Nimesema askari na mtoa mada hawapo updated , sijasema kwamba sheria hiyo haipo. Kuna vitu vinakufa automatically kwa sababu ya technology, ni swala la kutumia tu common sense.
Ni kama vile vocha za kukwangua, haijakatazwa na ipo, lakini kwa wanaojielewa, hakuna sababu ya kununua vocha ilhali kuna uwezekano wa kununua muda wa maongezi na vifurushi kupitia m pesa and the likes
Kada ya Askari kwa wengi ni option ya failures, na ndio sababu tunasumbuana barabarani kwa vitu ambavyo hata havina maana.
Hapo zamani kabla ya mambo ya technology, njia pekee ya kujua uhai wa bima ilikuwa ni kupitia hiyo sticker, na ndio iliwekwa hiyo sheria, siku hizi hata wewe mwenyewe unaweza kulifanya hilo kupitia simu ya mkononi.