubandika stika kwenye kioo cha mbele cha gari lako...
 
Tuko pamoja mkuu. Kama askari anataka kuhakiki, ni jukumu lake kuingiza registration number ya gari T123 XYZ kwenye machine yake itampa status ya BIMA. Kama hilo linawapa shida kulifanya, wasitusumbue sisi. Wapeleke maoni yao kwa walioleta huo utaratibu.
Exactly
It all boils down to elimu, askari wengi ni shida vichwani
Tra kwa mfano toka vitu viwe online hawahangaiki tena na stickers , wao akiomba kadi tu , anamaliza kila kitu kwenye system, kama ni wa kudaiwa au kuruhusiwa uendelee na safari
 
Wewe bado hujaelewa, hakuna Sheria inayokufa sababu ya kukua kwa technology
Ukitaka sheria ife basi ni lazima ifutwe, na hiyo Sheria bado ipo haijafutwa.
Umetoa mifano ya vitu ambavyo havihusiani, ungetolea mfano wa Sheria fulani kufa sababu ya technology
Sijasema sheria imekufa mkuu dont qoute me wrong!!
Nimesema sheria zilizopitwa na wakati zinahitaji busara
Tra kwa mfano hawahangaiki na stickers tena kwa sasa na kule wanaajiri wasomi,.
 
Huyo trafiki katumia ubabe tu kukulipisha kwa kosa ambalo limepitwa na wakati na pia ni la utata tu, maaana hiyo stika kama inavyoainaishwa kwenye sheria haitolewi tena kama zamani, kwa hiyo hakuna stika ya kubandika inayotolewa na bima na huwezi kubandika makaratasi ambayo unapewa na bima kwa vile makaratasi hayo sio stika.
 
Unalipaje faini wakati bima unayo? weee jamaa veepe.......mwambie akupeleke mahakamani.
 
Je wajua? Hauhitajiki kubandika stika ya bima kwenye chombo cha usafiri. Tumia VodaBima upate stika kwa SMS inayotambulika na mamlaka zote. Kununua, Piga *150*00# >Huduma za kifedha>VodaBima.
 
Utaratibu haufuti Sheria, Bali Sheria ndio hufuta utaratibu.
Sheria ndio zinaongoza nchi
Sasa nani mwenye makosa hapo?
Maana wenye dhamana ya kutoa sticker wameelekezwa haina haja ya kutoa hivyo hawatoi.

Kwanini tusipaze sauti huu wizi ukakoma
 
Mkuu askari aliverify uhai wa BIMA kupitia machine na kukuta kweli BIMA ni halali, Sheria aliyotumia yeye kunipiga fine ni kuwa sijabandika stika kioo cha mbele upande wa kushoto.

Hii ni sheria imeorodhoshwa kwenye machine zao.
Hukubandika kwakua ulikua unajua inakupasa ubandike au hukubandika kwakua ulipewa utaratibu mpya?
 
Back
Top Bottom